Afrika mashariki: Wafahamu nyota wa Tanzania,Kenya na Uganda wanaoipeperusha bendera ya Afrika mashariki duniani

hata zaidi bendera ya Afrika Mashariki kwa sababu Netflix ina zaidi ya watu milioni 203.7 wanaoiumia huduma hiyo kutazama filamu .

Chanzo cha picha, Twitter/IDRIS SULTAN

Muda wa kusoma: Dakika 4

Afrika mashariki imejaa nyota katika ulingo wa kimataifa kwa kuipeperusha bendera yake .Iwe ni katika michezo, sanaa na sayansi watu mbalimbali wameziletea sifa nchi za Afrika mashariki katika nyakati tofauti katika miaka ya hivi karibuni .

Kuna ambao muziki wao umeiweka Tanzania katika ramani ya burudani Afrika ,na majina maarufu hapa ni kama mwanamuziki Diamond Platinumz na wenzake wengi .

Hatahivyo pia kuna wengine ambao wamezidi kuipa sifa Afrika mashariki katika tasnia za michezo . Hawa hapa baadhi ya nyota hao ambao kazi zao na talanta zimewapa fursa ya kuwaletea Waafrika mashariki sifa na kutambuliwa .

Idris Sultan

Raia huyo wa Tanzania ni muigizaji na sasa ni muigizaji wa kwanza kutoka nchi hiyo kuhusishwa katika filamu iliyo kwenye mtandao wa Netflix .

Sultan ambaye pia ana wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii alifurahi sana kwa mafanikio hayo na aliwaambia wafuasi wake takriban milioni 6.6 kwenye instagram kwamba alifurahia sana heshima ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika tasnia ya filamu kwa kuhusika kwake na filamu hiyo kwa jina Slay.

Mshindi huyo wa zamani wa Big Brother Africa ni miongoni mwa majina mengine maarufu katika filamu hiyo wengine wakiwa Ramsey Naouh, Enhle Mbali, Dawn Thandeka Kang, Tumi Marake, Trevor Gumbi, Lillian Dube, Kaly Boss Asante, Shaleen Surtie na Fabiaa Lojege.

Aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ni miongoni mwa walioguswa sana na hatua aliyeipiga kijana huyu.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kushirikishwa kwa Idris katika filamu hiyo ya Netflix kutampa ukumbi mzuri wa kuipeperusha hata zaidi bendera ya Afrika Mashariki kwa sababu Netflix ina zaidi ya watu milioni 203.7 wanaoiumia huduma hiyo kutazama filamu .

Bruno Tarimo (vifua viwili)

Bruno Tarimo bondia raia wa Tanzania ambaye kwa sasa anaishi nchini Australia .

Alizaliwa tarehe 16 Juni mwaka wa 1995,huko Kilimanjaro . kwa sasa yeye ndiye bingwa wa IBF wa taji la Super Feather. Ameshiriki mapambano 30 na ameshinda 26 na kushindwa mawili huku akitoka sare katika mapigano mawili .

Bruno hata hivyo anasema nchi za kiafrika zinafaa kuweka mikakati ya kuwasaidia wanandondi .

Amesema changamoto kwa wanaspoti kama yeye ndizo zinazomfanya kufanya uamuzi wa kuamua kupigia ndondi yake nchini Australia . Akiwa nje ya nchi anasema inakuwa changamoto kwa bondia kupata ufadhili kama haungwi mkono na wadau wa nchi anakotoka.

Bruno hata hivyo anasema nchi za kiafrika zinafaa kuweka mikakati ya kuwasaidia wanandondi

Chanzo cha picha, Bruno Tarimo

Lupita Nyong'o

Lupita Amondi Nyong'o ni muigizaji kutoka Kenya ambaye alizaliwa mwaka wa 1983. Binti wa mwanasiasa Anyang' Nyong'o ,Lupita alizaliwa Mexico City ambako babake alikuwa akifundisha na alilelewa Kenya tangu akiwa na umri wa mwaka mmoja .

Alipata umaarufu mwaka wa 2013 aliposhinda tuzo ya muigizaji msaidizi bora katika filamu ya 12 years a slave na kuwa mkenya wa kwanza kushinda tuzo ya Oscar

Chanzo cha picha, AFP

Nyong'o alianza taaluma yake ya uigizaji Hollywood kama msaidizi wa uzalishaji wa filamu . mwaka wa 2008 alishirikishwa katika filamu yake ya kwanza East River na akarejea kenya kuhusishwakatika filamu ya msururu ya Shuga (2009-2012). Mnamo mwaka wa 2009 aliandika na kuielekeza filamu ya In My Genes.

Alipata umaarufu mwaka wa 2013 aliposhinda tuzo ya muigizaji msaidizi bora katika filamu ya 12 years a slave na kuwa mkenya wa kwanza kushinda tuzo ya Oscar . Tangia hapo amezidi kushirikishwa katika filamu mbali mbali ambazo zimemjengea sifa na jina na kuiweka Afrika mashariki katika ramani ya uigizai

Eliud Kipchoge

Chanzo cha picha, Eliud Kipchoge/Facebook

Eliud Kipchoge

Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge ni jina kubwa sasa katika riadha sio tu nchini Kenya bali kote duniani.

Alizaliwa mwaka wa 1984 na ameshinda mataji mbali mbali ya riadha ikiemo kuwa bingwa wa olimpiki katika mbio za marathon mwaka wa 2016 huo Rio na ubingwa wa dunia katika mbio za mita 5000 mwaka wa 2003 nchini Ufaransa .

Pia alivunja rekodi kwa kuwa mtu wa kwanza kuvunja rekodi ya kumaliza mbio za marathon chini ya muda wa saa mbili kwa kukimbia kwa muda wa saa 1.59.40.2.

Baada ya umaarufu wake kuenea amekuwa akiyawakilisha mashirika na kampeni mbali mbali kama balozi wa nia njema na ni miongoni mwa nyota wanaotambuliwa kwa urahisi kama anayetoka Kenya na Afrika mashariki kwa sababu ya mafanikio yake uwanjani.

Bobi Wine

Kando na kujijengea sifa kama mwanamuziki ,Bobi Wine ni mwanasiasa ambaye hatua yake ya kutaka kupigania nafasi ya uongozi kupitia kura Uganda na kuwataka vijana kupewa nafasi katika meza ya uongozi hatua ambayo imewavutia wengi na hata nje ya nchi anaonekana kama mpiganiaji mkubwa wa demokrasia afrika mashariki .

Bobi Wine

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanasiasa wengi nchini mwake na Afrika mashariki wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu wakati alipowania urais dhidi ya rais Yoweri Museveni na ukakamavu wake ulimpa sifa sio tu kama mwanasiasa kijana bali pia kilelezo kwa waliotaka kupewa fursa za uongozi ili kubadilisha hali ya maisha ya awatu wao .

Kando naye nchini Uganda pia kuna wasanii ambao wameiwakilisha vyema Uganda na afrika mashariki kama vile , Jose Chameleone, Eddy Knzo na Bebe Cool

Daniel Kaluuya

Ingawaje Daniel Kaluuya sio mganda kwani ni raia wa Uingereza wazazi wake ni waganda na hajasahau chimbuko lake . Ameshinda tuzo ya Oscar wiki hii kwa kuwa muigizaji bora msaidizi wa mwaka wa 2021 kwa filamu yake ya 'Judas and the Black Messiah'.

Ushindi wake ulisherehekewa kote afrika mashariki na mama yake pamoja na dada yake waliokuwa katika hafla ya tuzo hizo walibubujikwa machozi ya furaha wakati Kaluuya alipokuwa akitoa hotuba yake

Licha ya kuwa ni raia wa Uingereza ,wengi wamejivunia chimbuko lake la Uganda na Afrika mashariki

Chanzo cha picha, Reuters

Alizaliwa London na alilelewa na mama yake Damalie Namusoke wakati baba yake alipokuwa akiishi Uganda na haikuwa rahisi kwa baba yake kuwazuru Uingereza kwa sababu ya masharti ya visa .

Licha ya kuwa ni raia wa Uingereza ,wengi wamejivunia chimbuko lake la Uganda na Afrika mashariki.