Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei ameuawa, televisheni ya serikali imesema

Awali, Trump alithibitisha kuwa Khamenei amefariki kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa Truth Social.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid, Ambia Hirsi & Asha Juma

  1. Katika picha: Hisia mseto nchini Iran huku mashambulizi yakiendelea

    Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka ndani ya Iran tunapokaribia saa 24 tangu Israel na Marekani kuishambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati.

  2. Rais na wengine wawili watasimamia kipindi cha mpito - Iran yatangaza

    Iran imemtangaza kwamba rais wake, mkuu wa mahakama, na mmoja wa wanasheria wa Baraza la Walinzi - chombo chenye nguvu - watasimamia kipindi cha mpito kufuatia kifo cha Ayatollah Ali Khamenei.

    Jopo la Wataalamu wa Uongozi - baraza la maulama - sasa litageukia linatarajiwa kumteua mrithi wa Khamenei, jambo ambalo katiba inasema lazima lifanyike haraka iwezekanavyo.

    Kukufanyika kwa haraka kwa shughuli hiyokw wakati Iran inashambuliwa na Marekani na Israel kunaweza kuwa vigumu kutokana na sababu za kiusalama.

    Khamenei mwenyewe aliteuliwa siku hiyo hiyo Ruhollah Ayatollah Khomeini alipokufa.

  3. Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi...

    Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimethibitisha kwamba Kiongozi Mkuu Ali Khamenei ameuawa, katika mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran kutoka ambayo yalianza Jumamosi asubuhi (saa za ndani).

    Haya hapa yaliyojiri kwa mukhtasari:

    • Taarifa ya Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran, iliyosomwa vyombo kadhaa vya habari vya serikali, imethibitisha kuwa Ayatollah Khamenei aliuawa ofisini kwake mapema Jumamosi asubuhi.
    • Mtangazaji mmoja, alisema nchi itaanza siku 40 za maombolezo huku akitokwa na machozi, .
    • Zaidi ya watu 200 wameuawa wakati wa mashambulizi hayo, kulingana na shirika la Red Crescent, huku CBS News, mshirika wa habari wa BBC ikiripoti kuwa maafisa 40 wa Iran wameuawa.
    • Kujibu mashamblizi hayo, Iran ilifanya msururu wa mashambulizi Mashariki ya Kati, hasa dhidi ya mataifa washirika wa Marekani na ambapo Marekani ina kambi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na Dubai, Doha, Bahrain, na Kuwait.
    • Uingereza inashiriki katika "operesheni zilizoratibiwa za ulinzi wa kikanda" kulinda raia wa Uingereza na washirika wa kikanda, Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer amesema.
    • Rais Donald Trump hapo awali alisema Khamenei alikuwa "mmoja wa watu waovu zaidi katika historia" na kwamba kifo chake kilikuwa "fursa kubwa zaidi kwa Wairan kurujirudishia nchi yao". Alisema Marekani itaendelea kuishambulia Iran kwa mabomu - huku milipuko ikiendelea kusikika katika mji mkuu wake Tehran.
    • Marekani haiwezi kutangaza vita bila idhini ya bunge - na operesheni hii imegawanya wabunge, kwa kiasi kikubwa kulingana na vyama.
    • Umoja wa Mataifa pia umesema operesheni hiyo ya kijeshi inadhoofisha amani katika eneo hilo.
  4. Habari za hivi punde, Iran yaonya kuhusu 'mashambulizi mabaya'

    Tumepokea taarifa hivi punde kutoka kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ikionya kwamba watashambulia kambi za Marekani na Israel.

    "Operesheni mbaya zaidi ya katika historia ya vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaanza kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na vituo vya kigaidi vya Marekani muda mfupi ujao," inasema.

  5. Habari za hivi punde, Televisheni ya taifa ya Iran: Khamenei aliuawa ofisini kwake

    Tukiangazia tena maelezo zaidi taarifa ya Baraza Kuu la Usalama la Iran, iliyosomwa kwenye vituo vya Televisheni vya serikali hapo awali.

    Baraza hilo limesema kuwa Ayatollah Khamenei aliuawa mapema Jumamosi asubuhi katika ofisi yake "alipokuwa akitekeleza majukumu yake".

    Kwa kutumia picha za satelaiti, BBC Verify hapo awali ilithibitisha uharibifu mkubwa wa sehemu za Jumba la Uongozi, ambalo ni ofisi ya Khamenei mjini Tehran.

    Shirika la Habari la Tasnim linalohusiana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema kwamba kifo cha Khamenei ofisini mwake ni dhibitisho kwamba ripoti kwamba alikuwa akijificha zilikuwa "vita vya kisaikolojia vya adui".

    Soma pia:

  6. Mrithi wa Khamenei hakutajwa kwenye tangazo la kifo chake

    Taarifa kutoka Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, vyombo kadhaa vya habari vya serikali nchini Iran vimethibitisha kifo cha Ayatollah Khamenei.

    Rais wa Marekani Donald Trump saa chache zilizopita alisema Kiongozi Mkuu huyo aliuawa wakati wa shambulio la pamoja na Israel katika maeneo kadhaa kote Iran.

    Katika taarifa hiyo, haikutajwa ni jinsi gani Khamenei mwenye umri wa miaka 86 alivyofariki, au ni nani anayeweza kuchukua nafasi ya kiongozi.

    Jamaa wa Khamenei pia wameuawa katika mashambulizi hayo

    Hapo awali, vyombo vya habari vya serikali vilisema kwamba binti wa Khamenei, mkwewe na mjukuu wake pia waliuawa katika mashambulizi hayo.

    Kulingana na Shirika la Habari la Fars, ambalo lina uhusiano na Kikosi cha Revolutionary Guard, kuna ripoti kwamba mmoja wa mabinti wa Khamenei ameuawa pia.

    Pia unaweza kusoma:

  7. Habari za hivi punde, Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei ameuawa, televisheni ya serikali imesema

    Televisheni ya taifa ya Iran imethibitisha kuwa Ayatollah Ali Khamenei ameuawa.

    Siku arobaini za maombolezo zatangazwa nchini Iran

    Katika hotuba ya machozi, mtangazaji wa televisheni ya serikali ametangaza kifo cha Khamenei na kusema nchi itaingia katika siku 40 za maombolezo.

    Jamaa za Khamenei pia waliuawa katika mashambullizi hayo.

    Kulingana na Shirika la Habari la Fars ambalo lina mafungamano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kuna ripoti kwamba binti mmoja wa Khamenei ameuawa pia.

    Soma zaidi:

  8. CBS yasema maafisa 40 wa Iran wauawa katika shambulizi

    Chanzo cha habari cha kijasusi na chanzo cha kijeshi kimeambia mshirika wa vyombo vya habari wa BBC, CBS News, kwamba takriban maafisa 40 wa Iran wameuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

    Haijulikani wazi kama maafisa hao walikuwa katika eneo moja au tofauti.

    Walidai kwamba kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, alikuwa miongoni mwa waliofariki, pamoja na kamanda wa Kikosi cha Revolutionary na waziri wa ulinzi.

    Iran bado haijathibitisha ripoti zilizoenea kuhusu kifo cha Khamenei.

  9. UAE yalaani shambulio la Iran

    Umoja wa Falme za Kiarabu umelaani mashambulizi ya Iran dhidi ya eneo lake, ukiita ni "ukiukaji wa uhuru wa kitaifa na sheria za kimataifa".

    Katika chapisho kwenye mtandao wa X, UAE inaita hatua ya kulipiza kisasi ya Iran kuwa kuongeza hatari na "kitendo cha uwoga" kinachotishia usalama wa raia na kudhoofisha utulivu.

    Wizara yake ya ulinzi inasema iko " katika tahadhari ya juu" na tayari kukabiliana na vitisho vyovyote.

    Inaongeza kuwa vikosi vyake vya ulinzi vimezuia makombora 137 ya balestiki na ndege zisizo na rubani 209 zilizorushwa kuelekea nchini.

    Kumi na nne kati ya ndege zisizo na rubani zilizoanguka ndani ya maeneo na maji ya nchi hiyo zilisababisha "uharibifu fulani", inasema.

    Pia unaweza kusoma:

  10. Ziara ya Rubio kwenda Israel yafutwa

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio hatasafiri tena kwenda Israel siku ya Jumatatu "kutokana na hali ilivyo kwa sasa", ofisi yake imesema.

    Wizara ya mambo ya nje ilisema jana Rubio alikuwa amepangiwa kwenda Israel kujadili mada mbalimbali, ikiwemo Iran.

    "Kutokana na hali ilivyo kwa sasa, Waziri Rubio hatasafiri tena kwenda Israeli mnamo Machi 2," msemaji anasema.

  11. Habari za hivi punde, Trump asema Kiongozi Mkuu wa Iran amekufa

    Khamenei, mmoja wa watu waovu zaidi katika Historia, amekufa," Rais wa Marekani Donald Trump ameandika kwenye Truth Social.

    'Haki si kwa watu wa Iran pekee, bali kwa Wamarekani wote Bora' - Trump

    Katika akaunti yake kwenye mtandao wa Truth Social, Rais wa Marekani Donald Trump ameandika.

    "Hii si haki kwa watu wa Iran pekee, bali kwa Wamarekani wote Bora," amesema.

    "Hakufanikiwa kukwepa Majasusi wetu na Mifumo yetu ya Ufuatiliaji ya Kisasa, na, kwa ushirikiano wa karibu na Israeli, hakukuwa ambalo yeye, au viongozi wengine awaliouawa pamoja naye, wangeweza kufanya."

    "Hii ndiyo fursa kubwa zaidi kwa watu wa Iran kuirudisha Nchi yao," ameongeza.

    Awali, Rais Donald Trump wa Marekani alizungumza na NBC News kwa njia ya simu - na wamemuuliza kuhusu ripoti kwamba kiongozi mkuu wa Iran ameuawa na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel.

    "Nimezungumza na watu wengi, tunahisi huu ni ukweli," Inaripotiwa Trump amemwambia mtangazaji wa Marekani.

    "Idadi kubwa ya viongozi wao pia wameuawa," aliongeza, akirudia kile alichoambia ABC News.

    Pia aliambia NBC News kwamba operesheni ya Marekani nchini Iran "tayari imefanikiwa".

    Trump asema 'viongozi wengi wa Iran wameuawa

    Awali, Rais Trump alizungumza na ABC News na kusema kwamba mashambulizi ya Marekani "tayari yamesababisha uharibifu mkubwa" na kuwa viongozi "wengi" wa Iran wameuawa.

    "Hatujui yote, lakini mengi yanajulikana," Trump amesema katika mahojiano ya simu. Rais pia ameongeza kuwa Marekani "ina maono mema" juu kundi lijalo la viongozi wa Iran.

    Alipoulizwa kuhusu ni nani atakayechukua nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, Trump kisha ameiambia NBC: "Sijui, lakini wakati fulani watanipigia simu kuuliza ni nani ningependa."

    "Ninakuwa na mzaha kidogo ninaposema hivyo," Trump ameongeza:

    Trump alipoulizwa ikiwa ana 'uhakika' kiongozi mkuu wa Iran ameuawa

    Rachel Scott, mwandishi mkuu wa habari za kisiasa katika shirika la ABC News, amesema Donald Trump amemwambia tu kwamba "anaamini" kiongozi mkuu wa Iran amekufa.

    Alipoulizwa kama ana "uhakika", Trump inasemekana alisema: "Sitaki kusema chochote kwa uhakika hadi nitakapoona kwa maco yangu lakini tunaamini amekufa."

    "Na viongozi wao wengi wameuawa. Sio tu kutoka kwenye eneo moja bali pia kutoka kwenye maeneo mengine mawili ambayo pia tumeshambulia. Tulikuwa na taarifa nyingi za ujasusi hivyo basi, tunaamini viongozi wengi wameuawa."

    Soma zaidi:

  12. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zasema kuwa kiongozi mkuu wa Iran "ameuawa

    Kufuatia Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kusema "kuna dalili zinazoongezeka" zinazoonyesha kuwa kiongozi mkuu wa Iran "ameuawa"’, tunaona ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba ameuawa na mashambulizi ya Marekani na Israeli.

    Shirika la habari la Reuters, limemnukuu afisa mkuu wa Israeli, na kusema kuwa mwili wa Ayatollah Ali Khamenei umepatikana.

    Axios, imenukuu chanzo, na kusema balozi wa Israeli nchini Marekani Yechiel Leiter amewafahamisha maafisa wa Marekani kwamba Khamenei aliuawa katika shambulio lililofanyika kwenye makazi yake huko Tehran.

    Na vyanzo vingi vya Israeli, ikiwa ni pamoja na News 12 na Times of Israel, vinanukuu maafisa wa Israeli pia wakidai kwamba kiongozi huyo mkuu amefariki.

  13. Dalili zinaonyesha kuwa kiongozi mkuu wa Iran 'ameuawa' - Netanyahu

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amezungumzia shambulizi dhidi ya eneo la Iran la kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ambalo tuliliripoti mapema.

    ‘Kuna dalili zinazoongezeka zinazoonyesha kuwa "dikteta huyu" "ameuawa"’, Netanyahu amesema.

    Katika hotuba yake, Netanyahu amewaambia Wairan kuwa mashambulizi hayo yatawasaidia "kujiondoa katika udhalimu" na kuongeza kuwa wana "fursa moja tu" ya kupindua utawala wa Iran.

    "Nendeni mitaani kwa wingi mumalize kazi hii," Netanyahu amesema.

    Ni "wakati muafaka wa kuungana pamoja kwa ajili ya misheni ya kihistoria", Netanyahu ameongeza.

    Amemalizia hotuba yake kwa kuwataka raia wa Israeli kusikiliza ushauri wa usalama kutoka kwa Kamandi ya Nchi baada ya kupendekeza kwamba operesheni dhidi ya Iran itaendelea "kadiri itakavyohitajika".

    Soma zaidi:

  14. Mashambulizi mapya yaripotiwa Iran huku nayo ikifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi

    Mtu mmoja ameiambia BBC Persian kwamba mlipuko mpya umesikika magharibi mwa Tehran.

    Shirika la habari la AFP linaripoti kwamba waandishi wake wamesikia "mfululizo wa milipuko mipya" katika mji mkuu. Hapo awali shirika hilo lilisema shirika la habari la Iran Fars lilikuwa likiripoti kwamba vitongoji viwili katika mji wa Bushehr kusini mwa Iran - kuliko kiwanda cha nguvu za nyuklia - "vililengwa na makombora".

    Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu (IRNA) linaloendeshwa na serikali ya Iran pia linaripoti kuhusu milipuko mipya mjini Tehran.

    Ingawa chanzo hakijajulikana mara moja, hii inakuja baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran mapema hii leo, na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka Iran dhidi ya maeneo lengwa kote Mashariki ya Kati.

    Jeshi la Anga la Israeli pia limechapisha kwenye mtandao wa X, likisema "limeanzisha shambulio lingine la anga na linashambulia maeneo ya kurusha makombora na mifumo ya ulinzi katikati mwa Iran".

    Soma zaidi:

  15. Kuanzia Dubai hadi Doha, Iran yafanya mashambulizi Mashariki ya Kati

    Baada ya mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, hatua ya kulipiza kisasi ya Iran imeshuhudiwa kote Mashariki ya Kati - hasa katika maeneo yenye kambi za kijeshi za Marekani, au ambayo ni washirika wa Marekani:

    • Huko Dubai, UAE, mlipuko umeshuhudiwa katika hoteli ya Fairmont The Palm. Mamlaka ya Dubai imesema watu wanne wamejeruhiwa baada ya "jengo la eneo la Palm Jumeirah" kushambuliwa
    • Wizara ya ulinzi ya UAE pia ilisema imezuia wimbi jipya la makombora na ndege zisizo na rubani za Iran, baada ya kusema hapo awali kwamba nchi hiyo imekabiliwa na "shambulizi baya linalohusisha makombora ya Iran".
    • Huko Doha, Qatar, milipuko imeonekana kulenga kambi ya jeshi la anga ya al Udeid, kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika eneo hilo.
    • Kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani huko Bahrain " imeshambuliwa kwa kombora", kulingana na taarifa iliyonukuliwa na Shirika la Habari la Bahrain linaloendeshwa na serikali.
    • Milipuko ilisikika nchini Kuwait, na shirika la habari la eneo hilo Kuna, lilisema kwamba ndege isiyo na rubani iliyolenga uwanja wa ndege wa kimataifa ilisababisha "majeraha madogo kwa wafanyakazi kadhaa" huku uharibifu "mdogo" ukitokea kwenye kituo cha uwanja wa ndege.
    • Reuters imeripoti kwamba ulinzi wa anga wa Marekani ulidungua ndege isiyo na rubani juu ya kambi ya kijeshi ya Marekani karibu na Erbil, Iraq
    • Jordan - ambayo inapakana na Israeli - inasema kwamba vikosi vyake vya kijeshi vilidungua makombora mawili ya masafa marefu na kwamba vifusi vilianguka katika maeneo mbalimbali
    • Israel pia imeripoti wimbi la makombora ya Iran, huku ving'ora vikilia kote nchini. Jeshi la Israel linasema Iran inataka "kuwatisha raia na kuharibu maeneo yaliyo jirani"

    Soma zaidi:

  16. Waziri wa mambo ya nje wa Iran asema kiongozi mkuu yuko hai

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi amezungumza moja kwa moja na shirika la NBC News huku mtandao ukiendelea kuminywa kwa raia wengi nchini Iran.

    Araghchi anasema kwamba Iran "huenda imepoteza kamanda mmoja au wawili" lakini pia ameongeza kuwa kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, "yuko hai" kulingana na kile anachofahamu.

    Vyombo vya habari vya Iran hadi sasa vimekanusha kwamba maafisa na makamanda kadhaa wa Iran wameuawa, akiwemo rais na kamanda mkuu wa Jeshi.

    Araghchi amesema kwamba kipaumbele kwa Iran ni kupunguza mvutano na iko tayari kwa mazungumzo, mradi tu Marekani na Israel zisitishe mashambulizi yao.

    Huku akisema kwamba hakuna mawasiliano yoyote "hivi sasa", Araghchi ameongeza kwamba "ikiwa Wamarekani wanataka kuzungumza na sisi, wanajua jinsi wanavyoweza kuwasiliana na mimi".

    Iran na Marekani zimekuwa zikishiriki katika mazungumzo mapya ya nyuklia, huku duru ya hivi karibuni ikifanyika siku mbili zilizopita. Araghchi pia amethibitisha kwamba Iran inashambulia kambi za Marekani katika eneo hilo, lakini anaielezea kama kitendo cha "kujilinda".

  17. Habari ya wakati huu msomaji wetu. Leo tunaendelea na matangazo yetu maalum mubashara kukujuza kila kinachoendelea kuhusu mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran. Mimi ni Asha Juma. Karibu.

  18. Jeshi la Israel lasema limekamilisha "shambulio kubwa" dhidi ya Iran

    Jeshi la Israel lilitangaza kuwa limekamilisha "shambulio kubwa" dhidi ya utawala wa Iran.

    Taarifa ya jeshi ilisema: "Moja ya mashambulizi haya yalifanywa kwenye mfumo wa ulinzi wa anga wa juu (SA-65) huko Kermanshah magharibi mwa Iran."

    Taarifa hiyo iliendelea kusema: "Mashambulizi haya yalifanywa kwa lengo la kuanzisha na kuimarisha uhuru wa vitendo wa Jeshi la Anga la Israel juu ya anga ya Iran, ili kudhoofisha uwezo wa Walinzi wa Mapinduzi na vitisho dhidi ya eneo la ndani la Taifa la Israel."

    Soma zaidi:

  19. 'Vigogo kadhaa' wa utawala wa Iran wameuawa - Jeshi la Israel

    Afisa wa jeshi la Israel anasema "maafisa kadhaa wenye ushawishi" wa utawala wa Iran "wameuawa" katika shambulioyala leo.

    Afisa huyo anasema maeneo matatu ambapomaafisa wa serikali ya Iran walikuwa wamekusanyika yalishambuliwa kwa wakati mmoja wakati wa operesheni hiyo.

    Shambulio hilo lilipangwa "kwa muda wa miezi kadhaa", na ujasusi kubaini "fursa ya kuchukua hatua" wakati "maafisa wakuu wa serikali wangekutana".

    Wanaongeza kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limekuwa kifanya kazi "kwa ushirikiano wa karibu" na Jeshi la Marekani ili kupanga orodha "ya thamani" ya shabaha.

    "IDF iko tayari kushambulia Iran tena ikilazimika kufanya hivyo," wanasema.

  20. Waziri Mkuu wa Uingereza: Ndege zetu za kivita ziko angani kulinda watu wetu, maslahi na washirika wetu

    Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, amesema katika hotuba ya televisheni kuwa ndege za kivita za nchi hiyo “ziko angani leo kama sehemu ya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa kikanda ili kulinda watu wetu, maslahi yetu na washirika wetu.”

    Katika tamko lake la kwanza hadharani kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yaliyosababisha Tehran kurusha makombora kuelekea nchi mbalimbali katika eneo hilo, Starmer alisema hatua ya Uingereza “inaendana na sheria za kimataifa.”

    Kauli hiyo ilitolewa baada ya Starmer kuongoza kikao cha dharura cha mawaziri wakuu na maafisa waandamizi wa serikali, kinachojulikana kama kikao cha Cobra, kujadili maendeleo yanayoendelea na kuongezeka kwa mzozo katika Mashariki ya Kati.

    Soma Pia: