Rais wa Marekani
Donald Trump amesema anaona kuwa ni "vigumu ngumu zaidi, kusema ukweli, kufanya
kazi na Ukraine" kuliko Urusi katika majaribio ya kuleta amani kati ya
mataifa hayo mawili.
Marekani "inafanya vizuri sana
na Urusi", na "inaweza kuwa rahisi kufanya kazi na" Moscow kuliko Kyiv, Trump aliwaambia
waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval siku ya Ijumaa.
Saa kadhaa mapema, Trump alikuwa
amesema "anazingatia sana" vikwazo vikubwa na ushuru kwa Urusi hadi
usitishaji vita na Ukraine ufikiwe.
Wakati huohuo, Marekani imesitisha
kwa muda upatikanaji wa picha za satelaiti kwa Ukraine , huduma inayotolewa na kampuni ya teknolojia ya
anga ya juu Maxar aliiambia BBC Verify, baada ya Trump kuwa tayari kusitisha msaada
wa kijeshi kwa nchi hiyo.
Hii inakuja wiki moja baada ya
mazungumzo ya ajabu ya White House , ambapo Trump alimsuta Rais wa Ukraine
Volodymyr Zelensky kwa "kutoheshimu" Marekani.
Malumbano hayo ya hadharani yalifuatiwa wiki hii na Trump
kusitisha misaada yote ya kijeshi ya Marekani na ushirikiano wa kijasusi na
Kyiv .Urusi kisha ilifanya shambulio kubwa la
kombora na ndege zisizo na rubani kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine
Alhamisi usiku.