Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja, shukran kwa kuwa nasi lakini kumbuka unaweza kufuata taarifa zetu zaidi kwenye Chaneli yetu ya WhatsApp:
Chanzo cha picha, Getty Images
Bofya
hapa ili kujiunga na chaneli yetu ya WhatsApp ikiwa unatumia simu
yako ya mkononi au Wavuti ya WhatsAp
Watu 12 wajeruhiwa kwa kupigwa risasi Toronto
Chanzo cha picha, Getty Images
Washukiwa watatu wanasakwa baada ya watu 12
kujeruhiwa katika tukio la ufyaliaji risasi katika baa moja mjini Toronto,
polisi nchini Canada wamesema.
Tukio hilo lilitokea saa nne na dakika 29 siku ya Ijumaa karibu na mtaa wa Scarborough,
mashariki mwa Toronto.
Mamlaka ilisema watu sita walipata majeraha ya
risasi na wengine kujeruhiwa na vifaa kama vile vioo vilivyovunjika. Hata hivyo
majeraha hayakuwa ya kuhatarisha aisha.
Polisi wa Toronto walisema watu hao watatu
waliingia kwenye baa hiyo na "kufyatua risasi kiholela". Walikuwa
wamebeba bunduki na bastola.
Mkuu wa polisi Paul MacIntyre anasema nia ya
kutekeleza tukio hilo “kwa sasa haijajulikana na tunaangalia uwezekano wa aina
yoyote ule.”
Polisi walisema wanatumia rasilimali zote
zilizopo kuwatafuta washukiwa hao.
Tazama: Helikopta ikimuokoa mkongwe mwenye umri wa miaka 71 aliyekwama mtoni
Maelezo ya video, gari likiondolewa kwa helikopta ndani ya maji
Muogeleaji wa uokoaji kutoka kikosi cha walinzi wa pwani ya Amerika alimvuta mwanamke mwenye umri wa miaka 71 kutoka kwa gari lililokuwa likielekeza kwenye Mto McKenzie huko Oregon. Mhudumu wa pili wa gari alifika ufukweni peke yake.
Helikopta ilitumiwa kumshusha mwogeleaji kuelekea kwenye gari na kumpandisha mwanamke huyo hadi mahali salama. "Uokoaji ulilitatizwa na maji mengi, giza, na eneo hatari la gari hilo, ambalo lilikuwa limekwama kwenye ukingo wa mwamba katikati ya Mto McKenzie," Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Lane ilisema katika chapisho kwenye Facebook.
Mwanamke huyo alipata majeraha yasiyo ya kutishia maisha na mkaaji wa pili hakujeruhiwa.
Mechi ya Simba na Yanga yaahirishwa
Chanzo cha picha, SIMBA
Bodi ya ligi nchini Tanzania imetangaza kuhairishwa kwa mchezo wa ligi kui bara kati ya Simba vs Yanga ulitorajiwa kupingwa leo jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bosi ya ligi mchezo huo umehairishwa ili kuweza kutoa muda wa uchunguzi juu ya tukio la vurugu usiku wa tarehe 7 Machi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ikumbukwe mapema leo klabu za Simba na Yanga zilitoa matamkoo juu mchezo huo ambapo Simbwa walishinikiza kutokupeleka timu baada ya kushindwa kufanya mazoezi ya mwisho kama kanuni zinavyotaka Kwa upande wa Yanga kwenye tamko walikubari kupeleka timi uwanja kama kanuni zinavyotaka.
Unayofaa kujua kuhusu wimbi la mashambulizi ya Urusi yaliyoiwaua watu 14 nchini Ukraine
Chanzo cha picha, AFP
Takriban watu 14 wameuawa na wengine kama 30 kujeruhiwa kufuatia wimbi la mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine usiku kucha.
Hiki ndicho unachopaswa kujua kuhusu mashambulizi hayo:
Kumekuwa na wimbi jingine la mashambulizi ya anga ya Urusi dhidi ya Ukraine usiku kucha, huku takriban watu 14 wakiuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kote nchini.
Watu 11 waliuawa katika shambulio katika mji wa Dobropillya katika mkoa wa Donetsk , na wengine watatu walikufa katika shambulio la ndege isiyo na rubani huko Kharkiv.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema mashambulizi hayo ya anga yanaonyesha kuwa malengo ya Urusi katika vita hivyo "hayajabadilika".
Zelensky aliongeza kuwa ni muhimu sana kuongeza vikwazo kwa Kremlin
Shambulio hilo la usiku lilikuja saa chache baada ya Marekani kuthibitisha kuwa ilizuia Ukraine kupata picha za kibiashara za satelaiti , baada ya kusitisha msaada wa kijeshi na kijasusi mapema wiki hii.
Ukraine imeendeleza mashambulizi yake dhidi ya Urusi, huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikisema kuwa ilizuia ndege zisizo na rubani 31 katika eneo lake jana usiku.
Mzozo wa DRC: Dola milioni 5 kutolewa kwa atakayewakamata viongozi wa waasi
Maelezo ya picha, Corneille Nangaa (kushoto) ni mmoja wa viongozi wanaosakwa na serikali ya Rais Tchisekedi (kulia)
Wizara ya Sheria ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahidi kutoa dola
milioni 5 kwa yeyote atakayesaidia kumkamata Corneille Nangaa, kiongozi wa
muungano wa mto Kongo, Bertrand Bisimwa na Sultani Makenga - viongozi wa kiongozi wa kisiasa na kijeshi wa vuguvugu la Machi 23 (M23).
Watu wengine wawili ni waandishi wa habari
wanaoishi uhamishoni, ambao pia wanalengwa , atakayewakamata akiahidiwa zawadi ya dola milioni 4.
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Ahadi ya dola milioni 5 pia imetolewa kwa atakayemkamata kiongozi wa jijeshi wa M23, Sultan Makenga
Viongozi hao wa waasi walishtakiwa bila ya kuwepo mahakamani na kuhukumiwa adhabu ya kifo mwezi Agosti mwaka jana na mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa kwa uhalifu wa kivita, na kusababisha uasi na uhaini.
Shambulio la Urusi lawaua watu 11 katika mji karibu na Donetsk, Ukraine yasema
Chanzo cha picha, Donetsk Emergency Service
Takriban watu 11 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika shambulizi la Urusi katika mji wa Dobropillya, ulioko mashariki mwa mkoa wa Donetsk nchini Ukraine, mamlaka ya Ukraine imesema.
Majengo manane ya makazi na jengo la utawala yaliharibiwa katika shambulio hilo la Ijumaa, huduma ya dharura ya kikanda ziliripoti. Mji huo uko kaskazini-magharibi mwa jiji la Donetsk linaloshikiliwa na Urusi.
Ripoti hiyo pia ilisema vikosi vya Urusi vilianzisha shambulio la pili dhidi ya wahudumu wa dharura wakati walipokuwa wakipambana na moto uliowaka kutokana na shambulizi hilo.
Hii inakuja baada ya mapigano makali katika maeneo ya karibu, huku waendesha mashtaka wa Ukraine wakiripoti kuwa watano waliuawa katika mashambulizi ya Urusi Alhamisi usiku.
Vikosi vya usalama vya Syria vinatuhumiwa kuwanyonga makumi ya Waalawi
Chanzo cha picha, Reuters
Vikosi vya usalama vya Syria vinadaiwa kuwaua makumi ya watu wa jamii ya
wachache ya Alawite katika mkoa wa pwani wa Latakia, kulingana na kundi la ufuatiliaji
wa vita.
Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake makuu
nchini Uingereza (SOHR) lilisema kuwa raia 162 wameuawa katika "unyongaji
uwanjani" katika eneo hilo - kitovu cha rais aliyeondolewa madarakani
Bashir al-Assad, ambaye pia ni mfuasi wa dhehebu la Waalawi.
Chanzo cha wizara ya mambo ya ndani kililiambia shirika rasmi la habari
la nchi hiyo Sana kwamba "ukiukwaji wa haki za watu binafsi"
ulifanyika kwenye pwani na kuahidi kukomesha.
Habari za BBC hazijaweza kuthibitisha madai kwamba mauaji hayo
yalifanywa na vikosi vya watawala wapya wa Syria.
Trump asema ‘vigumu zaidi’ kufanya kazi na Ukraine kuliko Urusi
Rais wa Marekani
Donald Trump amesema anaona kuwa ni "vigumu ngumu zaidi, kusema ukweli, kufanya
kazi na Ukraine" kuliko Urusi katika majaribio ya kuleta amani kati ya
mataifa hayo mawili.
Marekani "inafanya vizuri sana
na Urusi", na "inaweza kuwa rahisi kufanya kazi na" Moscow kuliko Kyiv, Trump aliwaambia
waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval siku ya Ijumaa.
Saa kadhaa mapema, Trump alikuwa
amesema "anazingatia sana" vikwazo vikubwa na ushuru kwa Urusi hadi
usitishaji vita na Ukraine ufikiwe.
Wakati huohuo, Marekani imesitisha
kwa muda upatikanaji wa picha za satelaiti kwa Ukraine , huduma inayotolewa na kampuni ya teknolojia ya
anga ya juu Maxar aliiambia BBC Verify, baada ya Trump kuwa tayari kusitisha msaada
wa kijeshi kwa nchi hiyo.
Hii inakuja wiki moja baada ya
mazungumzo ya ajabu ya White House , ambapo Trump alimsuta Rais wa Ukraine
Volodymyr Zelensky kwa "kutoheshimu" Marekani.
Malumbano hayo ya hadharani yalifuatiwa wiki hii na Trump
kusitisha misaada yote ya kijeshi ya Marekani na ushirikiano wa kijasusi na
Kyiv .Urusi kisha ilifanya shambulio kubwa la
kombora na ndege zisizo na rubani kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine
Alhamisi usiku.