Donald Trump apata ushindi wa kishindo na wa kihistoria unaomrejesha tena katika Ikulu ya White House
Donald Trump ameshinda uchaguzi wa Marekani hatua ya kihistoria inayomrejesha katika Ikulu ya White House
Muhtasari
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Maoni kutoka Lebanon: 'Trump na Harris ni sawa'
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Viongozi wa Afrika wampongeza Trump kwa kushinda urais Marekani
- Matokeo ya uchaguzi Marekani:Vipi kuhusu majimbo ambayo yalipaswa kuamua kwa kura kuhusu utoaji mimba?
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Ni vigumu kutabiri jinsi Trump anavyopanga kutatua migogoro ya dunia
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Mkuu wa jeshi la Nigeria aaga dunia akiwa na umri wa miaka 56
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Ujumbe wa Hamas kwa Trump baada ya kupata ushindi: "Tunamhimiza ajifunze kutokana na makosa ya Biden"
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Viongozi wa dunia wampongeza Trump kwa ushindi wa uchaguzi wa rais Marekani
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Waziri mkuu wa Uingereza atazamia kufanya kazi na Trump
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Wafuasi wa Trump 'wana furaha sana' na 'wanahisi kushukuru'
- Matokeo ya uchaguzi Marekani: Ni lini tutajua matokeo rasmi ya uchaguzi Marekani?
- Jimbo la Pennsylvania latabiriwa kumwendea Trump
- Wafuasi wa Trump wanasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwa mgombea wao
- Wafuasi wa Trump washerehekea ushindi katika majimbo mawili muhimu
- Harris hatazungumza usiku wa leo na umati unaondoka
- Pendekezo la haki ya uavyaji mimba huko Florida limeshindwa
- Msimamo wa utawala wa Biden-Harris wa Israel wawaponza huko Michigan
- Upigaji kura wakamilika katika majimbo yote isipokuwa Hawaii na Alaska
- Harris anaungwa mkono na wanawake wengi
- Democrat wanatarajia kuhifadhi jimbo la Arizona
- Kura za wawakilishi maalum 270: Je, wagombea hushinda vipi?
- Trump ashinda katika jimbo la Florida huku shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea
Moja kwa moja
Na Asha Juma, Lizzy Masinga &Dinah Gahamanyi
Chaneli ya WhatsApp ya BBC Swahili: Jinsi ya kujiunga na kupata taarifa bora za habari

Bofya hapa ili kujiunga na chaneli yetu ya WhatsApp ikiwa unatumia simu yako ya mkononi au Wavuti ya WhatsApp.
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2024: Dola, Bitcoin zachupa wakati huu Trump akishinda urais

Chanzo cha picha, Getty Images
Dola ya Marekani imepanda wakati huu Donald Trump akishinda kiti cha urais na kurejea tena Ikulu ya Marekani.
Wawekezaji wanaweka dau kwamba mpango wa Trump wa kupunguza kodi na kuongeza ushuru utaongeza mfumuko wa bei na kupunguza kasi ya ongezeko la viwango vya riba.
Viwango vya juu kwa wawekezaji wa muda mrefu watavuna faida zaidi kwenye akiba na uwekezaji wa dola.
Bitcoin pia imefika rekodi ya juu, kufuatia ahadi ya Trump aliyoitoa katika kampeni kuhusu kuifanya Marekani kuwa kinara katika biashara ya sarafu za mtandaoni na kidigitali duniani.
Maoni kutoka Lebanon: 'Trump na Harris ni sawa'

Chanzo cha picha, Lee Durant
Kabla ya uchaguzi, kulikuwa na kutoridhika sana nchini Lebanon, na kwa kweli katika eneo lote, kuhusu sera ya Rais Biden ya Gaza.
Wengi wanasema Biden amekuwa akihusika katika mauaji ya Wapalestina zaidi ya 40,000 huku vita vya Israel dhidi ya Hamas vikiendelea huko.
Na, wengi wanasema, Marekani iliendelea kuiunga mkono Israel kwa silaha na mabomu yanayotumiwa huko Gaza na sasa dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon.
"Kwa kweli hatujali. Wote [Trump na mgombea wa Democratic, Kamala Harris] wana sera sawa," Sanaa El Banji, mfamasia, alituambia.
"Wanaunga mkono Israel na hawajali vita na hali ya Lebanon. Daima wanaunga mkono sera ya Israel." Lakini, aliongeza: "Trump ni mkali zaidi, aliye wazi zaidi kuliko wengine."

Chanzo cha picha, Lee Durant
Wafa Karameh, mfanyakazi wa umma aliyestaafu, alisema: "Wawili hao [Trump na Harris] ni sawa lakini tunatumai kwa Trump mambo yatakuwa bora kuliko yale ambayo yametokea katika miaka minne iliyopita."
Wakati huo huo, Omar Baalbahi, mhandisi, alisema: "Tunachotarajia ni kwamba ataleta amani katika eneo hili la dunia.

Chanzo cha picha, Lee Durant
Tunatarajia heri. Yeye ni mtu anayezungumza. Tumewaona Wanademokrasia na tumekuwa tukiteseka ... Mtu anapaswa kuwa na matumaini tunayo matumaini tu, sawa?''
Unaweza kusoma;
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2024: Viongozi wa Afrika wampongeza Trump kwa kushinda urais Marekani

Chanzo cha picha, Reuters
Viongozi wa mataifa mbali mbali ya Afrika wamekuwa wakitoa pongezi zao kwa Donald Trump ambaye ameshinda uchaguzi wa urais wa Marekani, kufuatia uchaguzi uliofanyika tarehe nne.
Rais wa Kenya William Samoei Ruto kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika: Mheshimiwa @realDonaldTrump
Kwa niaba ya Serikali na watu wa Jamhuri ya Kenya na kwa niaba yangu binafsi, nawasilisha kwa Mheshimiwa Rais, pongezi zangu za dhati kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa 47 wa Marekani. Ushindi wako ni ushahidi wa azma thabiti la watu wa Marekani ili kurejesha imani katika uongozi wako wa maono, ujasiri na ubunifu. Unapoanza awamu hii ya safari yako ya uongozi, Kenya iko tayari kuimarisha zaidi ushirikiano wetu katika masuala ya maslahi ya pamoja ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, teknolojia na uvumbuzi, amani na usalama, na maendeleo endelevu.
Kenya inathamini ushirikiano wake wa muda mrefu na Marekani kwa zaidi ya miaka sitini uliyojikita katika maadili yetu ya pamoja ya demokrasia, maendeleo na kuheshimiana. Tunatarajia kuimarisha ushirikiano wetu chini ya uongozi wako tunapofanya kazi pamoja kushughulikia changamoto za kimataifa, kukuza amani na usalama na kukuza ukuaji wa uchumi jumuishi kwa manufaa ya watu wetu. Hongera kwa mara nyingine tena Mheshimiwa Rais mteule, na uongozi wako uweze kuleta maendeleo na umoja kwa Marekani na kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yetu mawili makubwa. Tafadhali kubali, Mheshimiwa, pokea hakikisho la imani yangu kwako hapo juu.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Dambudzo Mnangagwa kupitia ukurasa wake wa facebook amesema: Hongera Rais mteule Donald Trump kwa ushindi wako wa uchaguzi.
''Ulimwengu unahitaji viongozi zaidi wanaozungumza kwa niaba ya watu.
Zimbabwe iko tayari kufanya kazi na wewe na watu wa Marekani ili kujenga ulimwengu bora, wenye mafanikio na amani zaidi'', ujumbe wa Mgangagwa ulihitimisha.
Kiongozi wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali pia amempongeza Trump. kaytika ujumbe wake wa X amesema: ''Hongera Rais Donald Trump (@realDonaldTrump) juu ya ushindi wako wa uchaguzi na kurudi. Natarajia kufanya kazi pamoja ili kuimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi zetu mbili katika kipindi chako''.
Katika ukurasa wake wa X , Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema ''Ninakupongeza wewe Mheshimiwa Rais Mteule wa Marekani @realDonaldTrump juu ya ushindi wako wa kihistoria katika uchaguzi. Ninatazamia kuendeleza ushirikiano na ushirikiano thabiti wa mataifa yetu mawili ili kuendeleza amani, usalama na ustawi wa pamoja kwa mataifa yetu mawili.''
Rais wa Misri wa Misri Abdel Fattah El- Sisi kupitia ukurasa wa X anasema: Natoa pongezi zangu za dhati kwa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump@realDonaldTrump. Nakutakia kila la kheri katika kufikia maslahi ya watu wa Marekani. Tunatarajia kufanya kazi pamoja ili kuimarisha amani, kudumisha amani na utulivu wa kikanda, na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Misri na Marekani na watu wao wa kirafiki. Nchi hizi mbili zimekuwa zikitoa mfano wa ushirikiano na zimefanikiwa kwa pamoja katika kufikia maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili rafiki, ambazo tunatarajia kuendelea katika hali hizi muhimu ambazo dunia inapitia.
Wakati huo huo Serikali ya Jamhuri ya Somaliland imetoa pongezi zake za dhati kwa Rais mteule @realDonaldTrump kuhusu ushindi wake. ''Tunatarajia kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya Somaliland na Marekani chini ya uongozi wake'', umesema ujumbe huo kupitia ukurasa wa X.
Soma zaidi:
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2024: Vipi kuhusu majimbo ambayo yalipaswa kuamua kwa kura kuhusu utoaji mimba?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika majimbo 10 ya Marekani, pamoja na uchaguzi wa rais, wapiga kura pia walitakiwa kuamua juu ya suala jingine muhimu: haki za utoaji mimba.
Maeneo haya yanazingatia iwapo yataanzisha ulinzi wa kisheria katika katiba ya majimbo yao ili kumhakikishia mwanamke haki ya kuavya mimba.
Huko Missouri, wapiga kura wamechagua kupitisha ulinzi wa kisheria.
Matokeo sawia yanatangazwa katika majimbo mengine sita, ingawa sio kura zote zimehesabiwa.
Dakota Kusini na Florida zinatarajiwa kupiga kura dhidi ya kuongezwa kwa ulinzi wa kisheria wa haki za uavyaji mimba kwenye katiba.
Unaweza kusoma;
Ni vigumu kutabiri jinsi Trump anavyopanga kutatua migogoro ya dunia,
Donald Trump anapenda kusema kwamba anamaliza vita, lakini anakaribia kurithi migogoro miwili mikubwa ambayo haikuwapo wakati alipokuwa madarakani mara ya mwisho: uvamizi kamili wa Urusi wa Ukraine na vita vya Israel vya pande nyingi katika Mashariki ya Kati.
Halafu kuna Korea Kaskazini, na mipango yake ya nyuklia na makombora ya masafa marefu, na uwezekano unaokuja wa kizuizi cha China cha mshirika wa Marekani, Taiwan.
Jinsi Trump 2.0 atakavyoshughulikia matatizo haya ni vigumu kutabiri, hasa bila mkono thabiti wa majenerali wenye tahadhari, wenye uzoefu mkubwa aliokuwa nao wakati wa urais wake uliopita.
Cha kushangaza, kwamba kutotabirika kwake sana wakati mwingine kunaweza kuwa faida – kunawafanya wapinzani wako wasielewe unachokifikiria.
Je, kurejea kwake kutamsukuma Putin kwenye makubaliano juu ya Ukraine? Je, kutamfanya Kim Jong-Un kurudi kwenye meza ya mazungumzo? Je, kutaizuia Beijing kujaribu kuchukua Taiwan? Je, itailazimisha Iran kuwarejesha wanamgambo wake ili kuzuia mashambulizi ya Israel yanayoungwa mkono na Marekani dhidi ya vituo vyake vya nyuklia?
Mkuu wa jeshi la Nigeria aaga dunia akiwa na umri wa miaka 56

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkuu wa jeshi la Nigeria Jenerali Taoreed Lagbaja amefariki dunia baada ya "kuugua" akiwa na umri wa miaka 56, Rais Bola Tinubu ametangaza.
Aliaga dunia Jumanne usiku jijini Lagos.
Maelezo kamili kuhusu ugonjwa wake hayakutolewa.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye X na msemaji wa rais Bayo Onanuga, Rais Tinubu alitoa salamu zake za "rambirambi" kwa familia ya Jenerali Lagbaja.
"Rais Tinubu anamtakia Luteni Jenerali Lagbaja amani ya milele na anaheshimu mchango wake muhimu kwa taifa," taarifa hiyo ilisomeka.
Kufariki kwake kunaashiria hasara kubwa kwa Wanajeshi wa Nigeria, ambapo "alikuwa na majukumu muhimu katika operesheni nyingi za usalama wa ndani", ilisema taarifa.
Jenerali Lagbaja ameacha mke, Mariya, na watoto wao wawili.
Ujumbe wa Hamas kwa Trump baada ya kupata ushindi: "Tunamhimiza ajifunze kutokana na makosa ya Biden"
Kiongozi mkuu wa vuguvugu la Hamas, Sami Abu Zuhri, amesema Jumatano kwamba Donald Trump atajaribiwa kuhusiana na kauli zake kwamba anaweza kusimamisha vita ndani ya saa chache iwapo atakuwa Rais wa Marekani.
Abu Zuhri aliliambia shirika la habari la Reuters: "Tunamhimiza Trump kujifunza kutokana na makosa ya (Rais Joe) Biden."
Kulingana na Agence France-Presse, Hamas pia ilitoa wito kwa Trump- "kuacha uungwaji mkono bila kujali" wa Israeli.

Viongozi wa dunia wampongeza Trump kwa ushindi wa uchaguzi wa rais Marekani

Chanzo cha picha, Reuters
Pongezi kutoka duniani kote zilianza kumiminika mara tu mgombea wa chama cha Republican Donald Trump alipotangaza ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Marekani.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amempongeza mgombea wa chama cha Republican Donald Trump kwa kile alichokielezea kama "ushindi wake wa kihistoria", na kusisitiza kuwa "uhusiano maalumu" kati ya nchi zao mbili "utaendelea kustawi."
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea utayari wake wa kufanya kazi pamoja. Macron alisema: "Hongera kwa Rais Donald Trump. Tuko tayari kufanya kazi pamoja kama tulivyofanya kwa miaka minne, kwa amani na ustawi zaidi."
Rais wa Tume ya Muungano wa Ulaya Ursula von der Leyen amesisitizia umuhimu wa mahusiano ya Ulaya na Marekani.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pia amempongeza Trump, akisisitiza haja ya kufanya kazi na Marekani "kukuza ustawi na uhuru."
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuelezea Donald Trump kama "rafiki yangu" baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Marekani, akielezea matumaini yake kwamba "uhusiano kati ya Uturuki na Marekani utakuwa imara."
Mfalme Abdullah II wa Jordan pia amempongeza Donald Trump kwa ushindi wake katika uchaguzi wa Marekani, akisisitizia umuhimu wa kuimarisha hatua za pamoja za "kuhakikisha kuna amani na utulivu wa kikanda na kimataifa."
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi pia amempongeza Trump, akisisitiza nia yake ya kufanya kazi pamoja kuleta amani na utulivu katika Mashariki ya Kati.
Emir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, alielezea nia yake ya kufanya kazi na Trump tena, akisema katika chapisho kwenye jukwaa la X, "Natarajia kuimarisha uhusiano wetu na ushirikiano wa kimkakati, na kuimarisha juhudi zetu za pamoja za kukuza usalama na utulivu katika kanda na ulimwengu."

Waziri mkuu wa Uingereza atazamia kufanya kazi na Trump

Chanzo cha picha, Getty Images
Keir Starmer amekuwa kiongozi wa pili duniani kumpongeza Donald Trump kwa kile anachokiita "ushindi wa kihistoria wa uchaguzi".
"Ninatarajia kufanya kazi nanyi katika miaka ijayo," waziri mkuu wa Uingereza anasema, akiongeza: "Kama washirika wa karibu zaidi, tuko bega kwa bega kutetea maadili yetu ya pamoja ya uhuru, demokrasia na biashara.
"Kutoka kwa ukuaji na usalama hadi uvumbuzi na teknolojia, ninajua kuwa uhusiano maalumu wa Uingereza na Marekani utaendelea kufanikiwa pande zote mbili za Atlantiki kwa miaka ijayo."
Unaweza kusoma;
Wafuasi wa Trump 'wana furaha sana' na 'wanahisi kushukuru'

Hali ya hewa nje ya kituo cha mikutano cha Palm Beach – ikiwa ni kumi - ni ya furaha, huku wafuasi wa Donald Trump wakijitokeza mitaani kwa karamu yake ya usiku wa uchaguzi.
Malori ya kubebea mizigo yanayoendesha kwa kupiga honi na mwanamume mmoja kwenye pikipiki anacheza wimbo wa hip-hop wenye maneno ya kumsifu Trump.
Fatima Henges, 30, alicheza kando ya barabara anaonekana akicheza kwenye karamu ya usiku wa leo na kusema "anafuraha, ana furaha kubwa" kuhusu matokeo kufikia sasa.
"Hatutaki kwenda nyumbani, lakini tunapaswa kufanya kazi kesho," anasema. "Nadhani ni vizuri kwa kila mtu, mabadiliko."
Roselba Morales, mhamiaji kutoka Mexico ambaye alipewa uraia wa asili mwaka jana, alikuwa amempigia kura Trump na anafurahi kumuona akifanya vyema usiku wa leo.
"Anataka amani, anataka usalama, anataka kuokoa watoto wetu," anasema, huku akipeperusha bendera kubwa ya Trump. "Ninahisi shukrani, asante Yesu!"
Unaweza pia kusoma:
Trump alisema nini katika hotuba yake ya ushindi?
- Katika saa moja iliyopita, Donald Trump ametangaza ushindi katika uchaguzi wa rais wa Marekani, akitoa hotuba pana kwa wafuasi wake huko Florida.Ikiwa umekosa, haya ndio aliyosema:
- Trump aliwashukuru wapiga kura: "Nataka kuwashukuru raia wa Marekani kwa heshima ya ajabu ya kuchaguliwa kuwa rais wako wa 47 na rais wako wa 45"
- Alisema angeshinda kura maarufu: Kura bado zinahesabiwa, lakini Trump anaonekana kuwa tayari kushinda kura nyingi katika uchaguzi huu. "Marekani imetupa uwezo ambao haujawahi kutolewa na wenye nguvu," alisema
- JD Vance "aligeuka kuwa chaguo zuri": Trump alimsifu mgombea mwenza, ambaye mwenyewe alisema Trump alikuwa ameweka historia kubwa katika taifa la Marekani " wakati wa hotuba.
- Elon musk ni "nyota": Sehemu ya hotuba ya Trump ilitolewa kwa bilionea wa teknolojia, ambaye Trump alisema alikuwa "mtu wa ajabu"
- RFK Jr "ataifanya Marekani kuwa na afya tena": Trump alionekana kupendekeza Robert F Kennedy Jr - aliyekuwa mgombea binafsi wa urais, atakuwa na jukumu linalohusiana na huduma ya afya katika utawala wake. Kennedy alijiondoa kwenye kinyang'anyiro mwezi Agosti ili kumuidhinisha Trump
Matokeo ya uchaguzi Marekani: Ni lini tutajua matokeo rasmi ya uchaguzi Marekani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Donald Trump tayari ametangaza kwamba amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Marekani .
Matokeo yanazidi kutangazwa katika majimbo mbali mbali nchini humo . Je,ni lini tutakapoweza kumjua mshindi na kufahamu matokeo rasmi?
Soma zaidi
Waziri Mkuu wa Israel ampongeza Trump 'kwa ushindi wa kihistoria' unaomrejesha White House

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Netanyahu na Trump, pichani mnamo 2020 Donald Trump ametangaza kupata ushindi katika uchaguzi huu wa urais na baadhi ya viongozi wa dunia wameanza kumpongeza.
"Hongera 'kwa ushindi wa kihistoria! Kurejea kwako kwa kihistoria katika Ikulu ya Marekani kunatoa mwanzo mpya kwa Marekani na kujitolea kwa kipekee kwa muungano mkubwa kati ya Israel na Marekani," anasema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Anaongeza: "Huu ni ushindi mkubwa!"
Naye Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amesema maneno kama hayo: "Amerejea kwa kishindo katika historia ya kisiasa ya Marekani! Hongera Rais Donald Trump kwa ushindi wake mkubwa.
Ushindi unaohitajika sana Ulimwenguni!"
Kumbuka: Trump ametangaza kupata ushindi - lakini bado hajafikia idadi ya 270 ya kura za wawakilishi maalum zinazohitajika.
Soma zaidi:
Trump amtaja Musk kama 'nyota mpya'

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya shangwe na nderemo kutoka kwa umati uliokusanyika, Trump alianza kuzungumza juu ya mtu ambaye amekuwa sehemu muhimu katika kampeni yake - mmiliki wa mtandao wa X na mtu tajiri zaidi duniani Elon Musk.
Alimtaja Musk kama "nyota mpya" wa Chama cha Republican, kabla ya kuendelea kusimulia hadithi ndefu kuhusu jinsi alivyomwacha bilionea huyo akiwa amesimama kwa dakika 40 wakati akitazama video ya roketi ya kampuni ya SpaceX.
Trump Musk anamtaja kama mtu "wa kipekee".
Soma zaidi:
Habari za hivi punde, Trump asema amepata 'ushindi adhimu '

Chanzo cha picha, Reuters
Donald Trump anawahutubia wafuasi wake sasa . Anasema kwamba hii itakuwa "zama za dhahabu" kwa Marekani.
"Huu ni ushindi mzuri sana kwa watu wa Marekani, ambao utaturuhusu kuifanya Marekani kuwa kubwa tena," anaongeza, akitumia kauli mbiu yake ya kampeni.
Trump ametangaza ushindi, ingawa bado hajapata kura rasmi zinazohitajika za wawakilishi maalum wanaopiga kura kumchagua rais

Chanzo cha picha, Reuters
Trump ashukuru familia, akiwemo mke wake Melania
Trump amemshukuru mkewe Melania, akimwita Mama wa Taifa
Amesifu kitabu chake, akisema ndio "namba moja kwa mauzo nchini".
"Amefanya kazi nzuri," amesema, akiongeza "amekuwa na bidii ya kusaidia watu".
Pia amewashukuru “watoto wake wa kipekee,” akiwataja kila mmoja wao wakisimama naye jukwaani.
Trump anamwalika Vance kuhutubia umati
Baadaye, Trump amempongeza mtu ambaye anasema atakuwa makamu wa rais ajaye wa Marekani: JD Vance.
Kisha, akamwomba kuhutubia umati wa watu kidogo.
Vance akapata muda wa kuelezea kampeni ya Trump kama "kitu cha kipekee katika siasa kuwahi kutokea".
Trump amesema Vance alikuwa chaguo bora.
Jimbo la Pennsylvania latabiriwa kumwendea Trump
Jimbo muhimu la Pennsylvania limetabiriwa kuwa litachukuliwa na Donald Trump.
Kura za wawakilishi maalum 19 za jimbo hilo zinamfanya kufikia 265 kwa jumla, pungufu kidogo tu ya 270 zinazohitajika kushinda urais.

Msisimko usio wa kawaida ulishuhudiwa wakati Fox News ilipokadiria ushindi wa Donald Trump katika kinyang'anyiro cha urais.
Unapata hisia ya jinsi ambavyo hata wafuasi wake hawaamini wanachokiona.
Wengi walikuwa tayari kusubiri kwa muda zaidi kabla ya matokeo.
Wafuasi wa Trump wanasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwa mgombea wao

Chanzo cha picha, Reuters
Donald Trump anatarajiwa kuzungumza kutoka makao makuu ya kampeni yake huko Florida muda wowote kutokea sasa.
Wafuasi wa Trump wanasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwa mgombea wao.
Kuna kamera ndani ya ukumbi uliojaa pomoni na muda mfupi uliopita umati wa watu walikuwa wakiruka juu na chini, mbwembwe zikiwa zimetanda kila sehemu.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters
Miongoni mwa watakaokuwepo ni Elon Musk, ambaye amemfanyia kampeni ya kukata na shoka Trump, pamoja na washirika wa kisiasa Robert F Kennedy Jr na Tulsi Gabbard.
Soma zaidi:
Wafuasi wa Trump washerehekea ushindi katika majimbo mawili muhimu
Picha zinaonyesha wafuasi wa Donald Trump wenye furaha, wakisherehekea katika baadhi ya sehemu za Marekani huku mteuzi wao wa rais akisonga mbele katika matokeo yaliyotarajiwa.
Wengine wamevalia kofia zilizoandikwa (Make America Great Again - kauli mbiu ya kampeni ya Trump), wengine wamejifunika bendera ya Marekani.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Reuters
