Kiongozi mkuu wa Iran Ayatullah Ali Khamenei asema maadui watapata 'jibu kali'

Marekani na Israel "bila shaka zitapata jibu kali", kiongozi mkuu wa Iran amesema, kufuatia shambulio la Israel dhidi ya Iran wiki moja iliyopita.

Muhtasari

  • Kiongozi mkuu wa Iran asema maadui watapata 'jibu kali'
  • Uingereza: Badenoch aapa kufanya mabadiliko mapya katika chama cha Conservatives baada ya ushindi wa uongozi
  • Duru za ujasusi za Ukraine: Urusi imehamisha maelfu ya wanajeshi kutoka Korea Kaskazini hadi mpaka wa Ukraine
  • Uchaguzi wa Marekani 2024: Je mshahara wa Rais wa Marekani ni kiasi gani?
  • Niliambiwa ni sasa au haitawezekana kamwe - Amorim kuhusu kuhamia Man Utd
  • Vita vya Gaza: Mashambulizi ya Israel yawauwa Wapalestina katika maeneo ya Jabalia na Nuseirat
  • Marekani yaimarisha kikosi chake Mashariki ya Kati, huku vifo vikiongezeka kufuatia mashambulizi ya Israel

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu kwa leo, tukutane tena hapo kesho.

  2. Kiongozi mkuu wa Iran asema maadui watapata 'jibu kali'

    g

    Chanzo cha picha, Handout via Reuters

    Maelezo ya picha, Majibu ya Iran kwa mashambulizi ya Israel yatazidisha hali tete katika Mashariki ya Kati

    Marekani na Israel "bila shaka zitapata jibu kali", kiongozi mkuu wa Iran amesema, kufuatia shambulio la Israel dhidi ya Iran wiki moja iliyopita.

    Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi siku ya Jumamosi kabla ya kuadhimisha mwaka wa 45 tangu kunyakuliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran mwaka 1979.

    Tisho hilo linakuja wakati Iran ikitathmini jinsi ya kujibu mashambulizi ya Israel ya mwezi uliopita, ambapo Iran ilisema iliwauwa wanajeshi wanne , wakati iliposema kuwa yalilenga kulipiza kisasi kwa shambulio la kombora la Iran dhidi ya Israel mapema mwezi Oktoba.

    Shambulio hilo la Iran lilikuja kujibu mauaji ya viongozi wa Hezbollah na Hamas, makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Iran yanayopigana na Israel - na kamanda mkuu wa Iran.

    Khamenei amesema maadui wa Iran, ikiwa ni pamoja na Israel na Marekani, "bila shaka watapata jibu kali kwa kile wanachofanya kwa Iran, watu wa Iran na wapiganaji".

    Kinachojulikana kama "mhimili wa upinzani" wa Iran ni muungano wa makundi yanayoungwa mkono na Tehran ambayo ni pamoja na Hamas huko Gaza, Hezbollah nchini Lebanon, Wahouthi nchini Yemen, na makundi yenye silaha nchini Iraq na Syria. Mengi yametajwa kama mashirika ya kigaidi na baadhi ya mataifa ya Magharibi.

    Israel inasemekana kusababisha uharibifu mkubwa kwa ulinzi wa anga na uwezo wa makombora wa Iran katika shambulio lake la tarehe 26 Oktoba, ingawa Iran haijakubali hilo.

    Unaweza pia kusoma:

  3. Uingereza: Badenoch aapa kufanya mabadiliko mapya katika chama cha Conservatives baada ya ushindi wa uongozi

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Kemi Badenoch amekuwa kiongozi mpya wa Conservatives na mwanamke wa kwanza mweusi kuongoza chama kikuu cha kisiasa cha Uingereza Jumamosi, baada ya kushinda mashindano ya uongozi kwa ahadi ya kurudisha chama katika kanuni zake za msingi.

    Benoch mwenye umri wa miaka 44, anachukua nafasi ya waziri mkuu wa zamani Rishi Sunak na ameahidi kukiongoza chama hicho katika kipindi cha upya baada ya kushindwa kwake katika uchaguzi wa Julai nchini Uingereza, akisema kimegeuka kuwa kituo cha kisiasa kwa "kutawala kutoka kushoto".

    Anachukua nafasi kutoka kwa Rishi Sunak, ambaye aliongoza Conservatives kushindwa vibaya zaidi katika uchaguzi wa Julai.

    Katika hotuba yake ya ushindi, aliwaambia wanachama wa chama kuwa ni "wakati wa kuanza kazi" na "wakati wa mpya".

    Badenoch, ambaye alilelewa nchini Nigeria, ni mwanamke wa kwanza mweusi kuongoza chama kikuu cha kisiasa nchini Uingereza.

    Yeye ni kiongozi wa sita wa Conservatives katika chini ya miaka minane na nusu na anakabiliwa na changamoto ya kuunganisha chama kilichovunjika.

  4. Duru za ujasusi za Ukraine: Urusi imehamisha maelfu ya wanajeshi kutoka Korea Kaskazini hadi mpaka wa Ukraine

    h

    Chanzo cha picha, ED Jones/AFP

    Maelezo ya picha, Urusi imekuwa ikikanusha kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wanajiandaa kwa mapigano nchini Ukraine (picha ya maktaba)

    Kurugenzi Kuu ya Ujasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilisema kuwa katika wiki iliyopita ya Oktoba, Urusi ilihamisha zaidi ya wanajeshi 7,000 kutoka Korea Kaskazini hadi maeneo yaliyo karibu na mpaka wa Ukraine.

    Kwa mujibu wa kurugenzi hiyo wanajeshi hao wa Korea kaskazini walisafirishwa kwa ndege 28 za kijeshi, na watakuwa na silaha za makombora ya 60-mm, na bunduki aina ya machine gun zenye uwezo mkubwa wa kulenga shabaha

    Siku ya Jumatano, Korea Kusini ilisema wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wamewasili nchini Urusi, na karibu 3,000 kati yao tayari wako katika sehemu ya magharibi ya nchi hiyo wakipatiwa mafunzo.

    Kwa mujibu wa Seoul, baadhi ya wanajeshi wanaweza kupelekwa katika mkoa wa Kursk, na wengine wanaweza kwenda Donbass.

    Mwakilishi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa, Sergei Kyslytsya, alisema kuwa Korea kaskazini inapanga kuunda angalau vitengo vitano vya wanajeshi 2,000-3,000 kila mmoja, ambavyo vitajiunga na vitengo vya Urusi kuficha uwepo wao na watakuwa na nyaraka na sare za Urusi.

    Rais wa Urusi Vladimir Putin hivi karibuni hakukana kutuma wanajeshi wake Korea Kaskazini, akisema kuwa ni Moscow na Pyongyang pekee ndizo zinazopaswa kuamua ni kwa namna gani zinashirikiana kijeshi.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  5. Uchaguzi wa Marekani 2024: Je mshahara wa Rais wa Marekani ni kiasi gani?

    g

    Kuanzia msimu huu wa uchaguzi, mshahara wa Rais wa Merika utaongezwa

    Mara nyingi watu hufikiri kwamba Rais wa Marekani anapata fedha nyingi katika mfumo wa mshahara na posho.

    Hakuna makosa katika fikra hii kwa sababu rais wa Marekani ndiye kiongozi wa moja ya nchi kubwa na yenye nguvu duniani.

    Lakini sivyo ilivyo hata kidogo.

    Sababu ni kwamba kila rais anayeongoza Marekani ameundwa kuwa mtumishi wa umma, wanalipwa mshahara na kodi ambazo wananchi wengine hulipa.

    Rais Joe Biden ambaye yuko mamlakani sasa anapokea dola 400,000 kwa mwaka.

    Lakini sio pesa ambazo rais ajaye - Kamala au Trump - atapokea.

    Hili si jambo la kushangaza kwa sababu ni muda mrefu umepita tangu mshahara wa rais kubadilishwa.

    Ikiwa Kamala Harris atashinda, rekodi zinaonyesha atapokea $235,100 zaidi juu ya mshahara wake kama makamu wa rais.

    Kwa miaka minne madarakani, Donald Trump hajapokea mshahara wa urais. Badala yake, anaendelea kuielekeza kwa idara zingine za serikali kila baada ya miezi mitatu.

    Kulingana na Katibu wa Jimbo la Kazi za Umma, Trump aliamuru kuwekeza pesa katika uwanja wa huduma ya afya na mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona mnamo 2020.

    Mshahara na Bajeti ya Rais wa Marekani

    Mshahara wa wastani wa kila mwaka - $400,000

    Gharama zingine kama nguo - $50,000

    Ada ya matengenezo ya wageni - $19,000

    Pesa hizo hutumika kulipa maafisa na wafanyikazi katika Ikulu ya White House - kama vile watunza bustani.

    Pia huduma ya afya ya rais ni bure, usafiri wake pia ni bure kwa gari la serikali, na ndege.

    Na anapata $100,000 kwa mwaka, ambayo ni bila kodi.

    Nyakati ambazo mshahara wa rais ulibadilishwa

    Tangu 1789, wakati George Washington alipokuwa rais, mshahara wa rais wa Marekani umebadilishwa mara sita tu.

    Hapo awali, rais alipokea $25,000 kwa mwezi. Lakini makadirio ya thamani ya pesa sasa itakuwa dola 895,700.

    Sababu inayofanya posho zipewe rais ni kuwazuia kufuja mali ya taifa.

    Mara ya mwisho mshahara wa rais kubadilishwa ilikuwa mwaka 2001, wakati wabunge walipouongeza mara mbili kutoka $200,000 hadi $400,000.

    • 1789: $25,000
    • 1873: $50,000
    • 1909: $75,000
    • 1949: $100,000
    • 1969: $200,000
    • 2001: $400,000

    Tukizingatia mshahara pekee, mapato ya rais ni chini ya wafanyakazi wanaolipwa zaidi nchini Marekani.

    Hata hivyo, ataendelea kupokea takriban $244,000 kila mwaka baada ya kujiuzulu.

    Vile vile ataendelea kupewa walinzi, huduma za afya bure na kumpeleka popote anapotaka bure.

    Unaweza pia kusoma:

  6. Niliambiwa ni sasa au haitawezekana kamwe - Amorim kuhusu kuhamia Man Utd

    g

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Ruben Amorim alishangiliwa na mashabiki wa Sporting kabla ya ushindi wa Ijumaa wa nyumbani wa 5-1 dhidi ya Estrela da Amadora

    Ruben Amorim anasema alitaka kuchukua kibarua cha umeneja wa Manchester United mwishoni mwa msimu huu lakini alikubali uteuzi wa katikati ya msimu baada ya kuambiwa ni achukue kibarua hicho "sasa au hatawahi kamwe".

    Amorim, 39, alithibitishwa kuwa kocha mkuu mpya wa Manchester United siku ya Ijumaa na atakamilisha uhamisho wake kwenda Old Trafford kutoka klabu ya Lisbon ya Sporting mnamo 11 Novemba.

    Akizungumza baada ya mechi ya kwanza ya Sporting tangu uteuzi huo – ambapo walipata ushindi wa 5-1 wa ligi dhidi ya Estrela siku ya Ijumaa ambao uliimarisha mwanzo wao mzuri baada ya mechi 10 - Amorim alielezea ombi lake pekee kufuatia ombi la United ambalo lilikuwa ni kuona shindano la sasa linafaulu, jambo ambalo tayari alikuwa amemjulisha rais wa klabu hiyo kwamba huo ungekuwa mwisho wake.

    Lakini kocha huyo wa Ureno aliambiwa hilo halingewezekana kwani klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza inatafutakocha mbadala mara moja wa Erik ten Hag, ambaye alitimuliwa Jumatatu.

  7. Vita vya Gaza: Mashambulizi ya Israel yawauwa Wapalestina katika maeneo ya Jabalia na Nuseirat

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wapalestina waliojeruhiwa wakiwa wamelala kwenye vitanda na sakafu katika hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Ukanda wa Gaza

    Mjini Gaza, Wapalestina kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa alfajiri ya Jumamosi katika shambulio la Israel la mji wa Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kambi ya Nuseirat.

    Vyanzo vya habari vya Palestina vimesema kuwa jeshi la anga la Israel lilishambulia shule ya Al-Rafei, ambayo inawahifadhi wakimbizi waliokimbia makazi yao katika mji wa Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kuwaua Wapalestina kadhaa.

    Wapalestina watatu, wakiwemo watoto wawili, pia waliuawa katika shambulio la bomu lililolenga nyumba moja katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.

    Wapalestina watano wamejeruhiwa baada ya mashambulizi mapya ya makombora ya Israel katika kambi ya Nuseirat kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, na katika mashambulizi ya makombora yaliyolenga nyumba moja katika mji wa Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

    Vikosi vya Israel vimeendelea kushambulia Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, 2023 na kuwaua zaidi ya Wapalestina 43,000 na kuwajeruhi wengine 102,000, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, kwa mujibu wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza.

    Unaweza pia kusoma:

  8. Marekani yaimarisha kikosi chake Mashariki ya Kati , huku vifo vikiongezeka kufuatia mashambulizi ya Israel

    h

    Chanzo cha picha, Reuters/Navy DOD

    Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imesema Jumamosi kuwa imeagiza kupelekwa kwa makombora ya ziada ya masafa marefu, vikosi vya wapiganaji, ndege za mafuta na makombora kadhaa za masafa marefu katika eneo la Mashariki ya Kati.

    "Kwa mujibu wa ahadi zetu za kuwalinda raia wa Marekani na vikosi vya Mashariki ya Kati, kuilinda Israel, na kupunguza mvutano kupitia kujizuia na diplomasia, Waziri wa Ulinzi ameamuru kupelekwa kwa makombora ya ziada ya masafa marefu, kikosi cha wapiganaji, na ndege kadhaa za kivita za Marekani aina ya B-52 za masafa marefu katika eneo hilo," taarifa ya Pentagon imesema.

    Taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Vikosi hivi vitaanza kuwasili katika miezi ijayo wakati kundi la mashambulizi la USS Abraham Lincoln likijiandaa kuondoka."

    Pia aliongeza kuwa kupelekwa kwa makombora hayo "kunatokana na uamuzi wa hivi karibuni wa kupeleka mfumo wa ulinzi wa makombora wa Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) nchini Israel pamoja na msimamo unaoendelea wa kitengo cha ulinzi cha Jeshi la majini katika Mashariki mwa Mediterranean."

    Unaweza pia kusoma:

  9. Hujambo na karibu kwa matangazo haya ya mubashara ikiwa leo ni Jumamosi 02.11.2024