Maelezo ya picha, The supermoon rose behind the dome of the Basilica of Our Lady of Mount Carmel in Valletta, Malta
Watazamaji nyota kote ulimwenguni walipata fursa ya kujionea Mwezi mpevu na mkubwa kuliko kawaida Jumanne usiku.
Mwezi huu mpevu, unaoitwa Mwezi wa Sturgeon, uliangaza anga la usiku ulipopaa juu ya upeo wa macho muda mfupi baada ya jua kutua.
Ni mwezi wa kwanza kati ya miandamo miwili ya mwezi huu - mwezi mpevu ujao utaonekana tarehe 30 Agosti utaitwa Mwezi wa Bluu ukiwa ni mwezi mpevu wa pili kuonekana katika mwezi mmoja wa kalenda.
Hizi ni baadhi ya picha bora za mwezi mpevu wa Jumanne kutoka kote duniani:
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mwezi mpevu wa Jumanne uliopewa jina la ongezeko la samaki aina ya sturgeon katika maziwa ya Amerika Kaskazini wakati huu wa mwaka, unaangaza juu ya majengo huko Pristina, Kosovo.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Na hapa ulipigwa picha huko Nicosia, Cyprus, ukiangaza anga la usiku nyuma ya Mnara wa Kumbusho wa Uhuru.
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mwezi huo mkubwa pia ulionekana nyuma ya mnara wa kudhibiti usafiri wa anga kwenye Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion, karibu na Tel Aviv huko Israeli.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Unaonekana hapa ikiwa imelingana kikamilifu na mnara wa TV katika Jiji la Huai'an, jimbo la Jiangsu, China
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mwezi mpevu unaonekana juu ya Mnara wa Galata huko Istanbul, Uturuki
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Iling'aa sana huku anga ya usiku ikizidi kuwa nyeusi juu ya Msikiti wa Grand Camlica huko Istanbul
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Pia ilionekana hapa ukiangaza juu ya eneo la biashara la Cuatro Torres huko Madrid, Uhispania