Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Arsenal kuwavaa wababe wao Bayern
Michuano ya klabu bingwa Ulaya inaendelea tena kesho jumanne kwa michezo miwili kwa mechi za marudiano, Arsenal watakuwa wenyeji wa Bayern Munich , Napoli wanawakaribisha Real Madrid.
KaTika mechi za awali Arsenal wakicheza ugenini dhidi ya Bayern Munich waliambulia kipigo cha mabao 5-1 huku Napoli wao wakicharazwa na Real Madrid ba 3-1.
Arsenal na Napoli zina kazi ya ziada ili kuweza kuendelea na mashindano hayo kwa kuwa wanahitaji ushindi wa magoli mengi katika michezo yao kwa kuwa Bayern na Madrid zina mtaji wa magoli mengi kupitia ushindi walioupata nyumbani kabla ya michezo hii