Virusi vya corona: Jimbo la New York lahalalisha ndoa za mitandao.

Maelezo ya sauti, Jimbo la New York lahalalisha ndoa za mitandao.

Gavana wa jimbo la NewYork Andrew Cuomo amepitisha sheria inayoruhusu ndoa za mitandaoni. Kuanzia sasa watu wanaweza kufunga ndoa, na kupata cheti cha ndoa kupitia njia ya mtandao, na atakayefungisha harusi atafanya hivyo kupitia video ya moja kwa moja. Gavana Cuomo amesema hakuna kizuizi sasa cha wapenzi kutofunga ndoa. Je unaweza kukubali harusi yako ifanyike kwa njia hii?