Kombe la Dunia 2018: 'Own Goal' anaongoza kwa mabao baada ya mechi 17

Chanzo cha picha, Getty Images
Cristiano Ronaldo, Lionel Messi Neymar na Harry Kane wana mpinzani mpya kombe hili katika azma yao ya kutwaa kiatu cha mfungaji bora Urusi 2018.
Wanawania tuzo ya mfungaji bora dhidi ya magoli ya kujifunga maarufu 'Own goal' au OG.
'Own goal' amepata bao mechi za Iran, Ufaransa, Croatia, Senegal na Russia.
Ingawa kombe la dunia Ufaransa 1998, ilishuhudia mabao sita ya kujifunga shindano nzima, nchini Urusi, baada ya mechi 17, mabao ni matano tayari.
Baada ya mechi zote, magoli ya kujifunga yalikuwa 6 mwaka wa 1998. Tumesalia na zaidi ya mechi 40 na mabao ni 5.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Mabao ya 'Own goal'
Iran (v Morocco), 15 Juni
Own Goal alipata bao lake la kwanza kwenye mechi kati ya Iran na Morocco,tarehe 15 Juni.
Kiungo wa Morocco Aziz Bouhaddouz alijifunga baada ya kuingia na kuipa Iran ushindi mechi ya kwanza kundi B.
Ufaransa (v Australia), 16 Juni
Own goal alipaa bao lake la pili kipute cha kundi C.
Beki wa Australia Aziz Behich naye alijifunga wakaicheza dhidi ya Ufaransa siku iliyofuata tarehe 16 Juni
Ilikuwa mechi ya ufunguzi kundi C
Goli hilo lilikuwa na umuhimu kwani liliipa Ufaransa ushindi na alama 3.
Croatia (v Nigeria), 16 Juni
Goli la tatu la mchezaji Own Goal Urusi 2018.
Kiungo wa Nigeria Oghenekaro Etebo alikuwa wa tatu kujifunga wakichuana na Croatia.
Alielekeza kona ya Luka Modric langoni na kuwa goli la kwanza la Croatia.
Senegal (v Poland), 19 Juni
Senegal ilipata uongozi dhidi ya Poland kufuatia goli la wenyewe lililofungwa na Thiago Cionek.
Kiungo mkabaji wa Senegal Idrissa Gueye aliachilia kombora lililoelekezwa langoni na beki Cionek mechi ya Kundi H.
Russia (v Misri), 19 Juni
Own Goal alikuwa wa kwanza kufunga safari hii kwneye mechi hiyo ya kundi A. Aliisaidia Russia kukaribia kufuzu kwa hatua ya muondoano.
Kiungo wa Misri Ahmed Fathi, alijifunga. Russia ilishinda mechi hiyo 3-1.

Wafungaji mabao bora kufikia sasa
- CRISTIANO RONALDO - Ureno 4
- ROMELU LUKAKU - Ubelgiji 4
- DENIS CHERYSHEV - Urusi 3
- DEGO COSTA - Uhispania 3
Aliyejaribu zaidi kufunga
- LIONEL MESSI - Argentina, mara 12

Ingawa Cristiano Ronaldo amefunga mabao manne, anahitaji bao moja zaidi kumfikia Own Goal.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Tusubiri hadi tarehe 15 Julai kuona iwapo Own Goal atatwaa kiatu cha mfungaji bora wa magoli.












