Vita vya Ukraine: Ushahidi wa matumizi makubwa ya mabomu yenye milipuko ya kutapakaa huko Kharkiv

Distinctive marks from a cluster munition in the roof of a car next to a playground in Kharkiv (Joel Gunter/BBC)
Maelezo ya picha, Alama tofauti kwenye paa la gari kutokana na bomu lenye mlipuko wa kutapakaa karibu na uwanja wa michezo huko Kharkiv (Joel Gunter/BBC)

Urusi imewaua mamia ya raia katika mji wa kaskazini-mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv kwa kurusha makombora kiholela na mabomu cluster yenye milipuko ya kutapakaa yaliyopigwa marufuku, kulingana na utafiti mpya wa Amnesty International.

Amnesty ilisema imepata ushahidi wa vikosi vya Urusi mara kwa mara kutumia mabomu mabomu aina ya 9N210/9N235, pamoja na silaha ''zinazotawanyika'' - roketi zinazorusha mabomu madogo madogo ambayo hulipuka baadaye kwa muda uliowekwa.

BBC ilitembelea maeneo matano tofauti yaliyoathirika katika vitongoji vya makazi huko Kharkiv na kuona ushahidi wa athari ya kipekee inayohusishwa na mabomu ya kutapakaa.

Tulionyesha picha kutoka kwenye eneo kwa wataalam watatu wa silaha, ambao wote walisema athari zililingana na silaha za utata.

''Athari hizo ni kutoka kwa mabomu ya yenye kutapakaa, ni sahihi kabisa,'' alisema Mark Hizney, mtafiti mkuu katika kitengo cha silaha cha Human Rights Watch.

''Na katika picha moja unaweza kuona mabaki kutoka kwa moja ya silaha zilizotumika,'' alisema.

Kanda za CCTV zilizopitishwa kwa BBC na mkazi katika moja ya tovuti zilionyesha milipuko iliyofuatana - ''kiashirio kikubwa sana cha mawasilisho kutoka kwa silaha kubwa,'' alisema Hamish de Bretton Gordon, kanali wa zamani wa Jeshi la Uingereza na mtaalamu wa silaha wa Chuo Kikuu cha Cambridge.

An apparent submunition impact from a cluster bomb in a Kharkiv residential neighbourhood
Maelezo ya picha, Mgawanyiko uliojitokeza nu athari za mabomu ya kutapakaa unaoonekana katika kitongoji cha makazi cha Kharkiv (Joel Gunter/BBC)

Mabomu ya cluster yana utata kwa sababu hulipua angani na kutoa kundi la mabomu madogo ambayo huanguka kiholela katika eneo kubwa, na hivyo kuwaweka raia katika hatari.

Mabomu madogo pia mara nyingi hushindwa kulipua na kusababisha tishio kwa miaka ijayo.

Zaidi ya nchi 120 zimetia saini mkataba unaokataza matumizi ya silaha hizo - ingawa si Urusi au Ukraine zilizotia saini.

Katika eneo moja la tukio lililoathirika la mabomu ya kutapakaa huko Kharkiv, karibu na eneo la makazi na uwanja wa michezo katika kitongoji cha Industrialnyi, athari ya uharibifu ilionekana kwa karibu aina tatu tofauti katika pande tatu za uwanja wa michezo.

Mke wa Ivan Litvynyenko Oksana alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo na baadaye akafariki dunia.

Litvynyenko, 40, aliambia BBC kwamba wanandoa hao walikuwa wakitembea kwenye uwanja wa michezo pamoja na binti yao mwenye umri wa miaka mitano wakati risasi zilipotokea.

Mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka 14 alikuwa ndani ya nyumba yao.

''Ghafla nikaona mwanga na nikasikia mlipuko wa kwanza,'' Litvynyenko alisema.

''Nilimshika binti yangu na kumkandamiza kwenye mti. Mke wangu alikuwa karibu mita tano na alidondoka.''

An impact site next to where Ivan Litvynyenko's wife was hit by shrapnel. (Joel Gunter/BBC)
Maelezo ya picha, Eneo lililoathirika karibu na uwanja wa michezo ambapo mke wa Ivan Litvynyenko alipigwa na bomu.

Oksana, 41, alipigwa na vipande vilivyopenya kwenye mgongo wake, kifuani na tumboni, na kutoboa mapafu yake na kuharibu uti wake wa mgongo.

Alikuwa katika uangalizi maalum kwa miezi miwili, hadi Jumapili, alipofariki kutokana na majeraha na kisukari, Litvynyenko alisema.

Madaktari walimfanyia upasuaji mara kadhaa lakini mwili wake haukuweza kuhimili," alisema, akizungumza saa chache baada ya kifo chake.

Akielezea shambulio hilo, Litvynyenko alisema aliona "msururu wa milipuko, mabomu mengi moja baada ya jingine".

Wakaazi wengine wawili waliokuwa ndani ya vyumba vyao wakati wa mgomo huo waliambia BBC kwamba walisikia milipuko iliyofuatana wakati shambulio hilo lilipotokea.

"Ungeweza kusikia milipuko kwa dakika kadhaa," alisema Danya Volynets, 26. "Tulipokuja nje niliweza kuona magari yaliyokuwa yakiungua. Ilionekana kana kwamba kila kitu kilikuwa kinawaka moto."

Tetiana Ahayeva, muuguzi mwenye umri wa miaka 53, alikuwa amesimama mbele ya jengo lake wakati mabomu yalipolipuka.

"Kulikuwa na sauti ya ghafla ya kama fataki kila mahali, nyingi, kila mahali," aliiambia Amnesty.

"Tulianguka chini na kujaribu kutafuta mahali pa kujificha. Mtoto wa jirani yetu, mvulana wa miaka 16 anayeitwa Artem Shevchenko, aliuawa papo hapo. Alikuwa na tundu la sentimita 1 kifuani. Baba yake alikuwa amepasuka nyonga huku akiwa na jeraha lililotokana na kipande cha bomu kwenye mguu wake."

Oksana Litvynyenko with her daughter. Oksana was badly wounded in April and died on Sunday. (Family handout)
Maelezo ya picha, Oksana alijeruhiwa vibaya mnamo Aprili na alifariki siku ya Jumapili. (Kielelezo cha familia)

Madaktari katika hospitali kuu ya Kharkiv walisema kuwa kati ya wahasiriwa walioletwa kutokana na shambulizi la uwanja wa michezo walikuwa na majeraha ya kupenya kwenye tumbo, kifuani na mgongoni, na walikusanya vipande vya chuma ambavyo vililingana na aina za mabomu madogo yaliyopatikana katika mabomu ya cluster ya 9N210/9N235.

Kulingana na shirika la Amnesty, shambulio hilo katika kitongoji cha Industrialnyi liliua takriban raia tisa na kujeruhi wengine 35, na kulipua eneo la mita za mraba 700.

Katika jengo jingine la makazi, katika eneo la Mtaa wa Haribaldi, Kharkiv, risasi ilitua kwenye lango la kuingilia kwenye jengo hilo, na kuua wanawake wawili vikongwe na wengine kujeruhiwa vibaya.

Athari ya kutapakaa kwa bomu hilo inaweza kuonekana karibu na mlangoni na kwenye njia iliyo karibu.

Kulikuwa na mfululizo wa milipuko moja baada ya jingine, "mkazi Nadia Kravchuk, 61, alisema. "Nilitoka nje na kuona mwanamke amelala hapa chini na mwanamke mwingine amelala hapa, na karibu nao alikuwa Lena, ambaye alipoteza miguu yake yote miwili. Alikuwa akilia huku akisema, "Nimepoteza mguu wangu."

Tetiana Bielova na Olena Sorokina walikuwa wameketi kwenye benchi nje wakati risasi ilipolipuliwa karibu.

Walinyanyuka ili waingie ndani ya jengo hilo lakini risasi ya pili ilitua kwenye lango la kuingilia na kuwaua Bielova na mwanamke mwingine aliyeitwa Tetiana aliyekuwa nao.

Sorokina alipoteza miguu yake yote miwili katika mlipuko huo.

Nadia Kravchuk looks down at damage from a munition that killed two of neighbours (Joel Gunter/BBC)
Maelezo ya picha, Nadia Kravchuk anaangalia chini uharibifu kutokana na silaha iliyoua majirani zake wawili (Joel Gunter/BBC)

Kwa jumla, katika utafiti wa uwanja wa wiki mbili, Amnesty ilichunguza migomo 41 huko Kharkiv ambapo takriban raia 62 waliuawa na 196 kujeruhiwa, shirika la kutoa misaada lilise

Walipata ushahidi wa makundi ya kivita na makombora ambayo hayakuwa na risasi na kuua watu waliokuwa wakinunua vitu, wakipanga foleni kutafuta msaada wa chakula, au wakitembea tu barabarani.

"Silaha hizi hazipaswi kutumiwa kamwe," Donatella Rovera, mshauri mkuu wa Amnesty wa kukabiliana na mzozo, aliiambia BBC.

"Haziwezi kubainishwa. Ni silaha za eneo hilo. Na zina madhara makubwa na kusababisha vifo vingi vya raia na majeraha."

Matumizi ya silaha yalikuwa "sawa na kuwalenga raia kimakusudi," Rovera alisema.

"Urusi haiwezi kudai kuwa haijui athari za aina hii ya silaha," alisema.

"Na uamuzi wa kuzitumia unaonyesha kutojali kabisa maisha ya raia."

Hapo awali Urusi ilikanusha kutumia mabomu ya cluster ya kutapakaa nchini Ukraine na kusisitiza kuwa majeshi ya Urusi yameshambulia tu malengo ya kijeshi.