Sanamu ya Cristiano Ronaldo yabadilishwa Ureno

Ronaldo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ronaldo akipigwa picha na sanamu hiyo ya awali mwaka jana

Sanamu ya awali ya mchezaji nyota wa Ureno na Cristiano Ronaldo ilipataa umaarufu sana duniani, lakini kwa sifa ambazo walioiandaa hawakutarajia.

Ilizua mjadala kutokana na hali kwamba wengi wa mashabiki wa nyota huyo waliamini haikuwa inafanana na Ronaldo.

Wengi hata walidhani ilimfanya aonekana mwenye tabasamu la ajabu, au hata kama kibonzo.

Sanamu hiyo ilikuwa imewekwa kwenye kisiwa cha Madeira, alikozaliwa CR7.

Sanamu ya kwanza (kushoto) na sanamu mpya

Chanzo cha picha, HOMEM DE GOUVEIA

Maelezo ya picha, Sanamu ya kwanza (kushoto) na sanamu mpya

Iliwekwa kwenye uwanja wa ndege wa kisiwa hicho ambao pia ulipewa jina lake baada ya Ureno kushinda Euro 2016.

Sasa, sanamu nyingine imewekwa na hiyo ya zamani kuondolewa.

Hii ya sasa inaonekana kidogo kukaribia kufanana na Ronaldo.

Lakini bado Cristiano hajasema anapendezwa na gani Zaidi.

Aliwika akicheza dhidi ya Uhispania Kombe la Dunia mwishoni mwa wiki ambapo aliwasaidia Ureno kutoka sare ya 3-3 kwa kufunga mabao yote matatu ya taifa lake.