Kiongozi wa kijeshi aivunja serikali Burkina Faso

Mtawala wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoré amemfuta kazi waziri mkuu wake Apollinaire Joachim Kyelem de Tambela na kuivunja serikali nzima.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja, shukran kwa kuwa nasi lakini kumbuka unaweza kufuata taarifa zetu zaidi kwenye Chaneli yetu ya WhatsApp:

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Bofya hapa ili kujiunga na chaneli yetu ya WhatsApp ikiwa unatumia simu yako ya mkononi au Wavuti ya WhatsApp.

  2. Habari za hivi punde, Damascus inaangukia mikononi mwa waasi kitongoji baada ya kitongoji, afisa wa Marekani anaiambia CBS

    Afisa mmoja wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa ameliambia shiraka la habari washirika wa BBC wa Marekani, CBS News, kwamba Damascus inaonekana kuwa "kitongoji kinachoangukia mikononi mwawaasi", huku wapiganaji wanaoupinga utawala wa Assad wakiendelea kusonga mbele kwenye barabara kuu ya kuelekea mji mkuu wa Syria.

    Kama tulivyokwisha sema, video inaonekana kuonyesha sanamu ikibomolewa na waandamanaji katika kitongoji cha kusini mwa Damascus, wakati mapigano yakiendelea katika mji wa tatu kwa ukubwa nchini Syria wa Homs.

    Hatahivyo, serikali ya Syria inakanusha utekaji wa waasi katika mji mkuu na kusema kuwa Rais Bashar al-Assad hajaukimbia mji huo.

  3. Kiongozi wa kijeshi aivunja serikali Burkina Faso

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Kapteni Ibrahim Traoré alichukua mamlaka katika mapinduzi miaka miwili iliyopita

    Mtawala wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoré amemfuta kazi waziri mkuu wake Apollinaire Joachim Kyelem de Tambela na kuivunja serikali nzima.

    Kufutwa kazi kwa waziri mkuu na baraza lake la mawaziri kulitangazwa katika amri iliyotiwa saini na kiongozi huyo wa serikali siku ya Ijumaa.

    Amri hiyo haikubainisha kwanini waziri mkuu huyo alifutwa kazi, lakini ilisema mawaziri wa serikali iliyovunjwa wataendelea kuhudumu hadi baraza jipya la mawaziri litakapoteuliwa.

    Tambela, ambaye ni raia aliteuliwa kuwa waziri mkuu mnamo 2022, muda mfupi baada ya Ibrahim Traoré kunyakua mamlaka katika mapinduzi.

    Kufutwa kwake kunakuja wiki chache baada ya waziri mkuu mwingine wa kiraia, Choguel Maïga, kufutwa kazi na kiongozi wa mapinduzi Jenerali Assimi Goïta katika nchi jirani ya Mali.

    Bado haijafahamika kama Kapteni Traoré atamuiga mwenzake wa Mali kwa kumteua afisa wa kijeshi kama waziri mkuu, ili kudumisha utawala wa kijeshi.

    Burkina Faso, sawa na majirani zake wa Sahel, inaendelea kukabiliwa na vitisho vya usalama kutoka kwa makundi ya Jihadi.

    Licha ya ahadi za jeshi za kuimarisha usalama, hali bado ni mbaya kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi.

    Unaweza pia kusoma:

  4. Waasi wa Syria wakaribia jiji kuu Damascus, huku hofu ikitanda katika mji huo mkuu

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Vikosi vya upinzani nchini Syria vinasema viko "karibu kilomita 20 kutoka lango la kusini la Damascus."

    Luteni Kanali Hassan Abdul-Ghani kutoka idara ya operesheni ya kijeshi ya makundi ya upinzani alitangaza kupitia Telegram siku ya Jumamosi, akisema: "Vikosi sasa viko chini ya kilomita 20 kutoka lango la kusini la mji mkuu, Damascus."

    Abdul-Ghani ameyasema hayo kwenye jukwaa la Telegram: "Vikosi vyetu viliingia katika mji wa Al-Sanamayn, kaskazini mwa Daraa, na kutangaza kuwa umekombolewa, kwahivyo tuko chini ya kilomita 20 kutoka lango la kusini la mji mkuu, Damascus''

    Pia walisema kupitia Telegram, "Ukombozi wa Gavana wa Quneitra, kusini magharibi mwa Syria.

    Hali ya wasiwasi imetanda katika mji mkuu wa Syria, Damascus, kwa mujibu wa kile ambacho BBC imekifuatilia, katika wakati ambapo makundi ya upinzani yanatafuta kupata mafanikio makubwa, baada ya kusonga mbele. Tayari wameteka maeneo ya Aleppo, Idlib na Hama, na tangazo lao la hivi karibuni la udhibiti wao juu ya Daraa.

    Raia wa Syria wanakimbilia kuweka akiba ya mahitaji yao huku kukiwa na ongezeko la bei za bidhaa "muhimu".

    Unaweza pia kusoma:

  5. Denmark yapeleka kundi la pili la ndege za kivita za F-16 nchini Ukraine

    h

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Hayo yamesemwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

    "Kundi la kwanza la ndege zilizotolewa na Danmark tayari zinadungua makombora ya Urusi na kuokoa watu wetu na miundombinu yetu. Ngao yetu ya anga sasa imeimarishwa zaidi," Zelensky alisema katika ujumbe kwenye kituo chake cha Telegram.

    Kundi la kwanza la ndege za kivita aina ya F-16 kutoka Denmark liliwasili nchini Ukraine mapema mwezi Agosti. Uholanzi pia iliripoti mnamo Oktoba kwamba Jeshi la Ukraine lilipokea ndege za aina hii.

    Gazeti la Times liliandika kwamba, zaidi ya hayo mwaka ujao Ukraine inapaswa kupokea ndege 20 aina ya F-16, ikiwa ni pamoja na kutoka Ubelgiji na Norway.

    Ndege hizi zina uwezo wa kurusha makombora ya cruise, ambayo Ukraine ina matumaini makubwa.

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Ndege za kivita za F-16 zilianza kutumika mwaka wa 1978. Ndege hizi za kivita ziliundwa ili kurusha makombora na kushambulia ndege za adui.

    Ndege hizi za kivita husaidia wanajeshi kusonga mbele ardhini kwa kushambulia eneo la mpaka wa adui.

    Hata hivyo, Phillips O'Brien anaripoti kwamba Ukraine itatumia ndege hizi za kivita kwa ajili ya ulinzi wake. Yeye ni profesa katika Idara ya Mafunzo ya Kimkakati katika Chuo Kikuu cha St. Andrews, Scotland.

    Soma zaidi taarifa hizi kuhusu ndege za F-16:

  6. Urutubishaji wa uranium wa Iran ni 'wa kutisha' - shirika linalodhibiti nyuklia

    g

    Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

    Maelezo ya picha, Rafael Grossi alisema "sio siri" baadhi ya wanasiasa nchini Iran walikuwa wanataka kuundwa kwa silaha za nyuklia.

    Mkuu wa shirika la uangalizi wa nyuklia la Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kuwa uamuzi wa Iran kuanza kuzalisha uranium iliyorutubishwa kwa kiwango kikubwa ni "wa kutisha sana".

    Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la udhibiti wa nishati ya atomiki (IAEA), Rafael Grossi alisema Iran inaongeza hifadhi yake ya uranium iliyorutubishwa hadi 60%, chini tu ya kiwango cha usafi kinachohitajika kwa silaha ya nyuklia.

    Hili litaonekana kwa wengi katika eneo hilo kama jibu la Tehran kwa vikwazo vyake vya kijeshi na kidiplomasia huko Syria, Lebanon na Gaza katika miezi ya hivi karibuni.

    Bwana Grossi alisema "sio siri" baadhi ya wanasiasa nchini Iran walikuwa wakitoa wito wa kubuniwa kwa silaha za nyuklia, lakini baada ya kufanya mazungumzo mjini Tehran wiki za hivi karibuni, alisema "haionekani kuwa njia ya kuchagua" uongozi wa sasa.

    Bw Grossi alikuwa akizungumza pembezoni mwa mkutano wa Manama Dialogue nchini Bahrain unaoendeshwa na taasisi yenye makao yake makuu jijini London, taasisi ya kimataifa ya mafunzo ya kimkakati.

    Aliionya Israel dhidi ya kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran, akisema matokeo yatakuwa "mabaya sana kwa kweli" katika suala la kulipiza kisasi kwa Tehran na uwezekano wa kuenea kwa mionzi.

  7. Kizaazaa huku wabunge wa chama tawala cha Korea Kusini wakiondoka bungeni kabla ya kura ya kumuondoa madarakani rais

    Reuters

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wabunge wa chama tawala cha Korea Kusini cha People Power Party (PPP) 107 kati ya 108 wa chama tawala, 107 wameondoka bungeni kabla ya kura ya kumuondoa madarakani tais wa nchi hiyo. Wabunge sasa waliztarajiwa kupigia kura hoja ya kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol anayezongwa na kashfa.

    Huenda chama hicho kilitumia mkakati wa kususia upigaji kura ili kuzuia watu kuasi, kwani kura ya kumuondoa ni kupitia kura zisizojulikana.

    Ahn Cheol-soo, profesa aliyegeuka kuwa mwanasiasa ambaye aliwania urais mwaka wa 2012, 2017 na 2022, ndiye mwanachama pekee wa PPP ambaye amesalia katika kiti chake.

    Ahn amekuwa akisema mara kwa mara kuwa atapiga kura ya kufunguliwa mashtaka ikiwa rais hatajiuzulu kwa hiari kabla ya upigaji kura.

    Wabunge wa wengi wa vyama vya upinzani wamekusanyika bungeni . Walikimbia mara tu wabunge walipoanza kuondoka, wakijaribu kuwazuia kuondoka.

    Walikuwa wakiimba "wasaliti" na "rudi tena kupiga kura".

    Kuna hasira kubwa. Ni mwanachama mmoja tu au wawili wa chama tawala ambao bado wamesalia ndani ya ukumbi, ikimaanisha kuwa kura hii sasa haitapigwa, amesema mwandishi wa BBC mjini Seol.

    Nje ya bunge, kulikuwa na umati wa watu huku Wakorea wengi zaidi wakikusanyika kwenye barabara ya bunge la ttaifa. Polisi wameimarisha hali ya usalama.

    Maandamano hayo yapo karibu na kituo cha treni ya chini ya ardhi, na vizuizi vikubwa vinaweza kuonekana kwenye kituo cha usafiri mapema huku watu wakimiminika.

    Mamlaka iliamua kufunga kituo hicho, na polisi wamepanga mistari kwenye maeneo mbalimbali kuongoza umati wa watu wanaoandamana.

    Soma zaidi hapa:

  8. Waghana wasubiri kumpata Rais mpya huku siku siku ya uchaguzi ikiwadia

    g

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Matokeo yamepangwa kutangazwa kufikia Jumanne

    Siku ya uchaguzi imefika nchini Ghana, huku mzozo wa madeni na gharama kubwa ya maisha vikiwa zaidi katika fikra za wapiga kura wengi.

    Taifa hilo la Afrika Magharibi lina uhakika wa kuwa na rais mpya huku Nana Akufo-Addo akiondoka madarakani baada ya kufikisha kikomo rasmi cha mihula miwili madarakani.

    Lakini nafasi yake inaweza kubadilishwa na sura inayofahamika, iwapo Rais wa zamani John Mahama atafanikiwa katika jaribio lake la kurejea mamlakani kupitia chama cha NDC.

    Mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia, ambaye atakuwa kiongozi wa kwanza wa Kiislamu nchini humo iwapo atashinda kwa tiketi ya chama tawala cha NPP.

    Soma zaidi:

  9. Tazama: Wakati sanamu ya rais wa zamani wa Syria ilipoporomoshwa katika mji wa Hama

    Maelezo ya video, Sanamu ya rais wa zamani ikiangushwa Hama

    Sanamu ya marehemu rais wa Syria, Hafez al-Assad, babake Rais Bashar al-Assad, imebomolewa katika mji wa Hama.

    Waasi wa Syria wanasema wamechukua udhibiti kamili wa mji mkuu wa pili wa nchi hiyo, baada ya jeshi kuondoka. Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu Hayat Tahrir al-Sham (HTS), Abu Mohammed al-Jawlani, alitangaza "ushindi" huko Hama na kuapa "hakutakuwa na kisasi".

    Hapo awali, wapiganaji wa HTS na washirika wao waliliteka gereza kuu la Hama na kuwaachilia wafungwa wakati kukiwa na vita vikali,

    Jeshi la Syria lilisema kuwa lilikuwa limetuma wanajeshi nje ya mji huo. Hama ni makazi ya watu milioni moja na iko kilomita 110 (maili 70) kusini mwa jiji la Aleppo, ambalo waasi waliliteka wiki iliyopita baada ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza kutoka ngome yao kaskazini-magharibi. Huko Aleppo, sanamu ya marehemu kaka wa Rais Bashar al-Assad, Bassel, pia iliharibiwa.

  10. Waasi wateka sehemu kubwa ya eneo kuu la kusini mwa Syria - ripoti

    f

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Deraa iko karibu na vivuko kuu vya mpaka na Jordan na ndipo uasi wa Syria ulianza Machi 2011

    Vikosi vya waasi kusini mwa Syria vimeripotiwa kuteka sehemu kubwa ya eneo la Deraa, mahali yalipotokea maasi ya mwaka 2011 dhidi ya Rais Bashar al-Assad.

    Wachunguzi wa vita wenye makao yake nchini Uingereza wanaripoti kwamba "vikundi vya ndani" viliweza kuchukua udhibiti wa maeneo mengi ya kijeshi huko kufuatia "mapigano makali" na vikosi vya serikali.

    Kulingana na shirika la habari la Reuters, vyanzo vya waasi vinasema kuwa wamefikia makubaliano ya jeshi kuondoka na maafisa wa kijeshi wapewe njia salama kuelekea mji mkuu, Damascus - takriban kilomita 100 (maili 62) kutoka.

    BBC imeshindwa kuthibitisha kwa uhuru ripoti hizi, ambazo zinakuja huku waasi wanaoongozwa na Waislamu kaskazini mwa Syria wakidai kufika viunga vya mji wa Homs.

    Unaweza pia kusoma:

  11. Hujambo na karibu kwa matangazo haya mubashara ya Jumamosi hii ya tarehe 07.12.2024