Marekani imeiwekea vikwazo Uturuki kwa kuwashambulia Wakurdi Syria

Maelezo ya video, Vikosi vya serikali ya Syria vilivyoingia mji wa Ain Issa

Marekani imeiwekea vikwazo wizara za Uturuki na maafisa wa serikali kujibu hatua ya nchi hiyo kuingilia kijeshi eneo la Kaskazini mwa Syria.

Rais Donald Trump pia amempigia simu mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kutaka kufikiwa kwa makubaliano ,Makamu wa rais Mike Pence amesema.

Bw. Pence amesema atazuru eneo hilo "haraka iwezekanavyo".

Hatua hiyo inakuja baada ya Marekani kuondoa wanajeshi wake kutoka eneo hilo ambayo baadhi ya watu wanasema iliipatia Uturuki "ishara ya kuenedelea mbele" na mpango wake .

Vikosi vya Marekani vimekuwa vikipambana kwa ushirikiano na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi la Islamic State (IS).

Mwanamke wa Kikurdi nchini Syria akilia wakati wa mazishi ya wapiganaji watano wa Syrian Democratic Forces mjini Ras al-Ain

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwanamke wa Kikurdi nchini Syria akilia wakati wa mazishi ya wapiganaji watano wa Syrian Democratic Forces mjini Ras al-Ain

Oparesheni ya Uturuki, ambayo ilianza wiki iliyopita, inalenga kukabili vikosi vya mapoja vya Syria (SDF) kutoka eneo hilo la mpakani.

Uturuki inaamini SDF ni kikosi cha magaidi.

Vikosi vya Uturuki pia vimebuni kile ambacho serikali yao inataja kuwa "eneo salama" la kuwapa makazi wakimbizi milioni mbili wa Syria ambao wamepewa hifadhi katika nchi hiyo.

Wengi wao sio wakurdi na wakosoaji wanaonya kuwa hatua hiyo huenda ikasababisha jamii ya wakurdi katika eneo hilo kulengwa kimakosa.

Wametaja hatua ya Marekani kujiondoa iliyosababisha Uturuki kuingia eneo hilo kama "usalati".

Kuna hofu kuwa hatua ya kuwahangaisha wenyeji katika eneo hilo huenda ikafufua tenga kundi IS, kwasababu maelfu ya jamaa za wapiganaji hao wanazuiliwa Kaskazini mwa Syria.

Mamia kati yao wanasemekana kutoroka katika moja ya kambi waliokwa wakizuiliwa.

Baada ya makabiliano makali, vikosi hivyo vinavyoongozwa na Wakurdi siku ya Jumapili vilitangaza kufikia makubaliano kati yao na serikali ya Syria kuomba msaada wa kijeshi ili kudhibiti mashambulizi kutoka kwa vikosi vya Uturuki.

Map of northern Syria
Presentational white space

Vikwazo hivyo ni vipi?

Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin alitangaza vikwazo, ambavyo vililenga wizara mbiili na maafisa wakuu watatu wa serikali, mjini Washington DC Jumatatu jioni.

Hatua ilichukuliwa dhidi ya wizara za Uturuki za ulinzi na kawi, pamoja na mawaziri wa ulinzi , kawi na ulalama wa ndani, Marekani ilisema katika taarifa.

Hatua hiyo inazulia mali zao nchini Marekani na kupiga marufuku kujiuhusisha kwao na shughuli zozote zinazowahusisha wao na mfumo wa kifedha wa Marekani.

"Hatua ya Uturuki inahatarisha maisha ya raia wasiokuwa na hatia na kusababisha vurugu katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kuhujumu kampeini ya kusinda ISIS [Islamic State]," taarifa hiyo iliongeza.

Rais wa Marekani Donald Trump anakabiliwa na shinikizo kubwa la kutaka iichukulie hatua mshirika wake wa katika Nato.

Mike Pence na Steven Mnuchin wakihutubia wanahabari nje ya Ikulu ya White House

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence anasisitiza kuwa nchi hiyo "haikuipatia Uturuki Ishara ya kuivamia Syria"

Katika taarifa iliyowekwa katika mtando wa Twitter, rais Trump pia alisema ataongezea kodi vyoma kutoka Uturuki kwa 50% na "kukomesha mara moja" mashauriano yanayohusiana na ''mkataba wa kibiashara wa dola bilioni 100" na Uturuki.

"Sisi Marekani na washirika wetu tumekomboa kwa asilimia 100 maeneo yaliyokuwa yanakaliwa na wanamgambo wa ISIS," taarifa hiyo ilisema. "Uturiki haistahili kuweka hatarini hatua iliofikiwa katika mapambano hayo."

Mapema Jumatatu, nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya EU ziliahidi kusitisha mapango wa kuiuzia silaha Uturuki, hali ambayo huenda ikageuka kuwa vikwazo kamili vya kisilaha dhidi ya nchi hiyo.

Ikijibu tamko hilo, Uturuki imesema itachunguza ushirikiano wake na EU kutokana na tabia yake "isiyo halali na ya upendeleo".

Presentational grey line

Ni nini kinachoendelea Syria?

Baada ya kufikia makubaliano na vikosi vinavyoongozwa na wapiganaji wa Kikurdi, jeshi la Syria lilianza kufanya mashambulizi kuelea mpakani siku ya Jumatatu.

Vyombo vya habari vya Syria vilitangaza kuwa vikosi vya serikali vimeingia katika mji wa Manbij, eneo ambalo Uturuki inataka kubuni "eneo salama".

Wanajeshi wa Uturuki na wapiganaji wanaopinga serikali ya Uturuki walianza kukusanyika karibu na mji huo.

Mkataba huo ulionekana kuimarisha utawala wa rais wa Syria Bashar al-Assad kwani ulimaanisha vikosi vyake vitarejea katika maeneo ya kaskazini mashariki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012, baada ya kujiondoa kwao katika maeneo mengine ili kukabiliana na waasi kutoa nafasi kwa wanamgambo wa Kikurdi kuchukua udhibiti wa eneo hilo.

Uturuki na washirika wake wakiendelea na mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi wanaoshikilia mji wa mpakani kaskazini mashariki mwa Syria

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Uturuki na washirika wake wakiendelea na mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi wanaoshikilia mji wa mpakani kaskazini mashariki mwa Syria

Licha ya kupinga jaribio lao la kutaka kujitenga na kujitawala, Bw. Assad hakupigania kukomboa eneo hilo, hasa baada ya wapiganaji wa Kikurdi kuwa washirika wake katika vikosi vya muungano dhidi ya IS kwa ushirikiano na vikosi vya Marekani.

Kando na kupiga vita IS, Wakurdi walikuwa kiungo muhimu kwa Marekani katika hatua ya kudhibiti ushawishi wa mahasimu wao Urusi na Iran katika mzozo wa Syria.

Kwa sasa, vikosi vya Syria havitapelekwa katika miji ya Tal Abyad na Ras al-Ain, ambako Uturuki imeelekeza juhudi zake.

Rais Erdogan wa Uturuki anasisitiza kuwa oparesheni hiyo itaendelea hadi pale inchi hiyo itakapofikia "malengo yake" licha ya kuingiliwa na vikosi vya serikali ya Syria.

"Mungu akitujaalia tutakomboa maeneo yanayokaribia mpaka wetu kutoka Manbij hadi Iraq na kuhakikisha kwamba katika awamu ya kwanza, watu milioni moja wanarudi makwao na katika awamu ya pili wakimbizi milioni mbili wa Syria wanarejea nyumbani kwa hiari," alisema katika hotuba yake kupitia Televisheni siku ya Jumanne .

Umoja wa Mataifa unasema watu takribani 160,000 wametoroka makazi yao lakini shirika kutetea haki la Syrian Observatory (SOHR) linasema idadi hiyo huenda ni zaidi 250,000 huku likiripoti vifo vya raia 70.

Shirika hilo lillilo na makao yake nchini Uingereza pia linasema wanachama 135 wa SDF wameuawa katika oparesheni hiyo kufikia sasapamoja na wapihanaji 122 wanaounga mkono serikali ya Uturuki na wanajeshi wanane wa Uturuki.

Shirika la habari la Uturiki, Anadolu limeripori vifo vya raia 18 katika mpaka wa kusini mwa Uturuki.