Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Drogba akataa kuichezea timu yake
Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Didier Drogba alikataa kuichezea Montreal Impact baada ya kuambiwa hataanzishwa dhidi ya Toronto ,kulingana na kocha Mauro Biello.
Drogba mwenye umri wa miaka 38 hakuwepo katika uwanja wa michezo wa Saputo ambapo Impact ilipata sare ya 2-2 na hivyobasi kuweza kufuzu kwa michuano ya muondoano ya ligi ya Marekani.
Montreal hapo awali ilikuwa imesema kuwa Drogba alikuwa anauguza jeraha la mgongo na hivyobasi asingeweza kucheza.
Lakini Biello alisema: Hakukubali kwamba angechezeshwa kama mchezaji wa ziada na mwishowe hakutaka kushirikishwa katika kikosi cha watu 18.
Kocha huyo aliongezea: Alikuwa na tatizo katika mgongo wake lakini alikuwa anaweza kucheza.
Drogba ambaye aliondoka Chelsea mwezi Julai 2015 amekuwa akitumiwa kama mchezaji wa ziada katika mechi mbili kati ya nne.
Amefunga mabao 10 katika mechi 21 msimu huu.