Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wayne Rooney kuihama Manchester United ?
Kumekuwa na taarifa kuhusu uwezekano wa Wayne Rooney kuihama Manchester United na kuelekea nchini China mwezi huu.
Lakini Kocha wa klabu ya Tianjin Quanjian ya nchini China, Fabio Canavaro amesema mazungumzo hayakuendelea.
Imefahamika kuwa kuna uwezekano wa kufanikisha mpango huo juma lijalo ni finyu na matarajio ni kuwa Rooney ataendelea kubaki Manchester united kwa kipindi chote cha msimu
Hata hivyo, upo uwezekano wa kuondoka kwa Rooney akiiacha Old Trafford baada ya kuichezea manchester united kwa miaka 13.
Matamanio ya Wyne Rooney inaeleweka ni kubaki na Manchester United mpaka mkataba wake utakapokwisha mwaka 2019, kutopata nafasi katika kikosi cha kwanza kimekuwa kikisabisha rooney kutaka kuiacha Manchester United.