Rais wa Uganda Yoweri Museveni atishia kuyaondoa majeshi yake Somalia
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametishia kuyaondoa majeshi ya nchi yake katika mpango wa usalama nchini Somalia.
Moja kwa moja
Korea Kaskazini yaadhimisha kuanzishwa kwa taifa hilo kimya

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Korea Kaskazini Korea Kaskazini imefanya maonesho ya gwaride la kuadhimisha miaka 73 tangu kuasisiwa kwa taifa hilo, lakini haikuonyesha silaha.
Mwandishi wa BBC anasema nchi hiyo haikuonesha makombora yake ya masafa marefu mara hii, wala mbwa wa kuwinda na vifaru vya kijeshi.
Rais Kim Jong-un alihudhuria sherehe hizo, lakini hakuzungumza kama kawaida yake.
Wachambuzi wa siasa wanasema seikali ya Korea Kaskazini inataka kuonesha dunia kwamba juhudi zake kwa sasa zimeelekezwa zaidi katika maswala ya ndani ya nchi.
Jinsi mtandao ilivyofurika picha za 'kejeli' kuhusu mapinduzi ya rais wa Guinea
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mashindano yanaendelea kwenye mtandao wa Twitter huku kila mmoja akijitahidi kupata muonekano wa rais wa Guinea Alpha Condé baada ya jeshi kumpindua katika mapinduzi yaliyofanyika Jumapili.
Picha ya Bw Condé mwanye umri wa miaka 83- ilisambazwa sana baada ya kukamatwa na wanajeshi.
Katika picha hiyo Bw Condé, ambaye alikuwa amezingirwa na wanajeshi, alinaonekana akiwa miguu peku huku akiwa ameketi kwenye kochi huku vifungo vya shati lake vikiwa wazi na kifua chake kikionekana.
Hawa ni baadhi ya washindani wakuu katika kampeni ya Twitter: #AlphaCondeChallenge:
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Ruka X ujumbe, 4Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Ruka X ujumbe, 5Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 5
Wapiganaji wa Tigray wapigwa Afar - Ethiopia

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Shule nyingi, hospitali na nyumba vimeharibiwa katika vita Serikali ya shirikisho ya Ethiopia imesema wapiganaji kutoka kaskazini mwa Tigray wameshindwa vita katika eneo la jirani la Afar na wameondoka eneo hilo.
Jeshi la Tigrayan limekanusha kupigwa .
Wanasema walihamisha jeshi lao eneo la Amhara kwa kuwa hakukuwa na mapigano yeyote Afar.
Kumekuwa na ghasia katika maeneo yote katika wiki za hivi karibuni , huku kila upande ukilaumu mwengine kukiuka haki za binadamu.
Kufungiwa kwa mitandao ,kumefanya kuwa na ugumu katika kudhibitisha taarifa kuhusu vita hiyo ambayo imekuwa ikiendelea karibu miezi kumi na moja.
Mashabiki wa soka waliochanjwa kuangalia mechi bure Afrika Kusini

Chanzo cha picha, AFP
Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini limesema mwezi ujao litatoa tiketi za bure kwa mashabiki wote wa soka waliopata chanjo ya corona kuingia bure uwanjani kushuhudia mechi za kufuzu kombe la dunia kati ya timu ya taifa hilo Bafana Bafana, na Ethiopia.
Shirikisho hilo limesema , mashabiki waliopata chanjo watapewa kipaumbele katika mechi na matukio mengine ya kiburudani.
Serikali ya Afrika ya kusini imekuwa ikiongeza juhudi katika kuwahamasisha watu kupata chanjo.
Ni watu milioni 10 tu ndio wamepata chanjo hiyo mpaka sasa ingawa serikali inahitaji kuwafikia watu 40.
Mzozo waibuka Somalia baada ya Waziri wa Usalama kufukuzwa kazi na Waziri Mkuu

Mzozo baina ya Rais na Waziri Mkuu wa somalia umeendelea kushika kasi baada ya tukio la kuondolewa kwa Waziri wa Usalama nchini humo.
Waziri Mkuu Mohamed Roble alimfukuza kazi waziri huyo siku ya Jumatano, jambo ambalo halikukubaliwa na Rais Mohamed Abdullahi Farmajo.
Roble aliamua kumuweka Waziri wa Ulinzi mwingine Hassan Hundubey Jimale kuwa mbadala wa Abdullahi Mohamed Nur huku Rais Farmajo akidai kuwa kitendo alichofanya msaidizi wake kinakiuka misingi ya katiba ya nchini humo.
Tukio hili ni la pili kutokea la Waziri Mkuu kufanya maamuzi bila ya kumshirikisha Rais, wiki iliyopita alimfukuza kazi mkuu wa kitengo cha upelelezi kwa madai ya kutoa ripoti ya kutoweka kwa afisa wa kitengo cha usalama.
Viongozi hawa wawili wameamua kuonesha hadharani tofauti zao na hata sera zao zisizoendana.
Rais Farmajo ameondoa makubaliano yaliyowekwa kwa waangalizi wa kimataifa huku Waziri Mkuu akionekana nchini Kenya kusaini makubaliano hayo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni atishia kuyaondoa majeshi yake Somalia

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametishia kuyaondoa majeshi ya nchi yake katika mpango wa usalama nchini Somalia.
Licha ya kwamba sio mara ya kwanza kwa Rais huyo kutishia ,amekuwa akifanya hivyo baada ya viongozi wa nchi hiyo kuhatarisha amani ya nchi hiyo na mpango wa uchaguzi unaopangwa kufanyika.
Akizungumza na chombo cha habari cha Ufaransa ‘France 24’ Rais Museveni amejibu swali aliloulizwa kuhusu mpango wake wa kuondoa majeshi yake ya UPDF nchini Somalia baada ya ongezeko la mashambulizi kutoka kwenye kundi la waasi la Al-Shabab pamoja na mgogoro wa kisiasa nhini humo.
Akielezea mgogoro wa kisiasa nchini Somalia mwaka 2011, Museveni alitaka maelewano ambayo yalipelekea kujiuzulu kwa aliyekuwa
Waziri Mkuu kipindi hicho Mohamed Abdullahi Farmaajo ambaye kwa sasa anahudumu kama Rais na katika kipindi hicho Museveni alitishia kuondoa majeshi yake.
Uganda inakuwa nchi ya kwanza kupeleka majeshi yake nchini Somalia kupitia mwamvuli wa kulinda amani Afrika wa mwaka 2007.
Wakati huo, Al-Qaeda wakishirikiana na Al-Shabaab walitishia kuiondoa madarakani serikali iliyokuwa ikungwa mkono na mataifa ya Magharibi. Wiki chache baadae, Uganda ilituma jeshi lake baada ya Azimio la Umoja wa Mataifa lililofanyika mwezi Machi, kuusaidia Umoja wa Afrika nchini Somalia hadi Disemba mwaka huu.
Museveni akielezea juu ya msimamo wake alisema kuwa hana imani sana majeshi yanayotoka nje ya Afrika lakini kutokana na kwamba kazi inayopaswa kufanywa ni kubwa basi hakukuwa na muda kushikilia maneno yake.
Amesema kuwa, maamuzi ya kujiondoa kwa majeshi yake yanaweza kufuata utaratibu wa mazungumzo na Umoja wa Afrika lakini ameona ni muda sasa wa wao wajilinde wenyewe.
Siku ya jumatatu, majibizano baina ya Rais na Waziri Mkuu wa Somalia yameendelea baada tu ya kufukuzwa kazi mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa.
Hata hivyo, inawezekana uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu ukasogezwa mbele baada ya uchaguzi wa wabunge kupelekwa mbele mwisho wa mwezi Novemba.
Kenya yatangaza ukame kuwa janga la taifa

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa ukame umeathiri baadhi ya sehemu za Kenya na hivyo ni janga la taifa.
Ukame huo umeathiri kaunti 10 kati ya kaunti 47 . Watu wapatao milioni mbili wameathirika nchini Kenya.
Rais ametaka wahanga wa janga hilo kusaidiwa na wizara ya mambo ya ndani.
Rais ametangaza hayo baada ya mkutano na viongozi wa eneo lililoathirika kaskazini mwa nchi hiyo, ambako hawajapata mvua kwa kiwango cha nusu ya 50%.
Wakazi wa eneo lililoathirika ,ambao ni wafugaji wanakabiliwa na njaa na wanyama wao wanakufa.
Serikali imesema itachukua hatua madhubuti kukabiliana na ukame huo.
Martha Koome: Idara ya mahakama Kenya iko huru -haina wagombeaji inayowapendelea

Chanzo cha picha, ZAKHEEM RAJAN
Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome amesema idara ya mahakama nchini humo iko huru na itatekeleza kazi yake bila muingilio wowote wa kisiasa .
Katika mahoojiano na BBC Koome ambaye ni mwanamke wa kwanza nchini humo kushikilia wadhifa huo amesema idara hiyo inajitayarisha vilivyo kuzishughulikia kesi zitakazotokana na uchagui mkuu wa mwaka ujao nchini Kenya .
‘Tuko mbioni kujitayarisha kwa mafunzo kuhusu masharti,kanuni na utaratibu wa uchaguzi na sheria zinazofaa kutumika.Tunawahakikishia wakenya kwamba tuko huru hatuna mgombeaji ama wagombeaji tunaowapendelea ‘ amesema Koome .
Koome amesemaana matumaini makubwa ya kufanikisha wajibu wa idara ya mahakama lich ya kuwepo changamoto mbali mbali anapotimiza siku 100 tangu ateuliwe katika nafasi hiyo
Amekiri kwamba ufisadi miongoni mwa maafisa wa idara hiyo na mrundiko wa kesi bado ni changamoto zinazofaa kushughulikiwa .
‘ Nina matumaini tunaweza kufanya vizuri katika idara ya mahakama ,ili kutekeleza jukumu kubwa kama walinzi wa kikatiba,sheria na wateteziwa haki za binadamu’ amesemaKoome
Jaji Koome amesema uhusiano kati ya serikali na idara ya mahakama ni jambo muhimu kufanikisha shughuli za serikali kwa wananchi .
Amesema idara zote za serikali zinategemeana na pana haja ya kulinda uhusiano mzuri.
Koome pia amesema idara ya mahakama nchini Kenya ingali inahitaji majaji Zaidi. Amesema wanahitaji majaji 20 wa mahakama kuu ili kuweza kushughulikia mrundiko wa kesi .
Demokrasia Afrika
Akizungumza kuhusu hali ya demokrasi katika bara la Afrika Koome amesema kuna baadhi ya mambo kama vile mapinduzi yanayofanywa na majeshi kama kikwazo kwa demokrasia .
Hata hivyo amesema Afrika ina sababu ya kufurahia hatua nzuri kama makabidhiano nay a madaraka kwa njia ya Amani katika baadhi ya nchi .
Mtu wa wadhifamkubwa kama yeye hufanya nini wakati hayupo kazini? Koome amesema wakati yuko nyumbani basi;
‘Mimi ni mama nyumbani ,napika ,nawakaribisha wageni wangu,naenda mashambani naenda kanisani na hata kuwafunza watoto jumapili’ anahitimisha Jaji huyo mkuu
Watoto wauzwa kwa dola 10, Tanzania

Maelezo ya picha, Kamanda wa Polisi Mbeya Ulrich Matei Vyombo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuhusu kukamatwa kwa watu wawili na jeshi la polisi mkoani Mbeya nyanda za juu kuini mwa Tanzania, wakihusishwa na tuhuma za kuuza watoto.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwasafirisha watoto 11 wenye umri kati ya miaka 10 mpaka 14 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kuwauza kwa wafugaji.
Mkuu wa jeshi la polisi Mbeya bwana Urlich Matei alisema watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 5, 2021 saa mbili usiku katika wilaya ya Mbarali wakiwa kwenye harakati za kuwasafirisha watoto hao.
Alisema watuhumiwa hao walikuwa wanauzwa kwa wafugaji kwa gharama ya fedha za kitanzania shilingi 25,000 au 30,000 ambazo ni sawa na dola 10-12$.Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Daniel Julius (21) na Kamungu Julius (30) wote wakazi wa wilaya ya Mbarali .
Aidha taarifa zinasema baada ya watoto hao kutoonekana kwa muda mrefu, baadhi ya familia zilianza kuweka msiba zikiamini kuwa watoto wao wamefariki.
Wakenya waendelea kutuma risala zao kufuatia kifo cha Orie Rogo Manduli

Chanzo cha picha, ORM/TWITTER
Wakenya wanaendelea kutoa risala zao baada ya kifo cha Orie Rogo Manduli, mwanamke ambaye wengi walimfahamu mtindo wake wa mavazi ya kupendeza na aliyekuwa mwanamkealiyevunja rekodi kadhaa kwa kutangulia kuafikia mambo mengi.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Alikuwa wa kwanza kushinda shindano la urembo la Miss Kenya na pia dereva wa kwanza mwanamke wa mbio za magari . Aliaga dunia jana akiwa na umri wa miaka 73.
Wengi wanamkumbuka kwa vazi lake la kichwa lililosheheni vitamba vya rangi mbali mbali za kuvutia na muonekanao wake uliwavutia wengi kote alikokwenda
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Manduli pia alikuwa mwanamke wa kwanza kuongozabaraza la mashirika yasio ya kiserikali ambalo ka wakati mmoja lilikuwa na nguvu nchini Kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyattaakimuomboleza Manduli alimtaja kama ‘Mtu aliyekuwa mstari wa mbele kupigania haki za wanawake’

Chanzo cha picha, SM/Twitter
Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo waua 120 DRC

Chanzo cha picha, WHO
Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo au meningitis umetangazwa kaskazini- mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Mpaka sasa watu zaidi ya 120 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.
Mgonjwa wa kwanza nchini DRC aliripotiwa Julai.
Zaidi ya watu 100 wamepata tiba wakiwa nyumbani au vituo vya afya.
Mlipuko huo umekuwa mgumu kukabiliana nao kwa kuwa jamii inauhusisha na uchawi, shirika la afya duniani (WHO) limeiambia BBC.
Sampuli zilizotumwa Ufaransa zimebaini kuwa bakteria wanaohusika na mlipuko huo wanaweza kusababisha janga kubwa.
Watu wengi wamekufa na jamii inapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwajibika.
Badala ya kutafuta tiba, baadhi ya watu wamekuwa wakitoka sehemu moja kwenda nyingine wakiwa na matumaini kuwa ugonjwa huo hautawafuata.
Serikali ya DRC na WHO wametuma vikosi vya watumishi wa afya kaskazini mashariki mwa jimbo la Tshopo ili kukabiliana na hali hiyo.
Baadhi yao hawana uwezo na wako katika hatari kwa milipuko ya mara kwa mara haswa wakati wa kiangazi - kutoka Januari hadi Julai.
Meningitis, ni ugonjwa ambao unaweza kusababisha kifo, unaambukiza kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kupitia matone, akipumua au akikohoa.
Afghanistan: Rais wa zamani Ashraf Ghani aomba msamaha kwa kukimbia nchi

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa zamani wa Afghanistan Ashraf Ghani ameomba msamaha kwa watu wa Afghanistan baada ya kukimbilia katika nchi za Falme za Kiarabu.
"Kuondoka Kabul ulikuwa uamuzi mgumu zaidi maishani mwangu," amesema, akiongeza kuwa anajuta kwamba "hakuweza kumaliza hilo kwa njia tofauti."
Bwana Ghani aliondoka ghafla nchini Afghanistan wakati wanamgambo wa Taliban walipokuwa wakiendelea kuingia kwenye mji mkuu mnamo Agosti 15.
Alisema hakuwa na nia ya kuwaacha watu wake lakini "ilikuwa ndio njia pekee iliyosalia."
Katika taarifa iliyoshirikishwa kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumatano, Bw. Ghani alisema hakuwa na njia nyingine yoyote zaidi ya kuondoka nchini humo ili kuepusha kuenea kwa ghasia.
"Niliondoka kwa kushawishiwa na usalama wa ikulu, ulionishauri kuwa kuendelea kuwepo kulihatarisha kutokea kwa mapigano mitaani na katika barabara za mji kama ilivyotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1990," aliandika, akiongeza kuwa alifanya hivyo "kuokoa mji wa Kabul na raia wake milioni sita".
Alisema alikuwa amejitolea kwa kipindi cha miaka 20 kusaidia Afghanistan kuwa "nchi ya kidemokrasia, mafanikio na huru."
Bwana Ghani ameongeza kuwa alikuwa na "masikitiko makubwa" kwamba "muda wangu mwenyewe uliishia kwa majuto kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wangu."
Rihanna atupilia mbali kesi dhidi ya baba yake mahakamani

Mwanamuziki Rihanna ametupilia mbali kesi dhidi ya baba yake, wiki chache kabla ya siku waliopaswa kukutana mahakamani.
Nyota huyo wa muziki aina ya pop alikuwa amemshtaki baba yake, Ronald Fenty, kwa kutumia jina lake vibaya kunufaisha kampuni yake ya burudani, na alimshtaki mnamo mwaka 2019 kwa matangazo ya uwongo na kuingilia maisha yake kwa hali iliyokiuka haki zake za kuwa na siri
Alisema pia kwamba alijaribu kumsajili katika safari yake ya nje ya nchi bila ruhusa.
Kesi hiyo ilitakiwa kuanza kusikilizwa mnamo Septemba 22, lakini Rihanna aliwasilisha ombi la kuitupilia mbali kesi hiyo Jumanne.
Hakuna sababu iliyotolewa, lakini ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha kwamba walifikia makubaliano ya kutatua mzozo wao nje ya mahakama na baba yake na mwenza wake wa kibiashara.

Chanzo cha picha, Getty Images
Rihanna, ambaye jina lake kamili ni Robyn Rihanna Fenty, alifungua kesi miaka miwili iliyopita, akisema: "Ingawa Bwana Fenty ni baba wa Rihanna, hana, na hajawahi kuwa na mamlaka ya kuchukua hatua kwa niaba ya Rihanna."
Alidai kuwa mnamo mwaka 2017, baba yake na mtu mwingine, Moses Perkins, waliunda kampuni inayoitwa Fenty Entertainment, ambayo ilidai mara kwa mara kuwa inahusiana na Rihanna.
Katika nyaraka za mahakamani, mawakili wake walisema: "Bwana Fenty na Bwana Perkins wametumia uwongo huu katika juhudi za kulaghai mamilioni ya madola kutoka kwa watu wengine kwa mabadilishano ya ahadi za uwongo kwamba wameidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya Rihanna."
Walidai kuwa kampuni ya Fenty Entertainment ilijaribu kusajili safari ya tarehe 15 Marekani Kusini yenye thamani ya $ 15m (£ 11m), na vile vile maonyesho huko Los Angeles na Las Vegas, bila Rihanna kujua.
Kwa kuongezea, walidai kwamba Ronald Fenty alikuwa akijaribu kufaidika na utambulisho wa nembo ya kibiashara ya "Fenty", ambayo Rihanna ameitumia kwa biashara zake kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya vipodozi ya mamilioni ya fedha, Fenty Beauty.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baba yake hapo awali alijaribu kuanzisha nembo yake ya kibiashara kwa kutumia jina Fenty, kama sehemu ya mpango wa kufungua msururu wa hoteli ambazo mtu pia anaweza kufanya manunuzi, alidai.
Hata hivyo, ofisi inayosimamia hataza na nembo za kibiashara Marekani ilikataa ombi hilo.
Akiomba kutolewa kwa agizo la kumzuia baba yake na mwenzi wake wa kibiashara kuchukua hatua hiyo, Rihanna alisema shughuli zake za biashara zilikiuka matangazo, ushindani na sheria za faragha na pia kulihatarisha "jeraha kubwa lisiloweza kutibiwa" kwa kmpuni ya Fenty ikiwa hatua hiyo haitasimamishwa.
Mwimbaji huyo, ambaye ni miongoni mwa wanamuziki tajiri duniani, kwa muda mrefu amekuwa na uhusiano mbaya na baba yake, ambaye awali, aliwahi kupambana na uraibu wa pombe na dawa za kulevya.
Hakuna kati ya wawili hao aliyepatikana mara moja kutoa maoni yake juu ya kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo ya kisheria.
Guinea yafukuzwa kutoka Jumuiya ya ECOWAS kufuatia mapinduzi ya kijeshi

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS wameiondoa Guinea kutoka jumuiya hio kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Jumapili ambayo yalimwondoa Rais Alpha Conde madarakani .
Uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia mkutano uliofanywa kwa njia ya mtandao Jumatano. Kulingana na Reuters, uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry.
Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS alisema kuwa mapinduzi ya kijeshi yalikiuka makubaliano ya jumuiya hiyo kuhusu utawala bora.
Umoja wa Afrika na ECOWAS wamelaani mapinduzi hayo ya kijeshi.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo Alhamisi tarehe 9,Septemba 2021
