Mapinduzi ya Burkina Faso: Kurejea kwa wababe wa kijeshi Afrika Magharibi

Baadhi ya raia wa Burkina Faso wameunga mkono udhibiti wa jeshi

Chanzo cha picha, Reuters

Kufuatia jeshi kufanya mapinduzi nchini Burkina Faso, mchambuzi wa kikanda Paul Melly anafikiria ni kwa nini Afrika Magharibi inashuhudia wimbi jipya la mapinduzi baada ya demokrasia kuonekana kukita mizizi katika eneo hilo.

Chini ya miezi mitano baada ya wanajeshi kuonekana kwenye televisheni ya taifa nchini Guinea kutangaza kuwa wamemuondoa madarakani Rais Alpha Condé, tukio hilo lilirudiwa siku ya Jumatatu nchini Burkina Faso, huku jeshi likitangaza kupinduliwa kwa mkuu wa nchi Roch Kaboré.

Na hilo bila kusahau mapinduzi mara mbili nchini Mali, ambapo maafisa wa jeshi walimwondoa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta mnamo Agosti 2020.

Waliahidi kambi ya kikanda ya Ecowas kuwa wataandaa uchaguzi kufikia mwezi ujao, lakini Mei 2021 walichukua tena udhibiti wakati wa mabadiliko hayo na baadaye kuweka mipango ya kusalia madarakani kwa karibu miaka mitano zaidi.

Hata hivyo, Afrika Magharibi ilikuwa eneo ambalo kikatiba siasa za kiraia za vyama vingi zimekuwa kawaida.

Takriban nchi zote angalau zilikuwa za kidemokrasia rasmi, hata kama baadhi ya marais waliochaguliwa, mara moja wakiwa madarakani, walipindisha kanuni ili kuendeleza kukaa kwao madarakani.

Sasa wanachama watatu wa kikanda , Ecowas wako chini ya uongozi wa wanaume waliovalia sare za jeshi.

Je, enzi iliyosahaulika kwa muda mrefu ya mwanajeshi mwenye nguvu inarejea?

Labda hiyo ni njia rahisi sana ya kutazama vitu.

Guinea siku zote ilikuwa tofauti kidogo - ikiwa na historia ndefu ya utawala duni na ukandamizaji.

Alpha Condé alichaguliwa kuwa mkuu wa nchi wa kwanza wa kidemokrasia mnamo 2010 lakini alizid kubadilisha katiba ili imruhusu kugombea muhula wao mnamo 2020 na kuwaweka jela wapinzani wengi.

Anguko lake la Septemba mwaka jana, mikononi mwa wanajeshi walioahidi serikali ya mpito shirikishi kuelekea demokrasia ya kweli, lilikutana na kukaribishwa karibu na watu wote wa Guinea; hakukuwa na dalili ya majuto hata kutoka kwa chama chake cha kisiasa.

Jinsi uasi ulivyosababisha mapinduzitena

Kinyume chake, nchini Burkina Faso, kama ilivyo nchini Mali, ni mzozo wa usalama unaosababishwa na wanajihadi ambao ni wazi umesababisha madhara makubwa.

Ripoti zisizokoma za mashambulizi ya Kiislamu zinazochochea hasira za wananchi katika mitaa ya mijini na chuki miongoni mwa askari ambao wanahisi wanatumwa nje, wakiwa na silaha nyepesi mno, wanaolipwa ujira mdogo au hata kupatiwa mlo kidogo, kuendeleza mapambano dhidi ya makundi ya wanamgambo.

Mapinduzi ya Ouagadougou wiki hii - kama mapinduzi ya 2020 nchini Mali, na hata utekaji wa kijeshi wa 2012 nchini humo - ni mlipuko wa hasira kutoka kwa askari wa chini na wa kati ambao wanahatarisha maisha yao kwenye mstari wa mbele katika mzozo wa kikatili usio na maelewano. .

Hisia zimekuwa nyingi sana tangu shambulio la wanajihadi la Novemba 14 kwenye ngome ya Inata gendarmerie kaskazini mwa Burkina Faso na kusababisha vifo vya wanajeshi 53 kati ya 120.

Baadhi nchini Burkina Faso wanataka vikosi vya Urusi kuchukua nafasi ya Wafaransa - kama walivyofanya nchini Mali

Chanzo cha picha, Reuters

Mahitaji ya mkakati madhubuti zaidi wa usalama yalikuwa yameongezeka hadi mwaka jana, na Rais Kaboré alibadilisha kwanza serikali yake na kisha uongozi wa jeshi katika juhudi za kurejesha kasi ya kisiasa na kuanza kurejesha utulivu kwa majimbo ya kaskazini na mashariki ya Burkina Faso yaliyopigwa.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita haya yameshuhudia zaidi ya shule 1,000 zikifungwa na watu milioni 1.5 kukimbia makazi yao ili kuepuka ghasia, wengine wakiachwa bila chaguo ila kuomba pesa au chakula katika mitaa ya mji mkuu. Zaidi ya watu 2,000 wamepoteza maisha.

Bila shaka, mgogoro wa Sahel sio mpya. Kwa muongo mmoja vikundi vya wanajihadi na mivutano kati ya jumuiya imetishia usalama wa maisha ya kila siku ya kijiji katika maeneo mengi zaidi ya eneo hilo, huku serikali dhaifu zikijitahidi kudumisha utawala wa kimsingi na huduma za umma.

Kuingilia kati kwa vikosi vya Ufaransa na Afrika Magharibi nchini Mali mnamo 2013 kulikomboa miji kutoka kwa uvamizi wa wanamgambo wa Kiislamu. Lakini haikuweza kusimamisha vurugu za vijijini.

Na katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita hali ya ukosefu wa usalama imeonekana kana kwamba inaongezeka - haswa nchini Burkina Faso, ambapo mtindo wa mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia na kambi za vikosi vya usalama umeenea kwa kasi kuelekea kusini kutoka maeneo ya mpakani na kuathiri jamii karibu zaidi na Ouagadougou.

Barabara kuu ya mashariki kuelekea Fada Ngourma na, zaidi ya hapo, mpaka na Niger, si salama tena. Na migodi hufichwa kwa urahisi katika vumbi la barabara za vijijini za mkoa huo, na kuhatarisha safari za kila siku za kwenda sokoni au shuleni.

Mauaji ya waasi ya Juni mwaka jana katika vijiji vya Solhan na Tadaryat, katika mkoa wa Yagha, yalisababisha vifo vya takriban watu 174.

Kivipi Kaboré alipoteza umaarufu wake?

Bw Kaboré alichaguliwa mnamo Novemba 2015, kufuatia mapinduzi ya nguvu ya watu ambayo yalipuuza utawala wa kimabavu uliopita. Na miaka mitano baadaye alichaguliwa tena kwa muhula wa pili kwa raha, katika uchaguzi wa haki na wa kidemokrasia ya kweli.

Lakini baada ya hapo alipata mdororo mkubwa wa umaarufu huku imani katika uwezo wake wa kukabiliana na ghasia zinazozidi kuwa mbaya za wanajihadi ilipoporomoka.

Baada ya minong'ono ya kutoridhika kijeshi katika wiki za hivi karibuni, askari katika kambi muhimu katika mji mkuu, Ouagadougou, hatimaye waliasi siku ya Jumapili, machafuko ambayo mwishoni mwa siku iliyofuata yalikuwa yamegeuka kuwa mapinduzi kamili.

Hayo yamejiri baada ya wimbi kubwa la mashambulizi ya wanajihadi mwaka uliotangulia na licha ya baadhi ya maendeleo ya baadae ya serikali, majirani wa eneo hilo na Ufaransa katika kampeni dhidi ya wanamgambo hao.

Shambulio la Inata lilikuja wakati serikali ilikuwa bado iko katikati ya kupanga upya mkakati wake na hali ya hofu imeongezeka tu.

Chini ya miezi mitatu baadaye, Bw Kaboré yuko nje ya mamlaka na yuko katika kizuizi cha jeshi.

Takriban watu milioni 1.5 wamelazimika kukimbia makazi yao nchini Burkina Faso kwa sababu ya uasi

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni rahisi kuhisi kana kwamba wanajihadi wanatafuta kwa makusudi kuzusha machafuko katika majeshi ya Sahel.

Lakini katika hali halisi, habari za shambulio moja la mauaji baada ya lingine, linalogharimu maisha ya wanakijiji, wafanyakazi wa kujitolea wa usalama wa ndani au askari , huchochea hali ya hofu na pengine kutojiweza ambayo inaweza kudhoofisha uaminifu wa jeshi.

Sasa kuna uvumi kuhusu iwapo Niger, ambayo imekuwa ikilengwa na makundi sawa na Mali na Burkina Faso, inaweza pia kukabiliwa na hatari ya kunyakuliwa kijeshi.

Rais wa Niger Mohamed Bazoum amezindua mpango mkubwa wa kuwashawishi wanakijiji kurejea katika maeneo ya nyumbani waliyokuwa wameyakimbia kwa sababu ya ghasia, lakini akiungwa mkono sasa na uwepo wa jeshi ulioimarishwa, na kurejeshwa kwa huduma za umma za mitaa na programu za maendeleo.

Hili ni jaribio la kuzuia ghasia za wanajihadi dhidi ya kupunguza idadi ya watu katika maeneo yote na kuharibu mfumo wa kijamii na kiuchumi wa eneo hilo. Je, itafanikiwa?

Baadhi ya wachambuzi wanaona kwamba suala la udhibiti wa Sahel "limeimarishwa" na kwamba maendeleo ndio jibu la kweli.

Lakini katika eneo lote la kanda, wengi wanajibu kuwa haiwezekani kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii bila kuhakikisha usalama kwanza.

Zaidi kuhusu mgogoro wa Burkina Faso na majirani zake:

Map
1px transparent line