Wanaume watatu waelezea walivyoasi kutoka kundi la Al-Shabab

Chanzo cha picha, AFP
Kundi la wanamgambo wa al-Shabab linasajili maelfu ya wanajeshi wanaotembea kwa miguu lakini pia linahitaji watu watakaotoa huduma za umma katika maeneo wanayodhibiti.
Na yeyote atakayepatikana akiasi kwa kutoroka adhabu yake ni kifo.
Wakati huohuo, serikali inajitahidi kuhamasisha walioasi, na pia inaendesha kituo cha kurekebisha tabia kuwasaidia kujumuika tena na jamii.
Fuatilia simulizi ya watu watatu walioamua kutoroka kundi la al-Shabab.
Ibrahim anasema ana umri wa miaka 35.
Moulid ana umri wa miaka 28 huku Ahmed akiwa na umri wa miaka 40.
Majina yaliyotumika na picha sio za watu halisi kwasababu ya usalama wao.
Hii ni kwasababu wote watatu wametoroka kundi la wanamgambo wa al-Shabab, ambalo limekuwepo kwa zaidi ya mwongo mmoja na pia linadhibiti sehemu kubwa ya Somali, na kama haitoshi, limeweka sheria na adhabu kali kwa wanaoasi.
Kundi hilo limeunda utawala wake wenye mawaziri, kikosi cha polisi na mfumo wake wa utekelezaji sheria.
Pia kundi hilo linaendesha shule na vituo vya afya, linaendeleza miradi ya unyunyiazi mashamba maji, linatengeneza barabara na madaraja na linahitaji watu kutekeleza kazi hizo.

Adhabu ya kuasi ni kifo. Kwa mujibu wa aliyeandaa taarifa hii, kundi la al-Shabab limesema kuwa adhabu hiyo ni kwa yeyote anayeondoka kundi hilo bila ruhusa na sio tu kwa wapiganaji.
"Sababu iliyonifanya nijiunge na al-Shabab ni pesa," amesema Ahmed, mzungumzaji mzuri kati ya watatu hao. "Walinilipa kuanzia dola 200 hadi dola 300 kwa mwezi. Nilisimamia mfumo wa usafirishaji katika eneo langu."
Ibrahim anakutanisha vidole vyake kwa pamoja akiashiria pesa. "Nilijiunga kwasababu ya pesa. Nilikuwa mwanajeshi wa al-Shabab wa kutembea kwa miguu kwa miaka mitatu. Ukiwa ndani unafurahia.
"Kile ambacho sikuwahi kukifurahia nikiwa mwanamgambo wa al-Shabab ni vile walivyojaribu kubadilisha akili yangu."
Kila wiki mbili wanatuma timu ya watu wakutubadilisha akili katika kikosi chetu ambao hutukalisha kwa saa kadhaa kukariri kitabu takatifu cha Koran na kurejelea kila saa vile serikali, Umoja wa Afrika na washirika wake wengine wa kimataifa walivyo makafiri na waasi-imani.
"Ni kana kwamba walikuwa wanatuingiza kadi za al-Shabab katika ubongo wetu."

Wanaume watatu wanasema hata wakati wanawafundisha mambo ya kuwabadilisha akili, ilifika muda wakafahamu kwamba kundi hilo halikuwa linapigana vita vitakatifu kama lilivyokuwa linadai ili kuimarisha Uislamu, lakini ni lenye njia zisizo wazi na za kupotosha. Na hata pesa walizokuwa wanalipwa hazikuwa sababu tena ya kuwafanya kusalia ndani ya kundi la al-Shabab.
Hata hivyo, uamuzi wa kuasi ulikuwa wa kuogofya zaidi ya kitu kingine chochote maishani mwao, wanasema.
Kwanza walitoroka, na kilichofuata ikawa ni safari yenye upweke ya kuondoka katika eneo la al-Shabab.
"Mwanzoni nilikuwa nikitembea usiku tu, miguu ilipasuka pasuka," Ahmed anasema. "Kwa bahati nzuri nilikuwa na simu yangu kwahiyo nilichofanya ni kuwasiliana na familia yangu.
Wakapata mtu ambaye ningeweza kumuamini aliyenielekeza hadi sehemu salama. Ilichukuwa siku kadhaa na kipindi chote hicho kila hatua niliopiga nilikuwa na hofu ya maisha yangu.
Nilikuwa na wasiwasi sana wa kusimamishwa na kurejeshwa kwa mamlaka ili nikabiliwe na adhabu ya kifo, kwa kuuliwa mbele ya umma, kwasababu hivyo ndio al-Shabab hufanya kwa wanaoasi"

Lakini pia kuna hofu upande wa pili wa kile kitakachotokea, wanamgambo waandamizi wanawaambia wasajili kuwa walioasi watateswa kwa kutumia umeme na vikosi vya usalama Somali.
Wengi hawajui serikali ni yenye kusamehe na pia kuna kituo cha urekebishaji tabia ambapo wataelimishwa na kurejeshwa tena katika jamii.
Hizo ni mbinu za kusambaza malengo ya al-Shabab juu ya walioasi.
Kuna vipeperushi ambavyo vimetengenezwa na vina picha kwa wale wasioweza kusoma na kuandika vinavyoonesha idadi ya wanamgambo wa al-Shabab waliookolewa na namba ya simu wanayoweza kupiga.
Hata hivyo kinachotokea ni idadi ya wanaoasi kuongezeka huku zaidi ya watu 60 wakitoroka kundi la al-Shabab katika kipindi cha miezi miwili mwanzoni mwaka huu.

Ibrahim, ambaye alikuwa na kundi la al-Shabab kwa miaka mitatu, ilimchukua miezi miwili kuamua kutoroka kundi hilo.
Anasema hatawahi kurejea katika kijiji anachotokea - na atajitahidi kadiri ya uwezo wake kusalia mji wa Mogadishu.
La sivyo, kundi la al-Shabab litamtafuta na kumuua.
Wanaume wote watatu waliishia katika kituo cha kurekebisha tabia cha Mogadishu, mji mkuu wa Somali.
Vitisho dhidi yao ni vya juu kiasi kwamba walipotembelewa walikuwa na walinzi 80 wanaolinda watu 84 waliotoroka kundi la al-Shabab.
Lakini kituo ch akurekebisha tabia cha Mogadishu ni cha wale wa waliokuwa wanachama wa ngazi ya chini huku wale walioasi ambao walikuwa na vyeo vya juu katika kundi hilo wakiwa na kituo chao.
Kabla ya kujumuishwa kwenye kituo cha urekebishaji tabia, walioasi wanachunguzwa na kitengo cha taifa cha ujasusi na kikosi cha usalama kuhakikisha kuwa wametoroka kundi hilo kwa kupenda kwao na pia wanashutumu itikadi zao.
Lakini mwanahabari mmoja Mogadishu anasema kuwa baadhi ya wanachama wa al-Shabab hufuatilia walioasi na kutumiwa ujumbe.

Lengo la kituo cha urekebishaji tabia ni kuwarejesha walioasi katika mstari kimwili, kiakili na kiimani ili kuwapa maarifa na taratibu waweze kuzoea maisha ya kawaida ama kwa kurejea katika jamii zao au hata kwenda kwengineko.
"Niliendesha gari lilokuwa linabeba silaha ambalo tuliliita 'Volvo', nilipokuwa katika kundi la al-Shabab. Na sikuogopa chochote," Moulid anasema.
"Nilipowasili baada ya kujisalimisha, msimamizi alitambua kipaji changu cha uendeshaji gari. Na nikafanyakazi kama dereva mwelekezi ndani ya kambi, na kufundisha wengine namna ya kuendesha gari. Sasa nimepata kazi kama dereva wa basi la shule. Ndoto yangu nikuendesha biashara yangu mwenyewe ya usafirishaji."
Ahmed naye sasa hivi anajihusisha na biashara ya ununuaji na uuzaji wa ardhi.
Ibrahim anaelezea vile alivyojifunza kuwa kinyozi katika kituo cha urekebishaji tabia.
Sasa hivi amefungua kinyozi chake Mogadishu ambapo ameajiri watu watatu. "Napata pesa nzuri zinazoniwezesha kukimu mahitaji ya wake zangu wawili na watoto wanane," anasema na kuongeza kuwa amewaleta mjini ambako anaishi nao.

Lakini je maisha baada ya kuwa al-Shabab yakoje?
Wanaume hao watatu wanakiri kuwa sio rahisi.
Moulid anaelezea kuwa baadhi ya watu wa familia yake wamemkana na wengine hawamuamini.
Ibrahim anasema hangeweza kurejea katika jamii yake hata kama hakungekuwa na hatari ya yeye kutafutwa na wanamgambo wa al-Shabab kwasababu ingawa familia yake imemsamehe, majirani zake bado.
And he says that deep inside he still has wounds from his time in al-Shabab - that he is haunted by it.
Na pia anakiri kuwa kuna mambo ya al-Shabab ambayo bado yanamuandama.
"Nina changamoto ya kufuta ile kadi ya al-Shabab kutoka kwenye ubongo wangu," anasema. "Picha za mambo mabaya niliofanya na mambo mabaya niliofanyiwa bado huwa nayakumbuka."

Na ndani ya kituo cha urejebishaji tabia, walioasi hufundishwa mambo ya msingi, lugha ya kiingereza, somo la hesabu na mengineo. Wengine wanajifunza makanika, kuchomelea vyuma, habari na teknolojia, udereva ba ujuzi mwingine.
Pia unaweza kutazama:













