Mambo ya kufanya kama humpendi mwajiri wako

Chanzo cha picha, Getty Images
''Unakuwa huwezi kufanya kazi kwenye kiwango kinachotakiwa, unakuwa hauna furaha, na hautaki kabisa ujitume zaidi.''
''Niliipenda sana kazi yangu lakini kama kuna bosi ambaye anachukia unachokifanya au anajaribu kukushusha thamani, inakuvunja moyo sana'' amesema Craig.
Mara ya kwanza alimpenda sana meneja wake lakini alianza kumchukia pale alipomuona anamgombeza msaidizi wake kwenye simu.

Na kuanzia hapo mambo yaliendelea kuwa mabaya. Alikuwa anamgombeza sana ofisini na kumdhihaki kwenye mkusanyiko wa watu.
''Kwanza yalianza maneno ya dharau'' ameeleza.
''Kidogo kidogo vitu vikaanza kubadilika kufikia kiasi cha kusema maneno ya shari, uadui na kujiona bora kuliko wengine.''
Ameongeza ''ilikuwa inaumiza sana kwenda kazini kila siku. Mahusinano yako na watu wa karibu yanakuwa yanaharibika kabisa.''
''Ukifanya kazi na bosi mbaya , mtu ambaye haoni thamani yako, inakufanya na wewe ujione mtu wa kiwango cha chini sana.
Unakuwa hauwezi kufanya kazi kwenye kiwango kinachotakiwa, unakuwa hauna furaha, na hautaki kabisa ujitume zaidi.''

Chanzo cha picha, Getty Images
Tatizo hili kwa Craig sio la kushangaza.
Uchunguzi uliofanywa na kampuni ya '' Chartered Institte of personnel ad Development (CIPD) umeonesha asilimia 7 ya watu wanasema hawaelewani na mabosi wao.
Ben Willmott ni kiongozi wa sheria za umma amesema katika kesi nyingi wafanyakazi huwalalamikia mabosi wao kwa sababu ya kupewa kazi nyingi au ukosefu wa haki wa muda mrefu.
''Ni mara nyingi sana, vitu vidogo vidogo ndivyo vinasababisha matatizo'' ameendelea kusema.
Kuepuka haya anawashauri waajiriwa wawe wazi na mabosi wao kuhusu tatizo lolote, kama wakijisikia huru kufanya hivyo.
''bosi anaweza kuwa hajui jinsi gani tabia yake inawaathiri watu wengine na hivyo kumwambia inaweza kuwa kitendo cha kumfanya abadilishe matendo yake,'' amesema Bw Willmott.
Lakini, anapelekea kwenye matatizo makubwa zaidi kama vile kudhihaki na kumuabisha mtu, ambazo zinatakiwa kushughulikiwa na afisa (HR) ama meneja mwingine.

Chanzo cha picha, Damian Beelay
Hata hivyo Damian Beeley ambaye ni mtaalamu wa uhusiano wa umma, aliwahi kuwa na matatizo na bosi wake, anasema kuwa kama jambo lina uhusiano binafsi basi ni bora uache kazi na kutafuta sehemu nyingine.
Lakini anasema kuwa ni tatizo ambalo anaweza kuwa nalo meneja kuliko mwajiri.
''Kama meneja kuna watu hawatokupenda lakini inabidi ufikirie kwanini hawakupendi,'' amesema.
''lakini kama wewe ni muajiriwa na unamchukia bosi wako , hiyo ni hali mbaya sana kuwa nayo''.












