Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vijana msibweteke - Conte
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada ya kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1 na kupiga hatua kubwa kuelekea katika ubingwa wa ligi Kuu.
Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi 11 kabla ya msimu kumalizika.
Akizungumza na wanahabari, Conte amesema wanapaswa kufikiri kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga kuanzia sasa mpaka mwishoni.
Kocha huyo amedai kuwa mpaka sasa walipofika ni pazuri lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na kuhakikisha wanaendeleza makali yao