Je, wafuasi wa Trump wanachochea chuki dhidi ya vyombo vya habari?

Chanzo cha picha, Getty Images
Vyombo vya habari nchini Marekani imehoji kuhusu video ya kudhihaki inayomuonyesha rais wa Marekani akiwakashifu wapinzani wake.
Mwandishi wa ikulu ya Marekani anadai kushangazwa na video hiyo na kumtaka Trump kutoa ufafanuzi wa kukanusha kuwa video hiyo sio ya kweli.
Hii ilionekana katika shughuli iliyokuwa imeandaliwa na wanaomuunga mkono Trump. Waandaaji wanasema kuwa video hiyo ilikuwa sehemu ya maonyesho.
Kampeni za uchaguzi wa urais kwa Trump kwa mwaka 2020 zimeingia doa katika hilo.
Msemaji wa kampeni hizo bwana Tim Murtaugh ameiambia BBC kuwa "video hiyo haikutengenezwa wana kampeni na hatuwezi kuhamasisha chuki ."
Siku ya jumatatu, msemaji wa ikulu ya Marekani Stephanie Grisham aliandika katika kurasa ya Twitter kuwa bwana Trump hajaiona video hiyo bado.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

"Lakini kutokana na kila kitu kilichosemwa, anailaani vikali video hiyo", alisema msemaji huyo .
Ingawa vyombo vya habari vya Marekani vinamtaka rais Trump mwenyewe ukanusha kuhusika katika video hiyo ambayo ilichezwa katika risoti ya Miami huko Florida wiki iliyopita.
"Wamarekani wote wanapaswa kulaani vikali uenezwaji huu wa chuki dhidi ya waandishi wa habari na wagombea wa urais," alisema Jonathan Karl, Rais wa jumuiya ya waandishi wa ikulu. "Tayari tumemwambia rais kuwa mbinu anazotumia zinaweza kuhamasisha vurugu."
Wanaomuunga mkono Trump wanasema kuwa video hiyo iliyoangaliwa na watu wengi iliandaliwa na timu inayojulikana kama 'TheGeekz'.
Jumuiya hiyo inayojulikana kama 'MemeWorld' wanasema katika maelezo yao kuwa hawakuhamasisha chuki.
"Hakuna mtu mwenye akili yake anayeweza kudhani kuwa video hii inataka kuhamasisha chuki dhidi ya vyombo vya habari".
Hii ni video gani?
Bwana Trump ametumika kama mwanaume ambaye anaingia kanisani na kuua watu ndani ya kanisa, hiyo ni taarifa ya uongo.
Vichwa vya watu wanaouliwa zimefunikwa na logo za mashirika ya habari kama vile BBC , CNN na wapinzani wake kama Barack Obama na Hillary Clinton.
Video hiyo imechukua sehemu ya filamu ya Kingsman ya mwaka 2014.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2

Mtoto wa rais Donald Trump na waziri wa habari wa zamani Sarah Huckabee Sanders walikuwa wamejipanga kuongea katika shughuli hiyo.
"Nilikuwa sifahamu chochote kuhusu video yeyote na wala siungi mkono harakati zozote zinazo zinazochochea vurugu," Bi Sanders aliiambia gazeti la New york Times.
Mwenyekiti wa chama cha Republican bi. Ronna McDaniel amelaani video hiyo kwenye kurasa ya Twitter .
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3

CNN ilitoa maelezo kuhusu jambo hilo said in a statement on Sunday: "Inasikitisha sana kuwa hii sio mara ya kwanza kwa wafuasi wa rais Trump kuhamasisha vurugu dhidi ya vyombo vya habari na kuona kuwa ni jambo la kuburudisha, huku ni kitu kibaya sana.
Wakati wa kampeni za mwaka 2016, Trump alikuwa anadai mara kwa mara kuwa anavishutumu vyombo vya habari kwa habari za uongo na kueleza jinsi vyombo vya habari kama miongoni mwa adui zake.
Hivi karibuni , Trump alimvamia mpinzani wake katika vyombo vya habari kwa madai ya rushwa.
Video inayofanana na video ile Trump aliweka kwenye kurasa yake mwaka 2017.

Chanzo cha picha, Twitter