Kipa wa Tunisia 'asingizia jereha' kufungua mwezi wa Ramadhan

Chanzo cha picha, Télévision Tunisienne 1
Kikosi cha kombe la dunia cha Tunisia kimepata njia ya kukabiliana na uchovu huku wakiendelea kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Katika mechi za kirafiki dhidi ya Ureno , aliyekuwa kipa wa Uturuki, Mouez Hassen alionekana kusingizia jeraha wakati funga hiyo ilipokamilika saa za jioni.
Alipokuwa akilala uwanjani ili kupata matibabu , wachezaji wenzake walikimbia hadi nje ya uwanja ili kunywa maji na tende.
Na hatua hiyo ilileta matokeo. Wakiwa nyuma 2-1 dhidi ya mabingwa wa Ulaya 2-1 Ureno, Tunisia walisawazisha dakika sita baada ya jeraha la Hassen na hivyobasi kumaliza mechi hiyo ikiwa 2-2.
Siku chache baadaye dhidi ya Uturuki, Hassen alisitisha mchezo kwa kulalia mgongo wake.
Kwa mara nyengine wachezaji wenzake walikula tende na kunywa maji waliyopewa na wahudumu wa kitendo cha ukufunzi . Mechi hiyo ilikwisha 2-2.

Chanzo cha picha, Télévision Tunisienne 1

Chanzo cha picha, Télévision Tunisienne 1
Kanda ya video ya kisa hicho ilisambazwa na akaunti ya mashabiki wa timu hiyo huku habari hiyo ikiwafurahisha wengi nchini humo
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Wachanganuzi nchini Tunisia kwa haraka walichunguza wakati kipa huyo aliposingizia kuumia katika mechi zote mbili katika dakika ya 58 na 47 mtawalia.
Muda huo uliingiana na muda wa Iftar ambapo Waislamu hufungua mwezi wa Ramadhan kwa kula tende na maji. Shirikisho la soka nchini Tunisia bado halijazungumzia kuhusu mapumziko hayo ya jeraha.
Lakini kipa Hassan alituma ujumbe wa Twitter: ''Niliumizwa, [akiweka emoji za kucheka]' akimjibu mchezaji mwenza Chaker Alhadhurt aliyejibu: ''Ni sawa sasa tunajua ulikuwa aukidanganya''
Macho yote sasa yatakuwa yakimlenga kipa wa Tunisia wakati timu hiyo itakapocheza mechi nyengine ya kirafiki dhidi ya Uhispania tarehe 9 Juni.
Mechi ya kwanza ya kombe la dunia dhidi ya timu hiyo ya Afrika kaskazini itafanyika Uingereza Juni 18 wakati ambapo Ramadhana itakuwa imekamilika.

Chanzo cha picha, AFP

Ramadhan ni nini?
Wakati wa Ramadhan, Waislamu hutakiwa kutokula chakula, maji na kutoshiriki katika tendo la ngono kutoka alfajiri hadi jioni.
Lengo lake ni kufanya ibada na kujizuia .Nia ya kutaka kufunga lazima ifanywe usiku kabla ya mtu kulala ama wakati wa chakula cha daku.
Inaruhusiwa kutofunga wakati wa Ramadhan miongoni mwa Waislamu iwapo mtu ana tatizo la kiakili, anahisi kiu kikali, anasafiri ama iwapo maisha yako yapo hatarani iwapo hutafungua.












