Dhoruba
hatari ya majira ya baridi imeikumba Marekani, na kusababisha vifo vya watu
wasiopungua saba na kukata umeme kwa maelfu ya nyumba.
Shule na
barabara kote nchini zimefungwa na safari za ndege zimefutwa huku theluti mbaya ikienea kutoka Texas hadi New England,
kulingana na Mamlaka ya Kitaifa ya Hali ya Hewa (NWS).
Watu wawili
wamefariki kutokana na baridi kali huko Louisiana, na vifo vingine
vinavyohusishwa na dhoruba hiyo vimeripotiwa huko Texas, Tennessee na Kansas.
Kufikia
Jumapili alasiri, zaidi ya kaya 800,000 zimepoteza umeme, kulingana na
poweroutage.us. Wakati huo huo, zaidi ya safari za ndege 11,000 zimefutwa, imeripoti FlightAware.
Theluji
nzito inaweza kuathiri takribani Wamarekani milioni 180 - zaidi ya nusu ya idadi
ya watu.
"Theluji
na barafu zitayeyuka polepole sana na hazitatoweka hivi karibuni," Allison
Santorelli, mtaalamu wa hali ya hewa katika Mamlaka ya Kitaifa ya Hali ya Hewa, ameiambia
CBS News.
Idara ya
Afya ya Louisiana imethibitisha Jumapili kwamba wanaume wawili wamefariki
kutokana na baridi kali.
Meya wa
Austin, Texas, amesema mtu mmoja amefariki kutokana na baridi.
Maafisa huko
Kansas wamesema mwanamke, ambaye mwili wake ulipatikana Jumapili alasiri ukiwa
umefunikwa na theluji, "huenda alikufa kutokana na baridi."
Vifo vya
watu watatu vinavyohusiana na hali ya hewa pia vimeripotiwa huko Tennessee.
Meya wa Jiji
la New York Zohran Mamdani aliandika katika chapisho kwenye X kwamba watu
watano katika jiji hilo walifariki Jumamosi lakini akaongeza kuwa chanzo cha vifo vyao bado hakijabainika.
Marekani inakumbwa
na moja ya dhoruba kubwa zaidi za theluji katika zaidi muongo mmoja
Wataalamu wa
hali ya hewa wameonya kwamba moja ya hatari kubwa za dhoruba hiyo ni barafu,
ambayo ina uwezo wa kuharibu miti, kuangusha nyaya za umeme na kufanya barabara
kuwa hatari.
Huko
Virginia na Kentucky, kumetokea mamia ya ajali barabarani.
Wacanada pia
wamekumbwa na theluji kubwa na mamia ya safari za ndege zilizofutwa.
Maafisa
wanakadiria kwamba kutakuwa na theluji ya sentimita 15-30 (inchi 5-11) katika
jimbo la Ontario.