Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Yaya Toure: Uamuzi wa Fifa utawaumiza wachezaji
Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure amesema wachezaji na mashabiki wanaweza kuumia kufuatia hatua ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuvunja kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika soka.
Toure mwenye umri wa miaka 33, alikuwa mmoja wa wajumbe katika kikosi kazi hicho kilichoundwa mwaka 2013 kusaidia kutokomeza ubaguzi.
Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura amesema kikosi kazi hicho kilikuwa na kazi maalumu ambayo tayari wameimaliza.
Hata hivyo, hatua hiyo imekosolewa vikali na wadau mbalimbali, akiwemo Toure ambaye alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki wa CSKA Moscow Octoba mwaka 2013.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast amesema hatua hiyo ya FIFA itaweza kuwaumiza mashabiki na wachezaji kama mipango sahihi isipowekwa.