Ukiwaangalia nyota hawa utadhani ni wachanga lakini wana miaka mingi

INSTAGRAM/KATE HENSHAW

Chanzo cha picha, INSTAGRAM/KATE HENSHAW

Kuna watu ambao umri wao hauwezi kukadirika na licha ya kuwa na miaka mingi ,muonekano wao unasalia kuwa wa ujana .

Ushawahi kumjua mtu tangia zamani na hadi sasa hajabadilika?Basi sio hao tu unaowajua kwani kuna nyota kadhaa wa muziki na filamu ambao kwa miaka mingi wamesalia kama walivyokua walipojitosa katika fani ya burudani .

Wiki hii muigizaji wa Nigeria Kate Kate Henshaw alipambana mitandao ya kijamii akisherehekea miaka 50 tangu kuzaliwa kwake na hakuna aliyeamini kwamba ametimu umri huo.

Kando na Kate kunao pia wasanii ambao wanafahamika kote ulimwenguni ambao mashabiki wengi wamekuwa wakishangaa ni ka namna gani wamefaulu kujiweka vizuri na kusalia na muonekana wa ujana hadi sasa .Hii hapa orodha ya mastaa wasiopoteza ujana licha ya umri wao wa juu

Kate Henshaw

Muigizaji maarufu wa filamu za Nollywood Kate Henshaw wiki hii alisherehekea miaka 50 tangu kuzaliwa kwake .

Aliziweka picha kadhaa katika mitandao yake ya kijamii na wengi wa mashabiki wake walishangaa kwamba alikuwa ametimu umri wa miaka 50.Kwa mtu yeyote kutakiw akukadiria umri wake ,ungefikiri labda ana miaka 30 lakini Kate amekula chumvi kwa miongo mitano.

Kate Henshaw

Chanzo cha picha, Kate Henshaw

Akimshukuru mungu kwa kumpa mwili mzuri wa ujana ,Kate alimiminiwa sifa na wengi katika mitandao ya kijamii waliomtakia maisha marefu . Wengi walitaka kujua anachokifanya kila siku ili kusalia na muonekano wa ujana

Ndoa

Kate Henshaw aliolewa na raia wa Uingereza Roderick James Nuttal mwaka wa 1999 na wakajaaliwa mtoto wa kike mnamo mwaka wa 2000.Hata hivyo ndoa yao ya miaka 12 iliisha na kila mtu akashika njia yake .

Kuhusu alivyoweza kusalia na muonekana wa ujana ,anasema yeye hupenda kudensi na kufanya mazoezi.

Kate ameshinda tuzo nyingi za filamu na kushirikishwa katika filamu nyingi za Nigeria zikiwemo "When the Sun Set' 'Chief Daddy','The Wives', 'Games Men Play', 'Scars of Womanhood', 'Roti', miongobni mwa nyingine nyingi

Will Smith

WS

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanzoni mwa milenia, Will Smith alikuwa na miaka 21.

Leo, mwigizaji huyo anayeonekana mchanga bado yupo katika sinema kubwa za Hollywood. Hivi karibuni, alionekana tena akicheza kama Mike Lowrey katika filamu "Bad Boys for Life." Smith kwa sasa ana umri wa miaka 52 .

Jenifer Lopez

JLO

Chanzo cha picha, Getty Images

Jennifer Lopez ana miaka 51 lakini inaonekana kama yuko vile vile kama alivyokuwa miaka 20 iliyopita.

Hakuna anayeamini jinsi J. Lo anavyoonekana bado mdogo kama ilivyokuwa miongo miwili iliyopita na kwamba sasa tayari yuko kwenye miaka ya 50.

Baada ya tamasha la mwaka jana la Super Bowl kila mtu aliachwa akizungumzia namna mwanamuziki huyu si tu ubunifu wake katika kucheza lakini pia kwa urembo wake unaomfanya aonekane bado mdogo kwa umri, mvuto huu ulimfanya kupewa jina la 'J.Glow'

Mbali na kuwa na ratiba ngumu ya maigizo, kutengeneza muziki, kutumbuiza kwenye matamasha, na kwenda kwenye uzinduzi wa filamu mbalimbali, kufana mazoezi na kulea watoto wake wawili , Max na Emme, Lopez anasema hupata muda wa kupata usingizi wa kutosha.

Lopez anaamini kuwa urembo huanzia ndani. '' Samahani, huo ndio ukweli! Aliliambia jarida la People mwaka 2016, ''Ninafikiri kunywa maji mengi, kula vyakula halisi, matunda mengi na mboga za majani ninakuwa navyo wakati wote, vyote vina nafasi katika muonekano wa ngozi yangu.''

Kanye West

KW

Chanzo cha picha, PA Media

Ni miaka 17 tangu Kanye West atoe albamu yake ya kwanza , na bado anaonekana vilevile.

Mwaka 2004, West alitoa albamu yake ya kwanza, ''The College Dropout.'' Miaka 16 baadaye alitoa albamu yake ya hivi karibini , ''Jesus is King.

Hivi sasa ana miaka 44.

Beyonce

beyonce

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwaka 2000, Beyonce alikuwa na miaka 19 na leo ana miaka 39 na bado anaonekana vyema

Miaka 20 baada ya Destiny's Child, Beyonce ni mshindi wa tuzo za Grammy, mwanamuziki wa kujitegemea na mama wa watoto watatu- Blue, Sir na Rumi

Wakati akitarajia kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa ambapo atafikisha miaka 40, mwanamama huyo amekuwa akiweka picha zake mtandaoni karibu kila siku, katika kuthibitisha kuwa bado yu mrembo pamoja na umri wake kusonga.

Picha zake alizoziweka kwenye mtandao wake wa Instagram zilizopendwa na mamilioni ya wafuasi wake.

Mashabiki wake waliandika ujumbe kama Hello, 'kweli umri wako unarudi nyuma' 'binti' na mengine mengi almradi kushangazwa na muonekano wake.

Jay-Z

jAY Z

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwaka 2000 mwanamuziki huyu wa miondoko ya rap alikuwa na miaka 31 sasa ana miaka 51.

Shawn Corey Carter amezaliwa tarehe 4 mwezi Disemba mwaka 1969, ni mfanyabiashara wa Kimarekani mwenye mafanikio makubwa kabisa, kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 26 nchini Marekani na kupokea Tuzo kadhaa za Grammy kwa kazi zake za kimuziki. Hadi sasa waliomjua kuanzia zamani akiingia katika fani wanashangaa kwamba hajaweza kuzeeka au kubadilika muonekano .