Lady Evelyn Cobold - Kwa nini mahujaji Waislamu wanatembelea kaburi lake la Scotland?

Ni katikati ya asubuhi katika nyanda za juu kaskazini-magharibi mwa Scotland na magari yanaanza kuingia kwenye mmaegesho ya magari mmsitu ulio karibu na A890 huko Glen Carron.

Siku inatabiriwa kuwa ya mvua, lakini kuna kipindi kifupi cha jua huku kundi la watembea kwa miguu 20 wakijiandaa kwa safari ya kilomita 10 (maili 6.2) kuelekea Gleann Fhiodhaig huko Wester Ross.

Ni hali inayoshuhudiwa katika mamia ya maegesho ya magari kote Scotland kila wikendi, lakini kundi hili la wanaotembea kwa miguu miguu pia ni la mahujaji - waongofu Waislamu ambao wanapanga kuzuru kaburi la mwana mfalme wa Victoria.

Walisafiri kutoka Edinburgh, Liverpool, Leicester na zaidi kwa heshima ya Lady Evelyn Cobbold - ambaye alidhaniwa kuwa mwanamke wa kwanza Muislamu mzaliwa wa Uingereza kwenda Macca kuhiji.

Sherehe hiyo ya kidini ilipangwa na Wakfu wa Waongofuwa Kiislamu, shirika la linalotoa msaada kwa waumini wapya wa dini ya Kiislamu nchini Uingereza.

Mwanzilishi Batool Al-Toma, mwenyewe ni mwongofu kutoka Ireland, anawaalika kundi kuanza safari yao kuelekea milimani.

"Tangu niliposikia kuhusu Lady Evelyn, Nimevutiwa na hadithi yake. Alikuwa mwanamke wa mkakamavu ambaye hakukubali kutengwa kwa sababu tu alikuwa mwanamke," Bi Al-Toma anasema.

Hata kabla hawajafika mbali katika matembezi ya mvua ikaanza kunyesha.

Huku upepo ukivuma na mvua ikiendelea kuwapiga baadhi yao walianza kutafakari safari ya mwisho ya Lady Evelyn kupanda mlima Glen hadi mahali alipochaguliwa kuzikwa.

Alifariki Januari 1963 wakati wa msimu wa baridi na alizikwa katika eneo lililotengwa kando ya mlima katika mtaa wake wa Glencarron.

Mpiga firimbi wa pekee, "aliyetetemeka kutokana na baridi", aliimba wimbo wa Maombolezo ya MacCrimmon na Imam kutoka Woking, Surrey, alifanya ibada ya mazishi, kulingana namaelezo yaliyochapishwa kwenye tovuti ya Inverness Mosque.

Kiungo cha Working bado kipo, huku mwakilishi kutoka msikiti wa mji akijiunga na matembezi haya kwenye kaburi lake karibu miaka 60 baadaye.

Lady Evelyn, ambaye ni alizaliwa Edinburgh mwishoni mwa miaka ya 1800, aliishi maisha yake ya utotoni kati ya ya Scotland na Afrika Kaskazini.

Wakati huko ndipo alipoonyeshwa Uislamu kwa mara ya kwanza, akitembelea misikiti na marafiki zake wa Algeria.

"Bila kujua nilikuwa Muislamu moyoni," aliandika baadaye.

Haijabainika ni lini hasa aliposilimu lakini nafasi ya kukutana na Papa alipokuwa akitembelea Roma ilionekana kuthibitisha imani yake.

"Papa Mtakatifu aliposema na ghafla kwa kuniuliza kama mimi ni Mkatoliki nilisita kwa muda kisha nikajibu kuwa mimi ni Muislamu," alisema.

"Ukweli ni kwamba wakati huo nilikuwa na mawazo kuhusu Uislamu kwa miaka mingi."

Lady Evelyn alipewa jina la Zainab na hatimaye akaenda kuhiji Makka akiwa na miaka 65.

Mmoja wa Waumini waliosilimu akitoa heshima kwa Bi Zainab ni Yvonne Ridley, anayeishi katika Mipaka ya Uskoti.

Ilikuwa ni uzoefu wake wa kufanya kazi kama mwandishi wa habari nchini Afghanistan na kutekwa na Taliban mwaka 2001 ambayo ilimpelekea kusilimu.

"Uongofu wangu ulichochewa kwa njia nyingi na kukamatwa kwangu na kuwekwa kizuizini mikononi mwa Taliban. Uzoefu huo uliniweka kwenye njia ambayo ilianza kama zoezi la kitaaluma lakini ilinipeleka kwenye safari ya kiroho," anasema.

Katika kitabu chake, In the Hands of the Taliban, Bi Ridley alisema alishangazwa na heshima na uungwana ambao wanaume wa Taliban walikuwa wamemuonyesha.

Wakati wa kifungo chake aliahidi kusoma Quran na alifanya hivyo baada ya kuachiliwa.

Bi Ridley alifahamu kuhusu Lady Evelyn kutoka kwa Bi Al-Toma walipokuwa Uturuki.

"Nilianza kusoma zaidi kuhusu mwanamke huyu wa ajabu wa Scotland, kwa hivyo mimi na Batool tuliamua tupate kikundi cha watu waliosilimu na kutoka nje na kuhiji kwenye kaburi lake," anasema.

Baada ya masaa matatu ya safari ya baridi na yenye unyevunyevu, mahujaji hao hupumzika kwa muda huku kiongozi wao Ismail Hewitt, akiwa amevalia sanda yake, anasonga mbele zaidi kutafuta mahali pa kupumzika pa Lady Evelyn.

Roho huinuliwa anaporudi nyuma kutoka mbali, akiashiria kwamba yuko mbele, njia fupi ya kupanda kilima.

Wote wanapanda juu kabla ya kukusanyika kwenye kaburi na kupiga magoti

Kila mmoja wao anatoa heshima zake kabla ya kuungana kwa maombi. Ni wakati uliojawa na hisa, baadhi ya wanachama wa kundi hilo wanabubujikwa na machozi.

Bi Al-Toma anakamilisha sherehe kwa kusoma sehemu ya kitabu cha Lady Evelyn, akitafakari safari yake ya kwenda kuhiji Makka.

Kupitia tukio hilo, nahisi ulimwengu mpya wa kushangaza umefichuliwa."

Baada ya kutembea kurudi barabarani, wasafiri walikaribishwa katika Msikiti wa Inverness kwa chakula na kupata nafasi ya kutafakari kuhusu ziara yao.

Bi Ridley anasema alichoshwa na matembezi lakini alihisi dua alizofanya kando ya kaburi "zilimjenga kiroho".

"Kulikuwa na paa ambaye alionekana kwenye kilima juu ya kaburi lake ambaye alikuwa ishara na kusonga," anasema.

"Huyu alikuwa ni mwanamke ambaye moyo wake ulikuwa katika Nyanda za Juu, lakini pia alikuwa amezama sana katika Uislamu."

Bi Al-Toma anakubali kwamba Lady Evelyn alikuwa kielelezo cha jinsi waongofu wapya bado wangeweza kukumbatia utambulisho wao na utamaduni wao.

"Yeye ni muhimu sana kwa waongofu hapa," anaongeza.

"Nina furaha kuwa nimesoma kitabu chake na kufanya matembezi haya huku nikistaajabia ujasiri wake, ushujaa na hali ya kusisimua. Alikuwa mvumbuzi wa kweli."