Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Eric Cantona: Guardiola anafaa kuifunza Man United
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Eric Cantona amesema kuwa anapenda ukufunzi wa Jose Mourinho - lakini angependa kikosi cha Man United kucheza kama kile cha Pep Guardiola.
Cantona, ambaye aliichezea United miaka mitano kati ya 1992 na 1997 alimtaja Mourinho kuwa mkufunzi mshindi ambaye ataendelea kushinda.
Lakini raia huyo wa Ufaransa aliambia BBC kwamba Mourinho anapendelea kulinda sana lango ambao sio mchezo wa Manchester United.
Alipoulizwa iwapo angempendelea kocha wa zamani wa Barcelona Guardiola kuchukua hatamu katika klabu hiyo alisema: United ni kama Barcelona.
''Nampenda Mourinho, napenda motisha yake, ni mwerevu sana, anachukua presha yote ya mechi .Lakini pia nampenda zaidi Guardiola''.
''Wote ni wakufunzi wazuri, lakini napendelea soka ya kushambulia wakati inashirikisha mchezo wa nipe nikupe. Ndio nilivyojaribu kucheza wakati wangu''.