Utani wa kuuza vidole vya mguu Zimbabwe waeleweka vibaya Nigeria

    • Author, Chiagozie Nwonwu
    • Nafasi, BBC News, Lagos
  • Muda wa kusoma: Dakika 2

Utani unaoendelea katika mtandao wa kijamii nchini Zimbabwe kuhusu watu kuuza vidole vyao vya miguu kwa fedha nyingi , kunachukuliwa na umuhimu mkubwa kwengineko barani Afrika.

Taarifa hiyo kwamba raia wa Zimbabwe wanauza vidole vyao vya miguuni ili kukabiliana na umasikini imesambaa sana nchini Nigeria.

Mwanablogu mmoja wa Zimbabwe amedai kwamba biashara hiyo inafanyika katika kituo kimoja cha maduka katika mji mkuu Harare.

Inanukuua ujumbe wa WhatsApp ukiwa na takwimu za hadi $40,000 (£31,800) zinazotolewa na watatbibu wa kitamaduni. Wakijulikana kama waganga bandia wanaoshirikishwa na uchawi - hushtumiwa na waganga wa kienyeji wanaoheshimika kwa jina 'sangoma' kusini mwa bara Afrika.

Lakini waandishi wanasema kiwango cha fedha kinachotumika ni $40,000 kwa kidole gumba , $25,000 kwa kidole cha katikati na $10,000 kwa kidole kidogo .

Utani wa vidole umesambaa kote nchini Zimbabwe , vikichapishwa na alama ya reli #Chigunwe, ikimaanisha Vidole vya mguuni katika lugha ya Shona , na hivyobasi kuzua ucheshi wakati ambalo hali ya kiuchumi imekuwa ngumu.

Lakini hakuna hata gazeti moja la Zimbabwe lililochukua habari hiyo na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twitter wamelalamika kwamba utani huo unazuia masuala muhimu yanayowakabili raia katika taifa hilo kuangaziwa.

Mwanablogu kwa jina Gambakwe alichapisha mnamo tarehe 28 mwezi Mei kwamba biashara ya kuuza vidole inaendelea katika duka kuu la Ximex Mall.

Siku chache baada ya chapisho la mwanablogu huyo, gazeti la burudani la H Metro lilichapisha mahojiano na wafanyabiashara wa soko haramu katika duka hilo ambao walisema kwamba , suala lote lilisambazwa kupitia kiasi baada ya baadhi yao kulisambaza kama utani.

Lakini tangu wakati huo, wanasema kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakielekea katika duka hilo la Ximex kuulizia kuhusu biashara hiyo kufuatia uvumi huo.

Watumiaji wa mtandao wa twitter kutoka mataifa kadhaa ya Afrika, ikiwemo Nigeria na Uganda, walianza kuchapisha kwamba raia wa Zimbabwe wamewaza kuuza vidole vyao vya mguuni kwa maelfu ya madola.

Kituo kimoja cha redio nchini Kenya pia kilichapisha ujumbe wa twitter , kikidai zilikuwa habari ambazo hazijathibitishwa, wakiwauliza mashabiki wao ni kiungo gani cha mwili wangelipenda kuuza.

Chapisho la mtandao wa Twitter lililofanywa na @InnocentZikky, ambalo lilisambazwa mara 2,668 na kupendwa mara 4731 katika kipindi cha saa 18 ni pamoja na picha za mguu usio na vidole vyote.

Kitengo cha BBC cha habari ambazo hazijathibitishwa kiliangazia kanda mbili za video zinazodaiwa kuwa watu waliouza vidole vyao au walikuwa katika harakati za kuuza vidole vyao na kuamini kwamba ni kitu kilichopangwa.

Lakini machapisho hayo ya mitandao ya kijhamii mara nyengine hutoa athari za kweli na yanaweza kuaminiwa na kuigwa.

Habari hiyo imegusa wengi nchini Nigeria hususan maeneo ambayo yanaaminika kushiriki katika matambiko ya kifedha - imani potofu kwamba matumizi ya viungo vya mwili yanaweza kuleta utajiri.

Mnamo mwezi Januari , watu watatu walikamatwa nchini Nigeria kwa madai ya kumuua msichana mdogo kwa lengo la kufanya tambiko.