Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Lebanon yasema watu 274 wameuawa katika siku mbaya zaidi ya mzozo baina ya Israel na Hezbollah

Taarifa kutoka wizara ya afya ya Lebanon zinasema kuwa watu 182 wameuawa na wengine 727 kujeruhiwa, wakiwemo watoto, wanawake na wahudumu wa afya katika mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon yaliyoanza asubuhi ya leo.

Muhtasari

  • Katika picha: Maelfu wakimbia huku Israel ikizidisha mashambulizi Lebanon
  • Tazama: Moshi ukifuka kusini mwa Lebanon baada ya mashambulizi ya Israel
  • Israel inakabiliwa na siku ngumu zijazo, asema Netanyahu
  • Watoto 21 wuawa Lebanon katika mashambulio ya Israel huku idadi ya vifo ikifikia 274
  • Lebanon yasema watu 274 wameuawa katika siku mbaya zaidi ya mzozo baina ya Israel na Hezbollah
  • Viongozi wa Chadema miongoni mwa watu 14 wanaotuhumiwa na polisi Tanzania kwa maandamano yaliyopigwa marufuku
  • Mke wa kiongozi wa upinzani Tanzania Freeman Mbowe na bintie waachiliwa huru
  • Seneta wa Kenya awasilisha hoja ya kupinga tabia ya Naibu wa Rais
  • Tazama: Hali ilivyokuwa katika mji wa Dar es Salaam katika siku ambapo upinzani ulikuwa umepanga maandamano
  • Tazama: Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alivyokamatwa
  • Lebanon yawaonya wakazi wa Kusini kwa ujumbe wa simu kuepuka maeneo ya Hezbollah yanayolengwa
  • Polisi yathibitisha kuwakamata viongozi wa Chadema na wengineo
  • IDF kutekeleza mashambulizi 'makubwa na kwa usahihi' zaidi nchini Lebanon
  • Kwa Picha: Hali ilivyo katika mji wa Dar es Salaam
  • Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akamatwa
  • Polisi watanda Dar es Salaam kuelekea maandamano ya Chadema
  • Sri Lanka yamuapisha rais mpya anayeegemea mrengo wa kushoto
  • Watu sita wafariki dunia baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko Japan
  • Zelensky kuwasilisha 'mpango wa ushindi' kwa Biden, Harris na Trump
  • Kocha wa Arsenal asema sare na Man City ni 'muujiza'
  • Italia: Watu wanne wa familia moja wafariki dunia katika mlipuko wa gesi
  • Trump asema hatagombea tena ikiwa atashindwa katika uchaguzi wa Novemba

Moja kwa moja

Na Asha Juma & Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya mubashara ya leo, tunakuacha na picha hizi za mashambulizi ya Israel nchini Lebanon:

  2. Katika picha: Maelfu wakimbia huku Israel ikizidisha mashambulizi Lebanon

    Mashambulio ya mabomu ya Israel yanaendelea kusini mwa Lebanon, ikiwa ni pamoja na kuzunguka mji wa pwani wa Tiro. Maelfu ya wakazi wanaripotiwa kutoroka eneo hilo kuelekea Beirut.

    Hizi ni picha za hivi punde zinazoingia kwenye chumba cha habari kutoka eneo la tukio.

  3. Tazama: Moshi ukifuka kusini mwa Lebanon baada ya mashambulizi ya Israel

  4. Israel inakabiliwa na siku ngumu zijazo, asema Netanyahu

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye amezungumza hivi punde ameonya kwamba "siku ngumu" zinakuja kwa nchi hiyo.

    Matamshi yake yametolewa baada ya mkutano uliofanyika katika makao makuu ya kijeshi ya Kirya mjini Tel Aviv ambapo alisisitiza kuwa Israel haingojei vitisho badala yake "inaviondoa" akimaanisha mashambulizi ya hivi karibuni ya nchi yake kusini mwa Lebanon.

    "Niliahidi kwamba tutabadilisha uwiano wa usalama, na usawa wa mamlaka katika eneo la kaskazini - hivyo ndivyo tunavyofanya," anasema.

    Wakati haya yakijiri jeshi la anga la Israel kwa sasa linajaribu kuharibu sehemu kubwa ya silaha za Hezbollah sasa. Lakini ingawa linafanikiwa katika muda mfupi, bila makubaliano ya kina ya kusitisha mapigano haitakuwa salama kabisa kwa raia wa Israeli kurejea katika makazi yao yaliyohamishiwa kaskazini.

    Kutuma wanajeshi wa ardhini wa Israeli sio jambo ambalo jeshi la nchi hiyo(IDF) litalifikiria kwa urahisi. Lilitumia miaka 18 ya maumivu ya vita nchini Lebanon, kuanzia mwa 1982 hadi 2000, na hatimaye ilijiondoa wakati majeruhi wake walipozidi kiasi cha kutoweza kuvumilika.

    Hata uvamizi wake mfupi mnamo 2006 ulisababisha hasara chungu. Hezbollah inajua hili, ambayo ndiyo sababu kwa kiasi fulani sasa inaapa kupambana kwa uvumilivu.

  5. Habari za hivi punde, Watoto 21 wauawa Lebanon katika mashambulio ya Israel huku idadi ya vifo ikifikia 274

    Mamlaka za Lebanon zimesasisha hivi punde kuwa idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel leo imefikia watu takriban 274 sasa. 21 kati yao ni watoto, kulingana na wizara ya afya ya Lebanon.

    Watu wengine 1,024 wamejeruhiwa katika mashambulio hayo, wizara hiyo inaongeza.

  6. Lebanon yasema watu 274 wameuawa katika siku mbaya zaidi ya mzozo baina ya Israel na Hezbollah

    Taarifa kutoka wizara ya afya ya Lebanon zinasema kuwa watu 182 wameuawa na wengine 727 kujeruhiwa, wakiwemo watoto, wanawake na wahudumu wa afya katika mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon yaliyoanza asubuhi ya leo.

    Vikosi vya Ulinzi vya Israel vinatahadharisha kuhusu mashambulizi makubwa katika Bonde la Bekaa kaskazini-mashariki mwa Lebanon, ambayo yanaripotiwa kuwa yanaendelea.

    Asubuhi ya leo jeshi la ulinzi la Israel IDF, kupitia msemaji wake Admiral Daniel Hagari, lilisema Hezbollah ina "miundombinu ya kijeshi" na ilitaka "kuligeuza eneo la kusini mwa Lebanon kuwa uwanja wa vita".

    Aliwashauri "raia kutoka vijiji vya Lebanon vilivyo ndani na karibu na majengo na maeneo yanayotumiwa na Hezbollah kwa madhumuni ya kijeshi" kuondoka mara moja kwa ajili ya usalama wao wenyewe.

    Hii ilikuwa kauli isiyo na utata ya jinsi Israel inavyoiona Lebanon lakini kwa wakaazi wa maeneo hayo, hapakuwa na uwazi kuhusu wapi wanapaswa kwenda la iwpo watalengwa na mashambulizi.

  7. Viongozi wa Chadema miongoni mwa watu 14 wanaotuhumiwa na polisi Tanzania kwa maandamano yaliyopigwa marufuku

    Jeshi la polisi nchini Tanzania limetoa ya watu orodha ya watuhumiwa wa maandamano yaliyopigwa marufuku. Miongoni mwa watu waliomo kwenye orodha hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa X ( zamani ikiitwa Twitter) ni Mwenyekiti wa chama cha Chadema, Freeman Aikael Mbowe naMakamu Mwenyekiti wake Tundu Antipas Lissu.

    ‘’jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mikakati ya kuzia vitendo vya uhalifu na kuhakikisha jiji la Dar es Salaam linaendelea kuwa shwari’’, limesema Jeshi hilo la polisi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

    Katika tangazo hilo polisi imesema kuwa viongozi wa chama hicho wali[anga kufanya maandamano tarehe 23/09/2024, ambayo Jeshi la Polisi lilitoa katazo la kutofanyika na kuyapiga marufuku’’

  8. Habari za hivi punde, Mke wa kiongozi wa upinzani Tanzania Freeman Mbowe na bintie waachiliwa huru

    Mke wa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Dr. Lilian Mbowe na bintie, Nicole Mbowe wameachiwa huru katika kituo cha Polisi Oysterbay. Walikamatwa kwa nyakati tofauti leo.

    Jopo la Mawakili likiongozwa na Peter Kibatala limefika kuhakikisha wote waliokamatwa wanaachiwa huru.

  9. Seneta wa Kenya awasilisha hoja ya kupinga tabia ya Naibu wa Rais

    Seneta mmoja nchini Kenya, Danson Mungatana amewasilisha hoja ya kupinga tabia ya Naibu Rais Rigathi Gachagua.

    Kiongozi huyo kutoka kaunti ya Tanariver amesema kuwa aliwasilisha hoja hiyo katika ofisi ya spika wa bunge la seneti mapema Jumatatu.

    Anadai kwamba Naibu huyo wa Rais amejihusisha na siasa za mgawanyiko na kusaliti kiapo chake cha ofisi yake miongoni mwa mengine.

    Hoja ya kupiga tabia dhidi ya mtu fulani ni mjadala wa kupinga vikali mwenendo wa afisa wa serikali; sio hoja ya kumuondoa mamlakani.

    Naibu Rais Rigathi Gachagua amekuwa akilalamikia kutengwa katika shughuli za kitaifa huku kukiwa na madai ya hoja ya kumuondoa madarakani.

    Katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha televisheni nchini Kenya Bw Gachagua alilalamikia kuondolewa katika kundi la WhatsApp la Rais William Ruto ambamo taarifa kuhusu masuala mbali mbali ya kitaifa na ziara za rais hutangazwa.

  10. Tazama: Hali ilivyokuwa katika mji wa Dar es Salaam katika siku ambapo upinzani ulikuwa umepanga maandamano

    Hali ya usalama ilikuwa imeimarishwa katika maeneo ya jiji la kibiashara la Dar es Salaam nchini Tanzania wakati ambapo maandamano yaliyotangazwa na chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yalikuwa yakitarajiwa.

    Baadaye kiongozi wa chama hicho Freeman Mboye baadaye alikamatwa na polisi.

  11. Tazama: Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alivyokamatwa

    Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam .Kabla ya Mbowe kukamatwa, alifika eneo hilo akiwa na gari dogo, kisha kuanza kuzungumza na waandishi wa habari.

    Septemba 11, 2024, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, akiwemo kada wake, Ali Kibao.

    Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.

    Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.

    Unaweza pia kusoma:

  12. Lebanon yawaonya wakazi wa Kusini kwa ujumbe wa simu kuepuka maeneo yanayolengwa ya Hezbollah

    Watu wa kusini mwa Lebanon wamekuwa wakipokea ujumbe wa maandishi na sauti asubuhi ya leo kuwaonya kukaa mbali na "majengo ya makazi ambayo yanatumiwa na Hezbollah kuficha silaha".

    Katika video moja inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii (ambayo niliweza kuithibitisha kupitia watu wanaoishi kusini mwa Lebanon), inaonyesha mwanakijiji ambaye amepokea ujumbe wa sauti, unaosema operesheni ya Israel inaendelea na imeingia katika "hatua mpya".

    Ujumbe wa agizo la sauti unaendelea kusema : "Ikiwa uko katika kijiji kinachotumiwa na Hezbollah, ondoka mara moja kwa usalama wako mwenyewe."

    Ujumbe huu wa simu unakuja wakati maonyo kama hayo yametumwa kwenye mitandao ya kijamii, kwa lugha za Kiingereza na Kiarabu na wasemaji wa jeshi la Israel.

    Maonyo hayo yameelekezwa kwa raia wa kusini mwa Lebanon na Bonde la Bekaa kaskazini mashariki, wakisema wanapaswa kukaa mbali na maeneo ambayo wapiganaji wa Hezbollah wanaendesha harakati zao au kuficha silaha.

  13. Polisi yathibitisha kuwakamata viongozi wa Chadema na wengineo

    Polisi nchini Tanzania imewakamata watu kumi na wanne (14) wakiwemo viongozi wa chama hicho Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Godbless lema.

    Kwa mujibu wa taarifa ya polisi viongozi hao wamekamatwa wakiwa wanahamasisha kufanyika kwa maandamano ambayo hayana kibali.

    "Taarifa rasmi tunazozitoa nikuwa watu hawa tunawashikilia na sio kuwa wametekwa kama taarifa zinazozagaa, huko mtaani ulinzi umeendelea kuhamasishwa ili kuilinda amani tulionayo," ameeleza Mkuu wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Jumanne Muliro.

    Polisi wanaendelea kusisitiza kuwa hakuna kibali cha kufanya maandamano hivyo wataendelea kuwakamata wote wanaohamasisha maandano hayo.

    Aidha polisi hawajaweka wazi ni lini watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani.

    Soma zaidi:

  14. IDF kutekeleza mashambulizi 'makubwa na kwa usahihi' zaidi nchini Lebanon

    Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel, Admiral Daniel Hagari, amesema jeshi litafanya mashambulizi makubwa na kwa usahihi zaidi nchini Lebanon.

    Ameonya watu akiwataka kuondoka kutoka maeneo lengwa ya Hezbollah "kwa usalama wao wenyewe".

    Hili linatokea baada ya wikiendi iliyosheheni mashambulizi huku mvutano ukiongezeka Mashariki ya Kati.

    Hezbollah yenye makao yake Lebanon ilirusha makombora 150 ndani ya Israel, kulingana na IDF, katika kile ilichosema ni kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya hivi majuzi yaliyoilenga Israel.

    Baadhi ya mashambulizi haya yalitokea kusini zaidi ndani ya Israeli kuliko shambulio lolote kutoka upande wa Lebanon tangu 8 Oktoba 2023, na nyumba zikaharibiwa.

    Israel pia ilifanya mashambulizi ya anga ikilenga maeneo ya kusini mwa Lebanon na kusema kuwa imeharibu maelfu miundombinu inayotumiwa kurusha roketi za Hezbollah.

    Pia, mazishi yalifanyika ya kamanda wa operesheni za Hezbollah Ibrahim Aqil, ambaye aliuawa katika shambulio la Israel kwenye viunga vya kusini mwa Beirut siku ya Ijumaa.

    Wizara ya afya ya Lebanon inasema watu 45, wakiwemo watoto watatu, waliuawa katika shambulizi la Ijumaa.

    Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant amezungumza na waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.

    Gallant anasema alimpa mwenzake wa Marekani "tathmini ya hali ya vitisho vya Hezbollah na kumfahamisha juu ya operesheni za IDF za kudhalilisha uwezo wa Hezbollah wa kuanzisha mashambulizi dhidi ya raia wa Israel," katika ujumbe kwenye mtandao wa X.

    Hali ya usalama wa kikanda kwa ujumla na "vitisho vinayotokana na Iran na washirika wake" pia yalizungumziwa, amesema.

    Soma zaidi:

  15. Kwa Picha: Hali ilivyo katika mji wa Dar es Salaam

  16. Habari za hivi punde, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akamatwa

    Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam .Kabla ya Mbowe kukamatwa, alifika eneo hilo akiwa na gari dogo, kisha kuanza kuzungumza na waandishi wa habari.

    Septemba 11, 2024, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, akiwemo kada wake, Ali Kibao.

    Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.

    Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.

    Amesema jambo lingine waliloliomba ni kurejeshewa kwa viongozi wa chama hicho, waliotekwa kwa nyakati tofauti wakiwa hai au hali ya umauti, akiwemo Deusdetith Soka, Dioniz Kipanya, Jacob Mlay na Mbwana Kombo.

    Sooma zaidi:

  17. Polisi watanda Dar es Salaam, Lissu akamatwa

    Polisi wa kupambana na ghasia wamekusanyika katika maeneo kadhaa katika jiji la Dar es Salaam asubuhi ya leo, kuelekea maandamano ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

    Vyombo vya habari vya ndani, vimeripoti uwepo usio wa kawaida wa polisi na magari ya maji ya kuwasha katika eneo la Ilala Boma na Magomeni katika jiji hilo la kibiashara.

    Chadema kilitangaza kitafanya maandamano ya kulaani matukio ya kutekwa watu na mauaji, lakini Jeshi la Polisi lilitangaza kupiga marufuku maandamano hayo.

    “Napenda kuwatangazia kuwepo kwa maandamano, kesho tarehe 23, Septemba, 2024 kuanzia saa tatu asubuhi. Yataanzia maeneo mawili, Ilala Boma na Magomeni Mapipa kuelekea viwanja vya Mnazi Mmoja,” alisema mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe siku ya jana.

    Vile vile, leo asubuhi Chadema imeandika kwenye akauti yake katika mtandao wake wa X, kwamba Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti wake Tundu Lissu.

    Maandamano na mikutano ya hadhara ya kisiasa yalipigwa marufuku kwa muda mrefu wakati wa utawala wa hayati John Pombe Magufuli, na mwanzoni mwa mwaka 2023 mrithi wake Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza ruhusa ya mikutano na shughuli nyingine za kisiasa.

    Soma zaidi:

  18. Sri Lanka yamuapisha rais mpya anayeegemea mrengo wa kushoto

    Rais mpya wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake ameapishwa kushika wadhifa huo, na kuahidi siasa "safi" huku nchi hiyo ikipata nafuu kutokana na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi.

    Dissanayake wa mrengo wa kushoto amejitokeza kama ‘mvurugaji’ wa hali ilivyo, na wachambuzi wanaona ushindi wake ni wa kukataa ufisadi na ushabiki wa kisiasa ambao umeisumbua nchi hiyo kwa muda mrefu.

    Uchaguzi wa Jumamosi ulikuwa wa kwanza tangu 2022, wakati kutoridhika kwa hali uchumi kulichochea maandamano makubwa na kusababisha kutimuliwa kwa rais wa zamani Gotabaya Rajapaksa kutoka madarakani.

    "Tunahitaji kuanzisha utamaduni mpya wa siasa safi," alisema. "Ninajitolea kufanikisha hili. Tutafanya kila linalowezekana ili kurejesha heshima ya watu na imani kwa mfumo wa kisiasa."

    Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 55, ambaye pia anajulikana kama AKD, aliwaambia raia wa Sri Lanka kwamba "demokrasia haiishii kwa kumteua kiongozi".

    "Tunahitaji kuimarisha demokrasia. Ninaahidi kufanya kila niwezalo kulinda demokrasia," alisema.

    "Nilishasema hapo awali kwamba mimi si mchawi - mimi ni raia wa kawaida. Kuna mambo ninayojua na nisiyoyajua. Lengo langu kuu ni kukusanya wale wenye ujuzi kusaidia kuinua nchi hii."

    Soma zaidi:

  19. Watu sita wafariki dunia baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko Japan

    Watu sita wamefariki dunia na wengine 10 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Ishikawa nchini Japan.

    Miji ya Wajima na Suzu, ambayo bado inaendelea kujikwamua kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililoharibu eneo hilo tarehe 1 Januari, ni miongoni mwa miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo, yaliyoanza Jumamosi na kuendelea hadi saa sita mchana kwa saa za huko siku ya Jumatatu.

    Siku ya Jumapili, miji yote miwili ilishuhudia mara mbili ya kiwango cha mvua wanachopata kwa kawaida mnamo mwezi Septemba kwa mwaka, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Mito mingi ilivunja kingo zake, kukata barabara na kutenga jamii zaidi ya 100 katika wilaya nzima, ripoti ziliongeza.

    Watu wawili kati ya waliofariki walipatikana karibu na mtaro ulioangukiwa na maporomoko ya udongo huko Wajima.

    Mmoja wao alikuwa mfanyakazi wa ujenzi anayefanya ukarabati wa barabara.

    Shirika la hali ya hewa la Japan lilitoa tahadhari ya juu zaidi "ya kutishia maisha" kwa eneo la Ishikawa siku ya Jumamosi na kuishusha hadi kwenye onyo la kawaida siku ya Jumapili.

    Hata hivyo, mamlaka imetoa wito wa kuendelea kuwa waangalifu kwani huenda mvua hiyo ikaendelea kunyesha hadi saa sita mchana siku ya Jumatatu.

    Mafuriko hayo yaliathiri makazi ya muda yaliyojengwa kwa ajili ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi la Siku ya Mwaka Mpya.

    Picha zilizopeperushwa na NHK zilionyesha mtaa mzima wa Wajima ukiwa umezama chini ya maji.

    Watu sita wamefariki dunia na wengine 10 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Ishikawa nchini Japan.

    Miji ya Wajima na Suzu, ambayo bado inaendelea kujikwamua kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililoharibu eneo hilo tarehe 1 Januari, ni miongoni mwa miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo, yaliyoanza Jumamosi na kuendelea hadi saa sita mchana kwa saa za huko siku ya Jumatatu.

    Siku ya Jumapili, miji yote miwili ilishuhudia mara mbili ya kiwango cha mvua wanachopata kwa kawaida mnamo mwezi Septemba kwa mwaka, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Mito mingi ilivunja kingo zake, kukata barabara na kutenga jamii zaidi ya 100 katika wilaya nzima, ripoti ziliongeza.

    Watu wawili kati ya waliofariki walipatikana karibu na mtaro ulioangukiwa na maporomoko ya udongo huko Wajima.

    Mmoja wao alikuwa mfanyakazi wa ujenzi anayefanya ukarabati wa barabara.

    Shirika la hali ya hewa la Japan lilitoa tahadhari ya juu zaidi "ya kutishia maisha" kwa eneo la Ishikawa siku ya Jumamosi na kuishusha hadi kwenye onyo la kawaida siku ya Jumapili.

    Hata hivyo, mamlaka imetoa wito wa kuendelea kuwa waangalifu kwani huenda mvua hiyo ikaendelea kunyesha hadi saa sita mchana siku ya Jumatatu.

    Mafuriko hayo yaliathiri makazi ya muda yaliyojengwa kwa ajili ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi la Siku ya Mwaka Mpya.

    Picha zilizopeperushwa na NHK zilionyesha mtaa mzima wa Wajima ukiwa umezama chini ya maji.

    Soma zaidi:

  20. Zelensky kuwasilisha 'mpango wa ushindi' kwa Biden, Harris na Trump

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatazamiwa kuwasilisha kile alichokiita "mpango wake wa ushindi" kwa Rais Joe Biden wakati wa ziara yake nchini Marekani wiki hii.

    Baada ya kukutana na Biden, Zelensky alisema anakusudia kuwasilisha mpango wake kwa Bunge na kwa wagombea wawili katika uchaguzi wa Marekani - Makamu wa Rais Kamala Harris na rais wa zamani Donald Trump.

    Trump hapo awali alikosoa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine na kumsifu Rais wa Urusi Vladimir Putin lakini akasema "pengine" atakutana na Zelensky.

    Ziara ya rais wa Ukraine nchini Marekani - ambako pia anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa - inaambatana na juhudi kutoka Ikulu ya White House kuandaa kifurushi kipya cha msaada wa kijeshi cha $375m kwa Ukraine.

    "Hili litaamua mustakabali wa vita hivi," Zelensky alisema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X pamoja na kwenye video aliyoitoa usiku akishuka kwenye ndege.

    Katika taarifa kabla ya ziara hiyo, kiongozi huyo wa Ukraine alihakiki vipengele vitatu vya mpango huu wa ushindi.

    Aliorodhesha michango zaidi ya silaha kwa ajili ya kijeshi na juhudi za kidiplomasia kuilazimisha Urusi kuingia katika amani, na kuiwajibisha Moscow kwa uvamizi wa nchi yake mwaka 2022.

    Ukraine imekuwa ikiomba kwa miezi kadhaa kwa Marekani, Uingereza na washirika wengine wa Magharibi kuondoa vikwazo vya utumiaji wa makombora ya masafa marefu ili iweze kulenga maeneo kadhaa nchini Urusi ambayo Kyiv inasema hutumiwa kuanzisha mashambulizi.

    Mapema mwezi Septemba, Putin alizionya nchi za Magharibi kwamba atazingatia mashambulizi ya makombora ya masafa marefu kama "ushiriki wa moja kwa moja" wa muungano wa kijeshi wa Nato katika vita.

    Soma zaidi: