Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tuzo za Oscar nani kuibuka mshindi?
Zulia jekundu limetandikwa katika ukumbi wa Dolby uliopo jijini Los Angeles kwa ajili ya sherehe za mwaka huu za Oscars.
Maandalizi ya mwaka huu yamekuwa magumu kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo maandamano, na hali mbaya ya hewa mbaya ambayo haikutarajiwa iliyopiga eneo la California, hata hivyo hakuna mvua inayotarajiwa pindi wasanii nyota watakapoanza kuwasili.
Tuzo kuu inatabiriwa kwenda kwa Picha bora ya mwaka , filamu ya muziki ya La La Land,wakati huo huo, mwigizaji nyota Denzel Washington ndiye anayeongoza katika kinyang'anyiro cha mwigizaji bora.
Denzel Washington , ni miongoni mwa nyota wa kiafrika wanagombe kushinda tuzo yenye umbo la sanamu ya dhahabu baada ya kutowakilishwa kwa miaka miwili, jambo ambalo liliibua kampeni iliyopewa jina la Oscar ni ya watu weupe.