Rais wa Tanzania Samia Suluhu akutana na kiongozi wa Chadema aliye uhamishoni Tundu Lissu

Taarifa hiyo imesema wawili hao walizungumza kuhusu ‘masuala mbali mbali yenye maslahi na ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’

Moja kwa moja

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo ya moja kwa moja ya kurasa wa BBC Swahili, Shukrani!

  2. Rais wa Tanzania Samia Suluhu akutana na Tundu Lissu Brussels

    TV

    Chanzo cha picha, IKULU TANZANIA

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na makamu mwenyekiti wa chama cha Chadema aliye uhamishoni Tundu Lissu.

    Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya rais inasema rais Samia alifanya mazungumzo mafupi na Lissu baada ya kukubali maombi ya kiongozi huyo wakati rais akiwa ziarani jijini Brussels.

    Taarifa hiyo imesema wawili hao walizungumza kuhusu ‘masuala mbali mbali yenye maslahi na ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’

    Katika ujumbe wake kupitia Twitter Zitto Kabwe wa chama cha ACT Wazalendo amesema hatimaye 'hekima imetawala na mlango wa mazungumzo kufunguka'.

    Ameongeza kwamba wanaamini kama chama kuwa mazungumzo ndio njia bora ya kushughulikia tofauti za kisiasa nchini Tanzania .

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Alichosema awali kuhusu kukutana na rais

    Mnamo mwezi Juni mwaka jana Lissu alisema kwamba alikuwa tayari kurudi Tanzania ili kufanya kazi na Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kwenda mafichoni nchini Ubelgiji baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2020.

    Bwana Lissu ambaye alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake wakati huo kuhusu demokrasia Afrika Mashariki, alisema kwamba tayari alikuwa amempigia simu rais Samia na kuomba kufanya mkutano naye.

    Akizungumza wakati huo mjini Nairobi, Lissu ambaye alipoteza uchaguzi wa mwaka wa 2020 kwa Hayati John Pombe Magufuli alisema kwamba lengo lake la kupata mkutano wa ana kwa ana na Rais Samia ni kuzungumzia kuhusu kupanua hali ya kidemokrasia ambayo alisema inatia wasiwasi.

    Alisema kwamba kwa rais huyo mpya kufanikiwa, mabadiliko ya kikatiba , kutoa uhuru kwa sauti za wapinzani ni muhimu .

  3. Uganda yasitisha upimaji wa lazima wa Covid katika uwanja wa ndege

    Uganda imesitisha upimaji wa lazima wa Covid-19 kwa abiria wote wanaoingia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe, kuanzia Jumatano.

    Tangu Oktoba mwaka jana, abiria wote walihitajika kufanya vipimo walipowasili, ikiwa waliwasilisha vipimo halali vya PRC hasi au la.

    Taarifa kutoka kwa wizara ya afya inasema kuwa kusimamishwa kwa upimaji kumetokana na kupungua kwa kesi chanya za Coronavirus zilizotambuliwa kwenye uwanja wa ndege, na kupungua kwa tishio la aina mbali mbali za kirusi hicho .

    Lakini abiria wanaoondoka au wanaoingia Uganda bado watahitajika kuwa na kipimo halali (kilichochukuliwa ndani ya saa 72 za kusafiri) kuwa hasi PRC kabla ya kupanda ndege zao.

    Uganda kwa sasa inaibuka kutoka kwa wimbi lake la tatu la janga hilo, ambalo lilitawaliwa na virusi aina ya Omicron. Wastani wa kesi 50 chanya zimerekodiwa kila siku katika wiki za hivi karibuni.

    Zaidi ya dozi milioni 15 za chanjo zimetolewa hadi sasa.

  4. Pundamilia 'albino' aonekana Serengeti

    m

    Chanzo cha picha, Tanapa

    Pundamilia ' Ndasiata' mwenye ualbino ameonekana Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mapema Februari mwaka huu.

    Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wanyama wenye rangi za kuangaza ambapo ualbino ndio sababu ya kawaida ya muonekano huo.

    TANAPA

    Chanzo cha picha, TANAPA

    Wakati, pumbamilia maarufu Tira ambaye pia alionekana Kenya na Tanzania alikuwa na rangi nyeusi iliyozidi na sasa anaendelea vizuri katika maeneo ya Serengeti, Tanzania ambako inaaminika kuwa ndio nchi yake ya asili.

    TANAPA

    Chanzo cha picha, TANAPA

  5. Mwanamke wa kwanza aripotiwa kuponywa VVU kwa kupandikizwa Seli shina

    Seli shina

    Mgonjwa mmoja wa saratani ya damu amekuwa mwanamke wa kwanza na mtu wa tatu kufikia sasa kuponywa VVU baada ya kupandikizwa seli shina kutoka kwa wafadhili ambaye kwa asili alikuwa sugu kwa virusi vinavyosababisha UKIMWI, watafiti waliripoti Jumanne.

    Kesi ya mwanamke wa makamo wa asili mchanganyiko, iliyowasilishwa katika Mkutano kuhusu virusi na maambukizi huko Denver, pia ni ya kwanza inayohusisha damu ya kitovu, mbinu mpya zaidi ambayo inaweza kufanya matibabu kupatikana kwa watu wengi zaidi.

    Tangu apokee damu kutibu saratani ya damu inayosambaa kwa kasi inayoanzia kwenye chembechembe za damu kwenye uboho - mwanamke huyo amekuwa katika hali ya kupona na kutokuwa na virusi kwa muda wa miezi 14, bila kuhitaji matibabu ya VVU yanayojulikana kama tiba ya kurefusha maisha.

    Kesi mbili za awali zilitokea kwa wanaume - mmoja mwenye asili ya mzungu na mwingine Latini - ambao walikuwa wamepokea seli shina za watu wazima, ambazo hutumiwa mara kwa mara katika upandikizaji wa uboho.

    "Hii sasa ni ripoti ya tatu ya tiba katika mazingira haya, na ya kwanza kwa mwanamke anayeishi na VVU," Sharon Lewin, Rais Mteule wa Jumuiya ya Kimataifa ya UKIMWI, alisema katika taarifa yake.

  6. Kiongozi wa mapinduzi ya Burkina Faso aapishwa kuwa rais

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso ambaye alichukua udhibiti katika mapinduzi wiki tatu zilizopita ameapishwa kuwa rais wa mpito.

    Akiwa amevalia sare za kijeshi na bereti nyekundu, Paul-Henri Damiba aliapa kuheshimu katiba katika hafla ndogo katika mji mkuu, Ouagadougou.

    Lt-Kanali Damiba aliongoza maafisa wa jeshi kumwondoa madarakani mkuu wa nchi aliyechaguliwa Roch Kaboré mwezi uliopita, akiwa na hasira kutokana na jinsi alivyoshughulikia uasi wa kijihadi.

    Jeshi linasema litarejesha utulivu wa kikatiba lakini halijatoa ratiba ya kurejea utawala wa kiraia.

    Afrika Magharibi imekumbwa na msururu wa mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya hivi karibuni.

  7. Mashambulizi ya Al-Shabab nchini Somalia yawaua takribani watu watano

    Jengo lililoharibiwa na masambulizi

    Chanzo cha picha, AFP

    Takriban watu watano wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya 16 kujeruhiwa wakati wa mashambulizi yaliyoratibiwa na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabab nje kidogo ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

    Polisi wanasema mashambulizi hayo ya asubuhi yaliwalenga polisi na vituo vya ukaguzi.

    Kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeda lilisema limetekeleza mashambulizi likisema wapiganaji wao walivamia kambi za serikali na kukamata magari ya kijeshi na silaha.

    Madai hayo hayajathibitishwa mara moja.

  8. DRC yakasirishwa na kauli ya Naibu Rais wa Kenya kuwaita 'waimbaji'

    William Ruto amesema Wacongo walikuwa waimbaji wavivu, ambao hawakumiliki ng'ombe

    Chanzo cha picha, AFP

    Kauli ya Naibu rais wa Kenya wakati wa mkutano wa kisiasa yamezua hasira mtandaoni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Siku ya Jumatatu, William Ruto aliwaambia wakazi wa Nyeri, katikati mwa Kenya, kwamba kulikuwa na soko kubwa la mazao yao ya maziwa nchini DR Congo - na alionekana akisema kuwa hakuna ng'ombe nchini humo.

    "Tuna soko nchini DR Congo... watu hawa ambao ni waimbaji... Watu hawa wana idadi ya watu takriban milioni 90 lakini hawana ng'ombe," alisema kwa Kiswahili - kipande chake ambacho kimesambazwa sana.

    Kauli hizo hazijapokelewa vyema nchini DR Congo, huku hata baadhi ya wanasiasa na waandishi wa habari wakizitaja kuwa ni za dharau kwani pia anaonekana kuwadharau Wacongo kuwa ni wavivu wanaojua kuimba tu.

    Seneta Francine Muyumba aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuyataja matamshi hayo kuwa ni "matusi" na "hayakubaliki" na kumtaka Bw Ruto kufuta kauli hiyo.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    "Kenya kama nchi inapaswa kusimama dhidi ya kauli hii ili kulinda urafiki tunaofurahia kati ya nchi zetu. "Tunaposubiri serikali yetu kuchukua hatua, tuko tayari kuchukua hatua za bunge," alisema.

    Suala hilo limekuwa likivuma kwenye mtandao wa Twitter nchini DR Congo kwa siku mbili zilizopita, huku baadhi ya ujumbe ukuionesha picha za mashamba ya ng'ombe nchini humo:

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Baadhi ya Wakenya wamemtetea Bw Ruto, wakisema alikuwa akiwahimiza tu wafugaji kutafuta fursa katika eneo zima.

  9. Algeria kutoa malipo ya kila mwezi kwa watu wasio na ajira

    Sasa kuna zaidi ya watu 600,000 wasio na ajira nchini Algeria.

    Chanzo cha picha, AFP

    Rais wa Algeria anasema serikali itaanzisha mafao ya ukosefu wa ajira kwa vijana wakati nchi hiyo ikipambana na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira.

    Rais Abdelmadjid Tebboune aliwaambia waandishi wa habari kwamba malipo kwa watafuta kazi wenye umri wa miaka 19 hadi 40 yataanza mwezi Machi.

    Wale ambao wamehitimu wataweza kukusanya malipo ya takriban dola 100 za Marekani 100 kwa mwezi, pamoja na baadhi ya mafao ya matibabu, hadi wapate kazi.

    Akitoa tangazo hilo, Bw Tebboune alisema kuwa Algeria ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya kuanzisha mpango huo.

    Aliongeza kuwa sasa kuna zaidi ya watu 600,000 wasio na ajira nchini Algeria.

  10. Mbappe: ‘Sijaamua hatma yangu’

    Kylian Mbappe amefunga mabao matano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kylian Mbappe amefunga mabao matano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu

    Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe amesema bado hajafanya uamuzi kuhusu hatma yake baada ya kufunga goli la lala salama dhidi ya Real Madrid katika hatua ya kwanza ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya katika dimba la Parc des Princes.

    Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliwatoka walinzi wawili wa Madrid katika dakika ya 94 kabla ya kupachika bao muhimu na kuipa ushindi wa bao 1-0 timu yake.

    Mkataba wa Mbappe unamalizika mwishoni mwa msimu akihusishwa na mipango ya kuhamia Real Madrid.

    "Nachezea moja ya timu bora duniani," aliiambia Movistar TV.

    "Nitajitoa kuisaidia timu yangu katika kipindi chote cha msimu kilichobakia. Bado sijaamua hatma yangu."

    Mchezo wa usiku Jumanne ulionekana kama mchezo muhimu kwa hatma ya Mbappe, haijalishi kama hilo lilikuwa sahihi ama la, nyota huyo alionyesha kiwango kizuri.

    Mwanidhi wa soka Ufaransa Julien Laurens anaamini Mbappe ataaamua hatma yake mwishoni mwa msimu.

    Ameiambia BBC kwamba "tunajua familia ya Mbappe inazungumza na klabu na ndoto yake ni kuichezea Real Madrid.

    Soma zaidi:

  11. Mji mkuu wa Somalia washuhudia milipuko na milio ya risasi

    Hakuna ripoti zozote za majeruhi au vifo zilizotolewa

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Hakuna ripoti zozote za majeruhi au vifo zilizotolewa

    Wanamgambo wa al-Shabab wameshambulia vituo vya polisi na vituo vya ukaguzi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, mapema Jumatano, mamlaka inasema.

    Milio ya risasi na milipuko mingi ilisikika mwendo wa saa 01:00 kwa saa za huko.

    Hata hivyo, Waziri wa Usalama wa Ndani Abdullahi Nor alisema kwenye Twitter kwamba vikosi vya usalama vimewashinda wanamgambo wanaohusishwa na al-Qaeda.

    Hata hivyo, bado hakuna ripoti zozote za majeruhi au vifo zilizotolewa.

    Wiki iliyopita, takriban watu sita walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kulenga basi dogo lililojaa wajumbe walioshiriki katika uchaguzi wa bunge unaoendelea nchini humo.

  12. Msimamo wa Tanzania kuhusu ushirikiano wa kibiashara wa EU

    Bendera za Umoja wa Ulaya na Tanzania

    Chanzo cha picha, European Union facebook

    Maelezo ya picha, Bendera za Umoja wa Ulaya na Tanzania

    Tanzania imetupilia mbali madai ya uwezekano wa makubaliano ya masharti ya Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

    Katika taarifa yake, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara nchini humo inashikilia kuwa itaridhia tu mkataba wa kibiashara baada ya masuala ambayo hayajakamilika kushughulikiwa kwa manufaa ya nchi na ukanda wa Afrika Mashariki.

    Tanzania hapo awali ilizungumzia wasiwasi wa kwamba Umoja wa Ulaya unaweza kujaza nchini humo bidhaa za bei ya chini katika makubaliano yaliyopendekezwa, na kuwa na athari mbaya kwa viwanda vyake vya ndani.

    Kenya na Rwanda ndizo nchi mbili pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zimetia saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) unaolenga kutokuwepo kwa kiwango maalum cha bidhaa na pia upatikanaji wa bidhaa bila kutozwa ushuru kwa bidhaa maalum kwa Umoja wa Ulaya.

    Hata hivyo, makubaliano ya kibiashara yanaweza tu kuwa na ufanisi baada ya kuidhinishwa na nchi zote wanachama wa umoja huo, na kulazimisha Nairobi kuwa na mpango wa muda na EU kuruhusu bidhaa zake kupatikana bila ushuru kwenye soko kubwa la EU.

    Baadhi ya nchi wanachama wa EAC wanataka kuwepo kwa kipengele cha ushuru maalum wa mauzo ya nje ili kulinda baadhi za sekta wanazoziona kuwa nyeti na kuzuia usafirishaji wa malighafi zao nje ya nchi.

    Pia unaweza kusoma:

  13. Zanzibar yaanza kutumia teknolojia mpya ya kupima Covid-19 kwa wasafari wake,

    Watu wakipimwa na kifaa kipya Zanzibar
    Maelezo ya picha, Watu wakipimwa na kifaa kipya Zanzibar

    Serikali ya Zanzibar hii leo, imezindua rasmi matumizi ya teknolojia mpya inayoweza kutambua uwezekano wa maambukizi ya Covid-19 kupitia vipimo vya smaku umeme yaani electromagnetic.

    Teknolojia hii, tofauti na zile nyengine, haihitaji msafiri kuchukuliwa sampuli ya vipimo kupitia mdomoni au puani, na vile vile msafiri bila kuguswa, anaweza kupimwa akiwa umbali wa mita moja na majibu yake ni ya hapo kwa hapo.

    Maelezo ya video, Zanzibar yaanza kutumia teknolojia mpya ya kupima Covid-19 kwa wasafari wake

    Hii ni mara ya kwanza kwa teknolojia hii kutumika barani Afrika, na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ndio unaandika historia ya kuwa uwanja wa kwanza wa kimataifa nchini Tanzania kuwa na teknolojia hii, ambayo imekuja kwa msaada kutoka serikali ya Abu Dhabi.

    Mkurugenzi wa mradi huu DadKarim Mulla anasema, utafiti uliopelekea kupatikana kwa teknolojia hii umefanyika Abu Dhabi na umegharimu takriban dola za kimarekani bilioni moja.

    Inaaminika kwamba, matumizi ya teknolojia hii, yanaweza kuleta afueni kubwa kwa wasafiri ambao kwa sasa wataweza kuendelea na safari zao kwa haraka zaidi bila usumbufu na kupoteza muda.

    Zanzibar na Abu Dhabi wamekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kihistoria ambapo ni jambo la kawaida kila mwaka kwa kisiwa hicho kupokea maelfu ya wageni kutoka nchi hizo mbili.

    Kundi la kwanza la wageni lililotumia teknolojia hiyo, limetua kwa ndege ya Fly Dubai mapema asubuhi ya leo.

    “Ni teknolojia nzuri. Inatoa majibu haraka sana, kwa kweli hata sikujua kama wanapima, nilihisi wananipiga picha tu. Nimefurahi, “ anasema mmoja wa wasafiri kutoka Saudi Arabia.

    Wakati huo huo, waziri wa Afya wa Zanzibar, amesema mpaka sasa Zanzibar haina mgonjwa mwenye maambukizi ya Covid-19 tangu mwezi Januari, hivyo ni muhimu kwa serikali kukumbatia teknolojia ambayo itawaweka salama wazanzibar na wageni.

    Zanzibar, kama maeneo mengine ya Tanzania, ilikumbwa na wingi la maambukizi ya Covid-19 tangu kuanza kuibuka kwa kirusi hicho.

    Mwaka jana, wakati kama huu, Zanzibar ilimpoteza makamu wake wa rais wa kwanza ambae alikufa kutokana na maambukizi ya Covid-19.

    Soma zaidi:

  14. Waasi wa Tigray watuhumiwa kwa ubakaji na mauaji ya genge

    Vituo vya umma vimeporwa na kuharibiwa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Vituo vya umma vimeporwa na kuharibiwa

    Ripoti mpya imetoa maelezo zaidi ya kile inachokiita ukiukaji mkubwa wa sheria ya haki za kibinadamu unaofanywa na wapiganaji waasi kutoka eneo la Tigray nchini Ethiopia.

    Ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International inawashutumu waasi wa Tigray kwa ubakaji wa genge na mauaji ya kimakusudi ya raia katika eneo jirani la Amhara ambapo walidhibiti eneo hilo kwa muda hadi walipofurushwa na vikosi vya serikali miezi miwili iliyopita.

    Amnesty inasema vikosi vya waasi viliua raia wasiokuwa na silaha katika mji wa Kobo na kuwanyanyasa kingono takriban wanawake na wasichana 30 katika kijiji cha Chena.

    Mali ya umma ikiwa ni pamoja na shule na vituo vya matibabu viliporwa au kuharibiwa.

    Hata hivyo, kundi la The Tigray People Liberation Front halijajibu madai ya hivi punde lakini limekanusha shutuma kama hizo hapo awali.

    Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia pia wameshutumiwa kwa mauaji na ubakaji.

    Soma:

  15. Tanzania kuanza kutengeneza chanjo ya corona

    Tanzania inalenga kuuza chanjo kwa majirani zake

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Tanzania inalenga kuuza chanjo kwa majirani zake

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali yake inataka kuanzisha kiwanda cha utengenezaji wa chanjo kama njia moja ya kutimiza mipango ya serikali ya kukabiliana na ugonjwa wa corona na magonjwa mengineo.

    Akizungumza na Rais wa baraza la Ulaya, Bwana Charles Michel huko Brussels hapo jana, alisema kuwa Tanzania inataka kuwa muuzaji wa chanjo za kuokoa maisha kwa jamii ya Afrika Mashiriki (EAC) na nchi washirika wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

    Rais ambaye yuko kwenye ziara rasmi huko Ubelgiji, alisema kuna uwezekano Tanzania ikatumia hadi bilioni 216 za Tanzania hadi kufikia mwaka 2030 ili kuagiza chanjo kutoka nje ya nchi akisisitizia umuhimu wa kuwa na kiwanda cha uzalishaji ndani ya nchi.

    ‘’Tanzania ingependa kuwasilisha pendekezo hili na natazamia kwa hamu kuungwa mkono kwa wazo hili na kufanikiwa. Nina amini, mpango huu ukitekelezwa, utafungua fursa zingine na kuimarisha uhusiano wetu zaidi,’’ alisema.

    Tangu kuanzishwa kwa ushirikiano na EU mwaka 1975, Tanzania imekuwa ikipata misaada ya maendeleo yenye thamani ya trilioni 5.98 pesa za Tanzania huku ikiwa imesalia kuwa moja ya mshirika muhimu kwa nchi hiyo

    Soma:

  16. New Zeeland: Wanasayansi wagundua kitoto cha papa wa ajabu

    Papa adimu wa maji ya kina kirefu

    Chanzo cha picha, BRIT FINUCCI

    Maelezo ya picha, Papa adimu wa maji ya kina kirefu aliyeanguliwa na timu ya wanasayansi kwenye pwani ya Kisiwa cha Kusini cha New Zealand.

    Wanasayansi nchini New Zealand wamegundua kitoto cha papa adimu cha ajabu (Ghost Shark), aina ya samaki isiyo fahamika sana, ambayo inaishi kwenye maficho ya kina kirefu cha bahari.

    Papa huyo wa ajabu- pia hujulikana kama chimaera - ni nadra sana kuonekana, huku vitoto ikiwa ni nadra zaidi kuonekana.

    Kiumbe hiki kipya kimepatikana kwenye kina cha bahari chenye urefu wa kilometa 1.2 chini ya bahari karibu na South Island.

    ‘Viumbe vinavyoishi kwenye kina kirefu zaidi cha bahari ni kazi kupatikana, kwa hivyo tunawaona kwa nadra sana’, alisema Dr. Brit Fanucci, mmoja wa timu ya wanasayansi waliomgundua papa huyo.

    Kwa mujibu wa wanasayansi, ghost shark si papa halisi, ila ni viumbe vinavyokaribiana kwa sifa na muonekano na papa halisi. Mifupa yao inaundwa na aina fulani ya tishu zinazompa muonekano wa ajabu au kutisha.

    Viumbe wengi wa aina hii, wanaishi kwenye kina kirefu cha maji ya bahari, ingawa baadhi wanapendelea kuishi kwenye kina kifupi cha maji ya ufukwe.

    Pia unaweza kusoma:

  17. Mwalimu aliyebaka wanafunzi 13 ahukumiwa kifungo cha maisha jela

    Wirawan alikuwa mmiliki na mwalimu wa shule ya bweni ya Indonesia

    Chanzo cha picha, WEST JAVA PROSECUTOR OFFICE

    Maelezo ya picha, Wirawan alikuwa mmiliki na mwalimu wa shule ya bweni ya Indonesia

    Mahakama moja ya Indonesia siku ya Jumanne ilimuhukumu mwalimu wa somo la dini ya Kiislamu kifungo cha maisha jela kwa kuwabaka wanafunzi 13 wa kike.

    Wanane kati yao walio na umri wa kati ya miaka 12 hadi 16 ni wajawazito kulingana na uchunguzi wa polisi.

    Kesi hiyo inaangazia unyanyasaji katika baadhi ya shule za mabweni ambazo nyingi ni vituo vya mafunzo ya kiislamu.

    Jaji aliamuru kwamba mwalimu Herry Wirawan, aliwanyanyasa kingono wanafunzi hao na kwamba baadhi yao walijeruhiwa vibaya.

    Wirawan

    Chanzo cha picha, WEST JAVA PROSECUTOR OFFICE

    Maelezo ya picha, Watetezi wa kesi yake wamekuwa wakifanya kazi ili nakala halisi ya taarifa hii ipatikane mtandaoni.

    Tabia ya Wirawan iligunduliwa mnamo mwezi Mei mwaka uliopita wakati mzazi wa msichana mmoja alipotangaza kwamba mwanawe wa kike ni mjamzito.

    Viongozi wa mashtaka walimtaka mwalimu huyo kuhukumiwa kifo ama hata kuchinjwa kwasababu uhalifu alioutenda ulikuwa mbaya na ulifanyika kati ya mwaka 2016 hadi 2021.

    Serikali ya Jakarta imetangaza kwamba itawalipa karibia dola 6000 kama fidia kila msichana aliyeathirika.

    Pia unaweza kusoma:

  18. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 16/02/2022