Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Trump asema Marekani inatafakari uwezekano wa kufikia makubaliano kuhusu Greenland

Rais wa Marekani Donald Trump alisema hatatumia nguvu kuichukua Greenland baada ya kile alichokiita mkutano uliofanikiwa pakubwa na kiongozi wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za magaribi NATO.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Mbunge wa Uganda na mshirika wa Bobi Wine akamatwa kwa ghasia za uchaguzi

    Polisi nchini Uganda wamemkamata mbunge na mshirika wa karibu wa kiongozi wa upinzani Bobi Wine kwa madai ya kuhusika katika ghasia zilizohusiana na uchaguzi wiki iliyopita.

    Muwanga Kivumbi, naibu kiongozi wa Wine's National Unity Platform (NUP), anatuhumiwa kuandaa mashambulizi kwenye kituo cha polisi na kituo cha kujumlisha kura baada ya kushindwa kwao katika uchaguzi, jambo ambalo chama kinakanusha.

    Polisi wamesema kuwa watu saba waliuawa katika tukio hilo, lakini mwanasiasa huyo ametoa maelezo tofauti, akisema kuwa watu 10 waliuawa nyumbani kwake wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa ubunge.

    Jeshi la Polisi la Uganda lilisema katika chapisho la X siku ya Alhamisi kwamba Kivumbi "atafikishwa mbele ya mahakama kwa wakati ufaao".

    "Kukamatwa kwake kunahusiana na matukio ya hivi majuzi ya vurugu za kisiasa," iliongeza.

    Kukamatwa kwa Kivumbi kunafuatia mvutano baada ya uchaguzi wa wiki jana ambapo Rais Yoweri Museveni alichaguliwa tena kwa muhula wa saba.

  2. Rais wa Bunge la Ulaya: Iran lazima iwe huru na itakuwa huru

    Rais wa Bunge la Ulaya amesema, "Kuanzia mitaa ya Tehran hadi katikati mwa Bunge la Ulaya, ujumbe uko wazi: Iran lazima iwe huru, Iran itakuwa huru."

    Roberta Metsola aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba Bunge la Ulaya "lilipiga kura kwa wingi mno kuunga mkono matarajio ya watu wa Iran."

    Aliandika kwamba Bunge la Ulaya limeitaka serikali ya Iran kuchukua hatua madhubuti "kukomesha ghasia" na kukomesha "ukandamizaji wa kikatili na mauaji makubwa ya waandamanaji wa amani."

    Kwa mujibu wa Bi Metsola, Bunge la Ulaya pia limetoa wito wa "kusitishwa kwa hukumu ya kifo" na kuiambia Iran kwamba ni lazima "ikomesha mara moja mauaji ya serikali yanayotekelezwa ili kunyamazisha upinzani."

    Kwa mujibu wa Rais wa Bunge la Ulaya, wanachama wa taasisi hii wanatoa wito wa kuachiliwa kwa wale waliowekwa kizuizini na "waandamanaji wote waliowekwa kizuizini na wafungwa wa kisiasa."

    Taasisi hiyo muhimu ya Ulaya pia imetoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya vipengele vya ukandamizaji nchini Iran, "Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu litangazwe kuwa shirika la kigaidi" na maafisa wake kufunguliwa mashtaka.

    Mwishoni mwa ujumbe huu, Bibi Metsola pia aliwaandikia watu wa Iran: “Hata nyaya zikikatwa tunasikia sauti yako, hata kukatika kwa umeme tunakuona, hauko peke yako. Bunge la Ulaya linasimama nawe kidete.

  3. Trump: Serikali ya Iran ilikuwa ikiwapiga risasi watu barabarani bila kujali

    Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alisafiri hadi Uswizi kuhudhuria mkutano wa Davos, alisema katika maoni yake ya hivi punde kuhusu maandamano ya Iran na ukandamizaji wao kwamba Jamhuri ya Kiislamu "imewapiga risasi watu barabarani bila kujali."

    Bw. Trump, akirejelea matamshi yake ya awali, alisema, "Walikuwa wanaenda kuwanyonga watu 837 siku ya Alhamisi. Niliwaambia, 'Hamuwezi kufanya hivyo.'

    Ameelezea matumaini kuwa serikali ya Iran haitachukua "hatua zaidi" kuwakandamiza waandamanaji.

    Rais wa Marekani pia alisema kuhusiana na suala la nyuklia la Iran kwamba "Iran lazima iache kujaribu kupata silaha za nyuklia na akaonya juu ya uwezekano wa kuchukua hatua za baadaye ikiwa juhudi hizo hazitasimamishwa."

    "Kwa hivyo tutajua walipo sasa kuhusiana na kile wanachofanya na nyuklia," Bw. Trump alisema. "Hawawezi kukuza nyuklia. Wanapaswa kuacha nyuklia"

  4. Trump ashawishi serikali za dunia kuhusu kamati ya Amani anayounda

    Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye bado yuko Devos, anazungumzia Tume ya Amani, tume ambayo anaitafutia soko, na akasema kwamba "kila mtu" anataka kuwa sehemu ya tume anayoiunda.

    Trump aliongeza kuwa ataendelea "kufanya kazi na serikali nyingine, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa."

    Trump pia alirejea kwa Tume ya Amani, akisema ina uwezo wa kuwa "moja ya taasisi muhimu zaidi kuwahi kuundwa," akiongeza kuwa itakuwa "heshima" kuwa mwenyekiti wake.

    "Inaendelea vizuri sana... kila nchi inataka kujiunga nayo," alisema.

    Hata hivyo, Uingereza inajizuia kujiunga na Tume ya Amani kwa sababu ya wasiwasi kuhusu ushiriki wa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin.

    Unaweza kusoma;

  5. Iran: Katika tukio la shambulio dhidi ya Iran, kambi zote za Marekani zitakuwa shabaha yetu

    Ali Abdollahi, kamanda wa IRGC Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya ya Kati, ametishia kwamba shambulio lolote dhidi ya Iran "litafanya kambi zote za Marekani kuwa shabaha zetu halali."

    Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, Bwana Abdollahi alisema, "Jibu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litakuwa la haraka zaidi, sahihi zaidi na la kuumiza zaidi kuliko hilo."

    Hapo jana, Rais Donald Trump wa Marekani katika mahojiano yake ya hivi punde zaidi ya televisheni, alisema akijibu vitisho vya siku chache zilizopita kutoka kwa maafisa na watu wenye misimamo mikali mjini Tehran ambao walitishia kumuua bila kukusudia kwamba iwapo hatua hiyo itachukuliwa dhidi ya maisha yake, Marekani "itailipua" Iran yote.

  6. Trump atangaza hadharani uwezo wa nyuklia wa Iran "umeharibiwa"

    Rais Donald Trump akizungumza kuhusu mashambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwaka jana, ambayo alisema "iliharibu kabisa" uwezo wa nyuklia wa nchi hiyo.

    "Iran inataka kuzungumza, na watazungumza," Trump aliongeza, kabla ya kuendelea kuzungumzia operesheni dhidi ya kundi linalojiita Islamic State (ISIS) nchini Syria.

    Trump kisha akasema kwamba "mambo mengi mazuri yanatokea," na akaelezea jinsi vitisho kwa Ulaya, Marekani na Mashariki ya Kati "vinapungua au kupungua." "Mwaka mmoja tu uliopita ulimwengu ulikuwa unawaka kihalisi, na watu wengi hawakujua," aliongeza.

    Kulingana na afisa wa zamani wa Pentagon, kutokana na kupungua kwa maandamano ya barabarani, Marekani inaweza kuendeleza sera ya shinikizo kwa kutishia rasilimali za mafuta za Iran ili kuirudisha Iran kwenye meza ya mazungumzo, badala ya kuchukua hatua moja kwa moja.

    "Ikiwa watu hawapo mitaani, itakuwa vigumu sana kufanya shambulizi na hiyo ndio changamoto," anasema Mara Carlin.

    "Kundi la meli za kubeba ndege huenda likawasili katika eneo hilo katikati ya wiki ijayo, na labda ikiwa mambo yanaonekana kuwa shwari na watu hawapo mitaani, meli zitakaa katika eneo hilo kama kizuizi."

    Kinachoonekana kuwa na uhakika hadi sasa ni kwamba Donald Trump si wa kawaida katika maamuzi yake. Wakati wa vita vya siku 12, awali alisema Marekani haitashiriki katika shambulio dhidi ya Iran, lakini ghafla akaamuru shambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.

    Mwaka uliopita, kulingana na shirika la "Armed Conflict Events and Locations Database" (ACLED), Marekani imefanya mashambulizi 626 ya anga katika nchi mbalimbali duniani kote, ikiwa ni pamoja na Somalia, Iran, Yemen, Nigeria, Venezuela, Iraq na Syria, yote yalifanywa kwa idhini ya rais wa Marekani.

    Mara Carlin anasema, kwa marais waliopita unajua wakati serikali iko tayari kutumia nguvu za kijeshi na wakati ambapo haitaki kutumia nguvu za kijeshi. Lakini kwa Rais Trump, kila kitu hakina uhakika na ni vigumu sana kutabiri."

    Soma Zaidi:

  7. Vita vya Ukraine 'vimegeuka kuwa vigumu zaidi' kumaliza - Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump amerudia madai yake kwamba amesuluhisha vita nane tangu aingie madarakani.

    Hata hivyo, Trump anasema anaamini suluhu lingine "linakuja hivi karibuni".

    Kuhusu vita vya Ukraine, anasema: "Ile niliyodhani itakuwa rahisi imegeuka kuwa pengine ngumu zaidi."

    Marekani imefichua mambo yote 28 ya pendekezo lake la kumaliza vita vya Urusi na Ukraine kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

    Mpango huo, ambao umekosolewa vikali kwa kuwa unaipendelea Urusi na waangalizi wengi, uko katika hatua yake ya rasimu na bado haujawekwa wazi.

    Rais Vladimir V. Putin wa Urusi amesema mpango huo unaweza "kuwa msingi wa makubaliano ya mwisho ya amani."

    Pia utakuwa ushindi mkubwa kwa kiongozi huyo wa Urusi, akiweka mipaka kwa nguvu za Magharibi, na kulazimisha Ukraine kuachia eneo ambalo haijapoteza kwenye uwanja wa vita.

    Soma Pia :

  8. Rais wa Uganda Yoweri Museveni amteua Flavian Zeija kuwa Jaji Mkuu

    Dkt. Flavian Zeija ameteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Uganda, akichukua nafasi ya Jaji Alfonse Owiny-Dollo Chigamoy aliyestaafu.

    Bunge la Uganda pia limethibitisha kuwa limekamilisha mchakato wa kumsaili na kumuidhinisha Dkt. Zeija.

    Ikulu ya Uganda ilithibitisha katika taarifa ya Alhamisi kuwa, kwa kutumia mamlaka aliyopewa Rais chini ya Kifungu cha 142(1) cha Katiba ya mwaka 1995, na kwa ushauri wa Tume ya Huduma za Mahakama, Rais Yoweri Kaguta Museveni amemteua Mheshimiwa Jaji Flavian Zeija kuwa Jaji Mkuu wa Uganda.

    Taarifa hiyo ilieleza kuwa uteuzi huo ulifuatia kuwasilishwa kwa jina la Jaji Zeija bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa, ambapo Bunge lilitoa idhini hiyo kwa mujibu wa katiba.

    Inaripotiwa kuwa Tume ya Huduma za Mahakama iliwasilisha majina ya Jaji Izama Madrama, Mike Chibita na Flavian Zeija kama wagombea waliokidhi vigezo, na kumpendekeza Rais achague mmoja kati yao.

    Uteuzi huu umetangazwa siku chache tu baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu, Alfonse Owiny-Dollo Chigamoy, kustaafu rasmi baada ya kutimiza umri wa lazima wa miaka 70.

    Owiny-Dollo alimkabidhi rasmi ofisi Jaji Zeija, akieleza kuwa sheria inamtaka Jaji Mkuu anayestaafu kumkabidhi madaraka naibu wake iwapo Jaji Mkuu wa kudumu bado hajateuliwa na Rais.

    Katika hali hii, Dkt. Zeija amekuwa Jaji Mkuu kaimu tangu Jumatatu alasiri, alipokabidhiwa ofisi hiyo.

    Vyanzo vimeeleza pia kuwa kulifanyika tukio jingine la makabidhiano jana bila uwepo wa vyombo vya habari katika makao makuu ya Mahakama, baada ya makabidhiano ya Jumatatu kufanyika kwa haraka ili kuepuka ukosoaji wa umma kuhusu ucheleweshaji wa mchakato huo.

    Uteuzi wa Dkt. Zeija umewashangaza wengi ndani ya Mahakama na hata Tume ya Huduma za Mahakama, kwani amepanda cheo kwa kasi kubwa.

    Amekaa chini ya mwaka mmoja tu katika nafasi ya Naibu Jaji Mkuu kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu.

    Dkt. Zeija aliteuliwa kuwa Naibu Jaji Mkuu tarehe 7 Februari 2025, akimrithi aliyekuwa Naibu Jaji Mkuu mstaafu, Jaji Richard Buteera. Kabla ya hapo, alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama (Principal Judge), nafasi ambayo baadaye ilishikiliwa kwa kaimu na Jaji Jane Okuo Kajuga kwa takriban mwaka mmoja.

    Mwezi uliopita, Rais Museveni alimteua rasmi Jaji Jane Okuo Kajuga, aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama (Principal Judge).

    Aidha, Spika wa Bunge la Uganda amethibitisha kuwa Jaji Flavian Zeija alisailiwa na Kamati ya Uteuzi ya Bunge baada ya kuteuliwa na Rais Museveni kuwa Jaji Mkuu.

    Spika alisema: “Mapema leo, Kamati ya Uteuzi ilikutana na kumsaili Jaji Flavian Zeija, ambaye aliteuliwa na Rais Museveni.”

  9. Ni nchi zipi zimekubali kujiunga na Bodi ya Amani ya Trump?

    Bodi ya Amani itaundwa na viongozi wa dunia, na awali ilibuniwa kama sehemu ya mpango wa kujenga upya Gaza, lakini mamlaka yake yamepanuka.

    Siku ya Jumatano, nchi saba zikiwemo Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na Misri zilitangaza kujiunga na bodi hiyo.

    Israel pia imethibitisha hadharani ushiriki wake.

    Idadi ya nchi zilikuwa tayari zimejiandikisha - ikiwa ni pamoja na Morocco, Belarus na Bahrain.

    Canada, Urusi na Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yamealikwa pia.

    Leo asubuhi Waziri wa Mambo ya Nje Yvette Cooper aliiambia BBC kwamba Uingereza haitatia saini leo, akielezea wasiwasi kuhusu kuhusika kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin.

    Trump ndio ameanza kuongea katika kongamano hilo linaloendelea kwasasa.

    Anaiita "siku ya kusisimua sana, ndefu katika kutengeneza". Anadai "kila mtu" anataka kuwa sehemu ya Bodi yake ya Amani.

    Anasema ataendelea "kufanya kazi na wengine wengi, ukiwemo Umoja wa Mataifa".

    Soma pia:

  10. Uingereza yasita kujiunga na Bodi ya Amani ya Trump, kisa?

    Uingereza imeamua kusubiri kabla ya kujiunga na Bodi ya Amani inayopendekezwa na Rais wa Marekani, Donald Trump, kutokana na wasiwasi kuhusu uwezekano wa ushiriki wa kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin.

    Waziri wa Mambo ya Nje, Yvette Cooper, amesema kuwa Uingereza ilialikwa kujiunga na bodi hiyo, lakini “haitakuwa miongoni mwa watia saini leo” katika hafla iliyopangwa kufanyika wakati wa Jukwaa la Uchumi Duniani mjini Davos.

    Akizungumza na BBC, Cooper alieleza kuwa serikali ya Uingereza bado inapitia kwa makini athari na mwelekeo wa mpango huo.

    Kwa mujibu wa Cooper, bodi hiyo ni “mkataba wa kisheria unaozua masuala mapana zaidi” kuliko lengo la awali la mpango huo, ambalo lilijikita katika kusitisha vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza.

    Hati ya mkataba uliopendekezwa na Ikulu ya White House haitaji eneo la Palestina, na inaonekana kulenga kuchukua au kuchukua nafasi ya baadhi ya majukumu yanayotekelezwa kwa sasa na Umoja wa Mataifa.

    Uamuzi huo umeibua maswali kuhusu athari zake kwa mfumo wa kimataifa wa diplomasia na usimamizi wa amani.

    Soma pia:

  11. Polisi wa Afrika Kusini hawajaweza kudhibiti magenge ya uhalifu, waziri asema

    Waziri wa masuala ya Polisi wa Afrika Kusini Firoz Cachalia amesema kwamba vikosi vya usalama bado havijaweza kupambana na magenge hatari ya wahalifu, katika kukiri waziwazi kunakoonesha ukubwa wa tatizo la uhalifu nchini humo.

    Ghasia za magenge, pamoja na wizi, zinachangia mauaji mengi nchini Afrika Kusini, ambayo ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani.

    Cachalia alisema vurugu za magenge zimezidi kuwa ngumu, hasa katika majimbo ya Eastern Cape na Western Cape, zikihitaji mikakati mipya zaidi ya polisi wa jadi. "Siamini kwamba kwa sasa tuko katika nafasi ya kushinda magenge haya," waziri huyo aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.

    Afrika Kusini, taifa lenye viwanda vingi zaidi barani Afrika, imekuwa ikipambana na uhalifu uliojikita zaidi.

    Watu wengi nchini Afrika Kusini wanamiliki bunduki zenye leseni kwa ajili ya kujilinda, lakini kuna bunduki nyingi zaidi haramu zinazosambazwa.

    Data ya polisi inaonesha kwamba wastani wa watu 63 waliuawa kila siku kati ya Aprili na Septemba mwaka jana.

    Unaweza kusoma;

  12. Jopo la Baraza la Wawakilishi la Marekani lamshutumu Clinton na mkewe kudharau wito katika uchunguzi wa Epstein

    Jopo muhimu la bunge la Marekani limepiga kura ya kumshutumu Rais wa zamani Bill Clinton na mkewe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinton, kwa kudharau Bunge kutokana na kukataa kwao kuitika wito katika uchunguzi wake dhidi ya Jeffrey Epstein wa aliyehukumiwa kwa uhalifu wa makosa ya ngono.

    Kamati ya Usimamizi ya Baraza la Wawakilishi inayoongozwa na Republican iliidhinisha hatua hiyo ya dharau, kwa kuungwa mkono na Wademokrasia kadhaa, na sasa itapelekwa kwa Baraza lote la Wawakilishi kwa ajili ya kupigiwa kura.

    Ikiwa itapitishwa na baraza la wawakilishi, suala hilo litapelekwa kwenye wizara ya sheria. Kamati hiyo ilikuwa imewaita wote wawili kutoa ushahidi kuhusu Epstein, ambaye Bill Clinton ameonekana naye kwenye picha katika miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

    Unaweza kusoma;

  13. Mwandishi wa habari wa Ufilipino akutwa na hatia ya kufadhili ugaidi

    Mwandishi wa habari kutoka Ufilipino amekutwa na hatia ya kufadhili ugaidi na kuadhibiwa kifungo cha miaka isiyopungua 12 gerezani, jambo ambalo mashirika ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyataja kama “kukiuka haki”.

    Frenchie Mae Cumpio, mwenye umri wa miaka 26, alikamatwa mnamo Februari 2020 baada ya wanajeshi kuchunguza nyumba yake ya kulala usiku na kudaiwa kupatikana handgrenadi, silaha, na bendera ya kikomunisti kitandani mwake.

    Mashirika ya haki za binadamu yalisema kuwa mashtaka hayo yalitengenezwa kwa uongo na Cumpio alitambuliwa kama hasimu wa serikali kwa kazi yake ya uandishi, ambayo ilikosoa polisi na jeshi.

    Waangalizi wanasema kuwa kutajwa huko dhidi ya waandishi wa habari na wanaharakati kuliongezeka chini ya utawala wa Rodrigo Duterte, ambaye aliendesha vita vya kikatili dhidi ya madawa ya kulevya kuanzia 2016 hadi 2022.

    Alhamisi, baada ya miaka sita gerezani bila kesi kuanza, Cumpio alifutiwa mashtaka yanayohusiana na umiliki haramu wa silaha na milipuko, lakini alikutwa na hatia ya kufadhili ugaidi.

    Anakabiliwa na kifungo cha miaka 12 gerezani. Mwenzake waliokuwa wakiishi chimba kimoja, Marielle Domequil, naye alikutwa na hatia na kupewa hukumu sawa na yake.

    "Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo ya hukumu hii, ikizingatiwa kwamba kuna kesi nyingine nyingi, na ningesema, kesi zilizobadilishwa, za kufadhili ugaidi ambazo bado zinaendelea kote nchini," Mwanasheria Josa Deinla, mmoja wa mawakili wa Cumpio, aliiambia BBC.

    Unaweza kusoma;

  14. Mo Salah arejea kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool

    Winga matata wa Liverpool Mohamed Salah hatimaye alirejea kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool na akapiga mechi yake ya kwanza tangu alipotoka kuiwakilisha Misri katika michuano ya soka ya bara la Afrika AFCON.

    Mshambuliaji huyo wa Misri alianzishwa kwenye kikosi cha Liverpool kilichoichabanga Olympic Marseille ya Ufaransa mabao matatu kwa nunge katika mechi ya klabu bingwa ulaya iliyosakatwa uga wa ugenini Velodrome.

    Mashabiki wengi duniani hawakuamini macho yao kumshuhudia sogora huyo wa Liverpool uwanjani ikiwa ishara kamili kumalizika mvutano baina yake na kocha Arne Slot na sasa amerudi kuitumikia Liverpool.

    Katika mtanange huo,Salah alipoteza fursa ya kufunga bao katika dakika ya 83 lakini Liverpool ilicheza vizuri na aliisaidia kushinda kiurahisi huku nyota wa mchezo huo akiwa Dominik Szoboszlai.

    Baadhi ya mashabiki na wachambuzi wa soka kutoka England walihofia kuwa safari ya Mo Salah Liverpool ilifikia mwisho mwezi Disemba baada ya mchezaji huyo kuelezea vyombo vya habari kuwa kuna watu Fulani hawakumtaka kwenye timu hiyo na hivyo walimlaumu yeye kwa matokeo mabovu ya timu wakati huo.

    Hata hivyo, kocha Arne Slot alisema kabla ya mechi hiyo ya jana na hata baada, kuwa amemaliza tofauti zake na Salah na amemrejesha kwenye kikosi cha kwanza kwa ajili ya kutafuta matokeo bora.

    Mo Salah aidha upande wake aliomba radhi kwa wachezaji wenzake wa Liverpool uongozi Pamoja na mashabiki nah atua hiyo inaonekana kufuta mzizi wa fitina baina ya Salah na Liverpool.

    Liverpool inacheza mechi ijayo dhidi ya Bournemouth katika mechi ijayo ya Ligi kuu ya Premier nchini England.

    Pia unaweza kusoma:

  15. Marekani kuwahamisha wafungwa wa Islamic State kutoka Syria hadi Iraq

    Jeshi la Marekani limeanza uhamisho wa hadi wafungwa 7,000 wa kundi la Islamic State (IS) kutoka gerezani kaskazini-mashariki mwa Syria kuelekea Iraq, huku serikali mpya ya Syria ikichukua udhibiti wa maeneo ambayo kwa muda mrefu yalidhibitiwa kwa uhuru na vikosi vya Wakurdi.

    Kamandi ya Kati ya Marekani (US Centcom) imesema tayari imehamisha wapiganaji 150 wa IS kutoka mkoa wa Hassakeh kwenda "eneo salama" nchini Iraq.

    Imesema kuwa hatua hii inalenga kuzuia wafungwa kutoroka na kujiunganisha upya.

    Uhamisho huu unafuatia makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yameweka sehemu kubwa ya kaskazini-mashariki mwa Syria chini ya udhibiti wa Damascus, baada ya Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria vinavyoongozwa na Wakurdi (SDF) kuondoka katika maeneo muhimu, ikiwa ni pamoja na vituo vya wafungwa vinavyoshikilia maelfu ya washukiwa wa IS na familia zao.

    Kundi la haki za binadamu la Reprieve lilionya kwamba wafungwa waliohamishwa hadi Iraq wanaweza kukabiliwa na mateso na kunyongwa na kuihimiza serikali ya Uingereza kubaini kama raia wowote wa Uingereza walikuwa miongoni mwa wale wanaohamishwa.

    Shirika hilo la hisani lilisema linaamini kwamba hakukuwa na zaidi ya wanaume 10 wa Uingereza walioshikiliwa katika magereza, ingawa idadi kamili haikuwa wazi.

    Takribani raia 55 hadi 60 wa Uingereza, wengi wao wakiwa watoto, bado wamefungwa katika kambi na magereza katika eneo hilo, lilisema.

  16. Shambulio la Israel huko Gaza laua waandishi wa habari watatu, kwa mujibu wa maafisa wa uokoaji

    Waandishi wa habari watatu wa Kipalestina wameuawa katika shambulio la Israel katikati mwa Gaza, kwa mujibu wa wahudumu wa uokoaji.

    Shirika la Ulinzi wa Raia la Gaza linaloendeshwa na Hamas lilisema gari lao lilipigwa katika eneo la al-Zahra, na likawataja waliouawa kuwa ni Mohammed Salah Qashta, Anas Ghneim na Abdul Raouf Shaat. Inaelezwa kuwa walikuwa wakifanya kazi kwenye shirika la misaada kutoka Misri.

    Jeshi la Israel lilisema lilishambulia “washukiwa kadhaa waliokuwa wakiendesha droni inayohusishwa na Hamas kwa namna iliyotishia askari wake,” na kuongeza kuwa tukio hilo bado linachunguzwa.

    Watu wengine wanane, wakiwemo watoto wawili, pia waliuawa na mizinga na risasi za Israel katika maeneo mbalimbali ya Gaza siku ya Jumatano, kulingana na wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.

    Takribani Wapalestina 466 wameuawa huko Gaza tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas kuanza tarehe 10 Oktoba, kulingana na wizara ya afya.

    Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake watatu wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na makundi yenye silaha ya Kipalestina katika kipindi hicho hicho.

    Unaweza kusoma;

  17. Nchi saba zaidi zakubali kujiunga na Baraza la Amani la Trump

    Nchi saba, zikiwemo Saudi Arabia, Uturuki na Misri, zimesema zitajiunga na Baraza la Amani la Rais wa Marekani Donald Trump, kulingana na taarifa ya pamoja.

    Nchi hizo zitajiunga na Israel, ambayo tayari ilithibitisha hadharani ushiriki wake mapema.

    Jioni ya Jumatano, Trump alisema kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin pia amekubali kujiunga, lakini Putin alisema nchi yake bado inachunguza mwaliko huo.

    Hapo awali, ilidhaniwa kuwa baraza hilo lililenga kusaidia kumaliza vita vya miaka miwili kati ya Israel na Hamas huko Gaza pamoja na kusimamia ujenzi upya.

    Hata hivyo, rasimu ya katiba iliyopendekezwa haijalitaja eneo la Palestina, na inaonekana kubuniwa ili kuchukua nafasi ya baadhi ya majukumu ya Umoja wa Mataifa (UN).

    Bado haijabainika ni nchi ngapi zimealikwa kujiunga na chombo kipya cha Trump, Canada na Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizoalikwa, lakini bado hazijatoa majibu yao hadharani.

    Hata hivyo, Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain, Albania, Armenia, Azerbaijan, Belarus, Hungary, Kazakhstan, Morocco na Vietnam tayari zimekubali kujiunga.

    Siku ya Jumatano, Vatican pia ilithibitisha kuwa Papa Leo amepokea mwaliko. Akizungumza na waandishi wa habari siku hiyo, Katibu wa Serikali wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, alisema Papa atahitaji muda wa kutafakari kabla ya kuamua iwapo atashiriki.

    Unaweza kusoma;

  18. Trump asema Marekani inatazama uwezekano wa kufikia makubaliano kuhusu Greenland

    Rais Donald Trump amesema Marekani inachunguza uwezekano wa kufikia makubaliano kuhusu Greenland baada ya mazungumzo na NATO, huku akiondoa mipango ya kuweka ushuru kwa washirika wa Ulaya waliopinga mpango wake wa Marekani wa kumiliki kisiwa hicho.

    Kupitia mitandao ya kijamii, Trump alisema kuwa “mkutano wenye mafanikio makubwa” na kiongozi wa NATO ulisababisha kuwepo kwa “mfumo” wa makubaliano yanayoweza kufikiwa kuhusu Greenland na eneo la Arctic, ingawa hakutoa maelezo mengi.

    NATO nayo ilielezea mkutano huo kuwa “wenye tija kubwa” na kusema kuwa majadiliano kuhusu mfumo huo uliotajwa na Trump yatalenga kuhakikisha usalama wa eneo la Arctic.

    Hapo awali, Trump aliliambia Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) huko Davos kwamba hatatumia nguvu za kijeshi, lakini anataka mazungumzo ili kufanikisha umiliki wa eneo hilo.

    Unaweza kusoma;

  19. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu leo