Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Aubameyang kuendelea kukipiga na Dortmund
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang hatouzwa katika majira haya ya kiangazi na atasalia katika timu yake.
Mkurugenzi wa Dortmund Michael Zorc, amethitibisha kuwa mchezaji huyo anayewinda na vilabu vya Paris St-Germain , AC Milan na Chelsea haendi kokote.
"Tumeshaamua kwamba Auba atabaki hapa kuendelea kuitumikia timu hii." Alieleza Mkurugenzi huyo.
Aubameyang msimu uliopita aliifungia timu yake jumla ya mabao 31 na kuisaidia kutwaaa taji la kombe la Ujeruman, na kumaliza katika nafasi ya tatu katika ligi ya Bundasliga.