China yaishinda Marekani kwa ushirika wa biashara na Muungano Ulaya

Chanzo cha picha, Getty Images
Uchina sasa ndio mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa Muungano wa Ulaya, ikiipiku Marekani katika mwaka 2020.
Uchina imeonesha kuwa na shughuli kubwa za biashara, huku biashara na washirika wakuu wa Muungano wa Ulaya ikipungua kutokana na janga la Covid-19.
Biashara baina ya Uchina na EU ilikuwa ya thamani ya dola bilioni 709b (€586bn, £511bn) mwaka jana, huku Marekani ikifanya biashara ya thamani ya dola bilioni 671 ya mauzo na uajizaji wa bidhaa kutoka Marekani.
Ingawa uchumi wa Uchina uliyumba katika kipindi cha robo ya mwaka jana kutokana nan a janga la corona, uchumi wake uliinuka baadae mwaka huo na kuchochea uhitaji wa bidhaa za Uchina kutoka Muungano wa Ulaya.
China lilikuwa ndilo taifa pekee lemnye uchumi mkubwa duniani kushuhudia ukuaji wa uchumi katika mwaka 2020, na hivyo kupata soko la magari ya Ulaya na bidhaa za anasa.
Wakati huohuo, faida ya mauzo ya nje ya Uchina kwa Ulaya yalipatikana kutokana na mauzo ya bidhaa za matibabu na za kielekroniki zilizohitajika kwa wingi.
"Katika mwaka 2020, China ilikuwa ni mshirika mkuu wa EU. Hii ilitokana na kuongezeka kwa mauzo ya 5.6% na uagizaji wa bidhaa kwa 2.2% ," kwa mujibu wa ofisi ya takwimu ya Muungano wa Ulaya- Eurostat.
Takwimu hizo zilikuwa sawa na data rasmi zilizochapishwa na Uchina mwezi wa Januari, ambazo zilionesha kuwa biashara ya taifa hilo na Muungano wa Ulaya ilikua hadi 5.3% hadi dola bilioni $696.4 katika mwaka 2020.
Upungufu wa kibiashara ya Muungano wa EU na uchina pia ulikua kutoka dola bilioni 199 hadi dola bilioni 219, kulingana na takwimu za Eurostat , ambazo zilitolewa siku ya Jumatatu.
Biashara kati ya Marekani na Uingereza pia ilianguka
Ingawa Marekani na Uingereza zimesalia kuwa masoko makubwa ya bidhaa kutoka Muungano wa Ulaya, biashara na mataifa yote mawili zilishuka kwa kiasi kikubwa, zimeonesha takwimu.
"Biashara na Marekani ilionekanesha rekodi ya kuporomoka katika uagizaji wa bidhaa kwa kiwango cha -13.2% na mauzo kwa kiwango cha -8.2%)," shirika la data lilisema.
Biashara kupitia baharai ya Altantiki imekumbwa na mzozo wa kibiashara ambao umesababisha kupanda kwa viwango vya ushuru kwa bidhaa za chuma na bidhaa kama vile pikipiki za Ufaransa ya Cognac au ya Marekani ya Harley-Davidson
Katika mwaka 2020, Marekani ilikuwa na ukubwa wa biashara wa thamani ya dola bilioni 171, na Muungano wa Ulaya, kiwango hiki kikiwa ni chini ya ukubwa wa biashara baina ya pande mbili katika mwaka 2019 ambapo biashara ya pande mbili ilikuwa na ukubwa wa thamani ya dola bilioni 174.
Haijafahamika wazi kama rais mpya Joe Biden atatathmini upya biashara kati ya Marekani na Ulaya.
Muungano wa Ulaya na China, hatahivyo, wanajaribu kuimarisha uhusiano wao wa kiuchumi, huku kila upande ukitaka kuidhinisha mkataba wa uwekezaji ambao utazipatia kampuni za Muungano wa Ulaya uwezo bora wa kuyafikia masoko ya Kichina.
Wachambuzi wanaaashiria mabadiliko ya uchumi wa dunia katika mwaka 2021 baada ya uzorotaji wa mwaka 2020.
Thamani halisi ya biashara ya dunia inatarajiwa kupatanda kwa 7.6% baada ya kushuka kwa 13.5% katika mwaka 2020 hadi sawa na dola trilioni 16.4 , kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya IHS Markit.












