F-16 : Kwa nini ndege hii ya kivita bado inahitajika sana?

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Na Stephen Dowling

BBC Future

Ndege ya kivita ya F-16 iliruka kwa mara ya kwanza mwaka wa 1974, lakini bado ni ndege muhimu sasa kama ilivyokuwa wakati huo.

Ikiwa si kwa majaribio ya haraka ya miaka 50 iliyopita, mpango mzima wa F-16 haungeweza kuvuka hadi safari yake ya kwanza ya kutisha.

Wakati rubani Phil Oestricher alipopanda kwenye chumba cha marubani cha mfano wa ndege hiyo ya General Dynamics YF-16 katika Kambi ya Jeshi la Anga la Edwards huko California tarehe 20 Januari 1974, dhamira yake ilikuwa ya moja kwa moja - jaribio la teksi ya mwendo kasi ambapo ndege ingesafiri ardhini chini ya nguvu ya injini yake yenyewe.

YF-16 ilikuwa imezinduliwa kwa umma zaidi ya mwezi mmoja tu uliopita. Safari ya kwanza ya ndege haikupangwa kufanyika hadi mapema Februari.

Lakini ndege hiyo yenye uwezo mkubwa wa siku za baadaye ilikuwa na mawazo mengine.

Oestricher alipoinua pua ya ndege kidogo, YF-16 ilianza kuyumba-yumba kwa kasi sana hivi kwamba bawa la kushoto la ndege hiyo na mkia wa kulia uligonga lami. "Kadiri Oestricher alivyopigana kwa bidii ili kudumisha udhibiti hali ilizidi kuwa mbaya kama YF-16 ilipoanza kugeukia upande wa kushoto," liliandika gazeti la Seattle Post Intelligencer , likiripoti kuhusu safari ya kwanza iliyokaribia kuwa janga. Oestricher aligundua kwamba angelazimika kuondoka kwenye jaribio lililopangwa na kuipeleka juu ndege hiyo - na haraka sana - kabla haijaanguka.

Baada ya muda fulani wa kusimama - wakati mmoja ndege ilishuka chini kwenye njia ya kurukia ndege - Oestricher aliweza kuchukua kasi ya kutosha na kuingia angani na kukamilisha safari isiyotarajiwa ya dakika sita kabla ya kutua tena kambini.

Kwa sababu ya ustadi wake wa kurusha ndege, Oestricher alikuwa amezuia maafa - na kusaidia kuleta uhai wa ndege ambayo imekuwa mojawapo ya mafanikio zaidi katika kumbukumbu . Miaka 50 baadaye, zaidi ya ndege 4,600 za F-16 zimeundwa kutoka kiwanda, na uzalishaji hauonyeshi dalili ya kukomeshwa.

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ikiwa Oerlicher hangefaulu kuokoa YF-16 kutokana na ajali kwenye jaribio lake la kwanza la kasi kama teksi , kungekuwa na pengo kubwa la umbo la F-16 katika vikosi vingi vya anga duniani. Muundo wa ndege pia umekuwa na athari ya kudumu kwa usafiri wa anga leo pia, ikitoa matumizi ya kwanza ya teknolojia ambayo sasa ni ya kawaida katika mashirika ya ndege ya abiria, kwa mfano.

Wakati wowote wa mchana - au usiku - kuna uwezekano mkubwa kwamba ndege ya F-16 ipo angani, mahali popote ulimwenguni. Tangu kuanza kutumika na Jeshi la Wanahewa la Marekani (USAF) mwaka 1978, F-16 imekuwa ikitumiwa na vikosi vingine 25 vya anga, kutoka Norway hadi Chile, Morocco hadi Singapore. Mnamo 2023, miaka 45 baada ya kuanza huduma, zaidi ya 800 zilibaki zikitumiwa na USAF .

F-16 ikiwa imeundwa kama ndege ndogo ya kupigana angani ,nyepesi na mahiri zaidi, imechukua majukumu zaidi na zaidi, kutoka kwa mashambulizi ya ardhini hadi ya doria za baharini ,hadi upelelezi wa picha hadi kuwinda virusha makombora kutoka ardhini hadi angani. Tangu 2015, imekuwa ndege nyingi zaidi za kijeshi zinazotumia mabawa yaliyotundikwa; zaidi ya 2,000 zinafikiriwa kuwa bado zinatumika duniani kote leo.

Ombi la Ukraine kwa nchi za Magharibi kwa silaha za kisasa kupinga uvamizi wa Urusi mwaka 2022 limejumuisha wito wa F-16 kwa kikosi chake cha anga. Marubani wa Ukraine kwa sasa wanafanya mazoezi kutumia F-16s nchini Denmark, na usafirishaji unatarajiwa kuanza majira ya kiangazi. Mapema Januari, Slovakia ilikuwa nchi ya hivi punde kuwasilisha ndege zake za kwanza za F-16 , miaka 50 karibu siku tangu ndege hiyo ilipoanza kutumika angani.

Kuweka ndege ya kivita ya mstari wa mbele katika huduma - kando na uzalishaji - kwa miongo mitano sio kazi rahisi. Sababu kwa nini vikosi vya anga bado vinataka F-16 ni kutokana na baadhi ya vipengele vya kiubunifu vya kweli vya muundo wake, na baadhi ya mafunzo magumu yaliyopatikana kutokana na mapigano ya angani katika Vita vya Vietnam.

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wa miaka ya 1960, Marekani ilikuwa imekubali teknolojia mpya ya kombora la angani hadi angani kama silaha bora ya kudungua ndege za adui. Vita vya Vietnam vilipoanza mwaka wa 1965, baadhi ya ndege zake za kivita za mstari wa mbele, kama vile F-4 Phantom II , hazikuwa na bunduki; Wapangaji wa kijeshi wa Marekani waliamini kuwa makombora ya ndege hiyo yalitosha.

Ndege za kivita za Marekani zenye kombora, hata hivyo, zilikabiliana dhidi ya ndege ndogo na nyepesi za MiG ziliotengenezwa na Soviet wakati vita vya Vietnam vikiendelea. Baadhi ya MiG za Vietnam Kaskazini zilifanana kwa karibu na za Kisovieti ambazo zilipigana kwenye peninsula ya Korea mwanzoni mwa miaka ya 1950, na sasa zilichukuliwa kuwa karibu kupitwa na wakati katika nchi za Magharibi. Katika mapigano ya karibu, hata hivyo, ambapo ndege za Marekani hazikuweza kubeba makombora yao, ziliweza kuwa wapinzani wa kutisha.

Kati ya 1965 na 1968, ndege za Amerika bado zilizipiga nyingi za Kivietinamu Kaskazini kuliko walivyokuwa wakipoteza, lakini pengo lilipungua sana . Ndege kubwa za Marekani zenye injini-mbili zilikuwa rahisi kuziona kwa mbali; MiG ndogo, zenye injini moja hazikuwa rahisi kuziona angani.

Suluhisho mojawapo lilikuwa kuanzisha shule za mafunzo kama vile " Top Gun " ya Jeshi la Wanamaji la Marekani, ambayo iliwafundisha marubani wa Marekani ustadi uliopotea wa kupigana kwa kufukuzana hewani; hii ilianza kutumika kabla ya mwisho wa Vita vya Vietnam, na kuboresha kwa kiasi kikubwa uwiano wa kuua-kwa-hasara kwa Marekani. Mapigano ya angani yalikuwa yameanza katika Vita vya Kwanza vya Dunia, katika ndege ndogo zenye kasi zaidi kuliko gari la familia. Mapambano sawa katika jeti zinazoweza kuruka kwa maili mia kadhaa kwa saa ni hali tofauti kabisa - kasi ya juu inamaanisha unakabiliwa na nguvu za juu za mvuto, au G-force.

Lakini nyingine ilikuwa mpango kabambe zaidi ulioundwa ili kukabiliana na uboreshaji wa ndege za Soviet. Wakuu wa ulinzi wa Marekani tayari walikuwa wameshtushwa, mwishoni mwa miaka ya 1960, kwa kuibuka kwa ndege ya Soviet MiG-25, ndege kubwa ya kivita ambayo inaweza kuruka mara tatu ya kasi ya sauti.

Wito wa Pentagon wa kutaka majibu yenye nguvu ili kukabiliana na MiG-25 ulipelekea McDonnell-Douglas F-15 Eagle , kifaa cha kisasa , kikubwa na cha haraka kilichoundwa kuangusha ndege ya adui katika mwinuko wa juu kwa makombora ya kuongozwa na rada. Lakini Umoja wa Kisovieti na washirika wake wa Mkataba wa Warsaw kama vile Poland na Ujerumani Mashariki waliwasilisha maelfu ya ndege zaidi za kivita ambazo zingeruka na kupigana kwa kiwango cha chini.

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Kilichohitajika pia ni ndege ndogo, nyepesi ambayo inaweza kuangusha ndege za adui kwa makombora ya kutafuta joto na bunduki - somo la moja kwa moja kutoka vita vya Vietnam.

USAF ingehitaji mamia ya ndege kama hizo , na kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba nchi za Nato na washirika wengine wa Amerika kote ulimwenguni wangefuata mkondo huo. Miundo mitano iliishia katika meza ya mradi huu wa faida kubwa, na mbili zikiibuka haraka kama za kipekee - YF-16 kutoka General Dynamics (sasa ni sehemu ya Lockheed-Martin) na YF -17 kutoka kwa mpinzani Northrop .

YF-16 iliundwa ili kupambana angani kwanza kabisa, na hiyo iliathiri moja kwa moja vipengele vya muundo wake, ikiwa ni pamoja na dari yake ya chumba cha marubani. Rubani angekaa kwenye chumba cha marubani kilichoinuliwa chenye mwavuli mkubwa ambao unatoa mtazamo usio na kifani -sawa na ndege za kivita za mapema ambazo zilibadilishwa na ndege zenye silaha za kombora. "Angalau sehemu ya 'mafia wapiganaji' waliokuwa wakiisukuma walikuwa wakitazama nyuma -Korea na F-86 Saber ," anasema Tim Robinson, mtaalamu wa masuala ya anga katika Shirika la Anga la Royal nchini Uingereza. "Walikuwa wakiangalia kitu ambacho kilikuwa rahisi kubadilika na kilikuwa na maono mazuri sana kwa rubani aliye na mwavuli wa mapovu."

Wazo moja ambalo lilipendekezwa, Robinson anaendelea, lilikuwa ni kuondoa kabisa rada. "Wazo lilikuwa kuwa na makombora mawili na bunduki. Na wangelazimika kufyatua vitu hivi. Walikuwa wakiangalia idadi ya ndege za Soviet na walikuwa wakifikiria: 'Gosh, tutahitaji nyingi hizi, lazima tujenge ndege nyingi."

Ndege mpya haikuhitaji masafa marefu ya F-15, kwa hivyo inaweza kuwa ndogo zaidi na nyepesi na ingehitaji injini moja badala ya mbili za F-15. Mchanganyiko huo wa uzani wa chini na injini yenye nguvu hutengeneza uwiano wa juu wa " uzito', ambayo sio tu kuwezesha kasi ya juu lakini pia uwezo wa kugeuka kwa kasi -tosha kwa ajili ya mapambano ya angani.

F-16 iliundwa kustahimili hadi 9G katika vita vya hewani(ambayo ina maana kwamba chochote ambacho kingekuwa na uzito wa kilo 1 kwenye ardhi kinaweza kuwa na kilo 9 ). Kuruka kwa kiwango cha juu cha -G huleta mkazo mkubwa kwa fremu ya anga na rubani . F-4 kwa kulinganisha, inaweza kuvuta 7G, lakini si kwa muda mrefu kwani fremu yake ya hewa nzito iliondoa kasi na urefu kwa haraka zaidi.

Ili kumsaidia rubani kuendelea kuwa na fahamu akiwa ndani , kiti cha chumba cha marubani kwenye F16 huegemezwa, ambayo husaidia kupunguza baadhi ya athari kwa rubani. Jeff Bolton ni mwandishi wa habari wa usafiri wa anga na mtangazaji ambaye amesafiri mara mbili katika toleo la viti viwili la F-16, linalotumika kwa mafunzo ya marubani na misheni maalum. "Niko karibu 6ft 4in (1.9m), kwa hivyo inanibana, inanibana, lakini bado ningeweza kupunguza kiti changu , na ningeweza kuingiza mkono wangu kati ya kofia yangu na dari. Na kuna, Nadhani, utambuzi kutoka kwa mwili wako kwamba 'umevaa' ndege."

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Muundo wa chumba cha marubani wa F-16 ulienda mbali zaidi kuliko kiti kilichoegemezwa na mwonekano mzuri. Wabunifu wa ndege hiyo waliondoa moja ya sifa kuu za ndege za kivita tangu Vita vya Kwanza vya Dunia - fimbo ya kudhibiti kati ya miguu ya rubani. Badala yake, F-16 ilikuwa na kidhibiti cha mtindo wa kijiti upande wa kulia wa chumba cha marubani, kama vile ungetumia kwenye kiigaji cha mchezo wa kompyuta.

Awali F-16 iliundwa ili kupiga jeki F-15 katika miinuko ya chini, lakini hivi karibuni iligundulika kuwa - kama vile Vita vya Pili vya Dunia Supermarine Spitfire - fremu ya anga ya F-16 iliiruhusu kubeba mizigo mizito zaidi, mafuta zaidi na rada kubwa zaidi. "F-16 ni karibu kisu bora kabisa cha Jeshi la Uswizi," Bolton anasema.

F-16, katika Karne ya 21, imekuwa muhimu vile vile kama ndege ya mashambulizi ya ardhini - si kitu ambacho wabunifu wake walikuwa nacho kwenye mawazo mapema miaka ya 1970. Kubadilika huko kuliiruhusu kutekeleza majukumu zaidi na zaidi, ambayo ilifanya izidi kuvutia kwa vikosi vya anga. "Pale ambapo kuna mzozo, pengine kuna F-16 inayohusika mahali fulani," anasema Robinson.

Jina la utani la asili la F-16 lilikuwa "Fighting Falcon", lakini jina hilo halikudumu , anasema Robinson. "Hakuna mtu anayewahi kulitumia. Wanaiita Viper, sababu ikiwa ilitoka mwishoni mwa miaka ya 70 wakati sawa na [mfululizo wa TV] Battlestar Galactica. Inaonekana kama Nyoka wa Kikoloni ," Robinson anasema, akirejelea anga za juu zilizoangaziwa katika kipindi. "Bado inaonekana kama ni yake katika siku zijazo."

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

F-16 iko mbioni kubadilishwa Marekani na baadhi ya vikosi vya anga vya Nato na ndege nyingine ya vita iliyotengenezwa na Lockheed, F-35. Kila F-35 inagharimu zaidi ya $100m (£81m) na imeundwa kuharibu ndege za adui kwa makombora ya masafa marefu, muda mrefu kabla ya F-35 kunyakuliwa kwenye rada zao. F-16 bila programu jalizi inaweza tu kugharimu theluthi moja ya bei hiyo.

Itakuwa 2056 kabla ya F-35 kuadhimisha miaka 50 tangu kuruka kwa mara ya kwanza. Kuna uwezekano mkubwa kwamba hata wakati huo, mahali fulani ulimwenguni F-16 bado zitakuwa zikiruka.

Unaweza Pia Kusoma

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah