Amazon imeweka kamera zinazoweza kupima Covid 19
Kampuni kubwa ya teknolojia ya Amazon imeweka kamera katika ghala zake nchini Uingereza na kote duniani ili kuwapima wafanyikazi wake dalili za virusi vya Corona. Kamera hizo zina uwezo wa kugundua kipimo cha mtu cha joto ikilinganisha na ile ya mazingira yao. Je unadhani kampuni zengine zinafaa kuiga mfano huo ? Sema nasi kwenye ukurasa wa Facebook, BBCNewsSwahili
