Urusi na Ukraine: Kitakachotokea iwapo Vradmir Putin atatangaza rasmi vita dhidi ya Ukraine

Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Jumatatu mtandao wa habari wa Marekani CNN ulitangaza kuwa Rais wa Urusi Vradimir Putin anaweza kutangaza rasmi vita dhidi ya Ukraine tarehe 9 , ukiwanukuu maafisa wa Marekani.

Ulisema kuwa Putin anaweza kutumia siku ya ushindi ya nchi hiyo Victory Day kama sababu ya kutangaza mafanikio ya ya kivita ya nchi hiyo nchini Ukraine, kufanya mashambulizi zaidi, au kufanya yote kwa pamoja, vyanzo vilivyohojiwa na televisheni hiyo vilisema. Wanatazamia kutangazwa kwa azimio rasmi la vita kutolewa.

Tarehe 9 Mei, Urusi husherehekea ushindi katika Vita kuu ya II ya dunia -siku ambayo ni ya mapumziko kwa taifa ima ambayo ina maana ya kipekee kwa familia nyingi za Warusi. Siku hii pia huwa ni siku muhimu kwa taifa kutoa propaganda zake . Mwaka huu pia ni siku muhimu kwa jeshi la Urusi, wakati Rais Putin anaweza kujigamba kwa mafanikio makubwa ya vita vya Ukraine.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ulianza Fenruari 24, lakini kwa sasa S maafisa wa Urusi wanasisitiza kwamba ''operesheni maalumu ya kijeshi'' inafanyika katika Ukraine, maneno "vita" na "uvamizi" katika dhana ya uhasama yamepigwa marufuku kutumiwa nchini Urusi.

Kulingana na CNN, tangazo rasmi la vita linaweza kuongeza uungaji mkono wa umma, pamoja na kuwaruhusu maafisa Warusi kutoa wito wa kuhamasisha umma kuuunga mkono vita, jambo ambalo kwa sasa Urusi inalihitaji sana.

Urusi inasema nini?

Russia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wataalamu wengi wanasema viongozi wa kijeshi wa Urusi wanataka kutumia siku ya tarehe 9 Mei kama tarehe ya kushinda vita katika ukraine

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov Jumatano alisema ripoti za uwezekano wa tangazo la Urusi kutangaza rasmi vita dhidi ya Urusi tarehe 9 Mei "sio ukweli na ni upuuzi ."

Tarehe 20 Februari, siku tatu kabla ya mwanzo wa kile kinachoitwa na Urusi operesheni maalum ya kijeshi , Peskov aliziita ripoti za mipango ya uvamizi wa vikosi vya Urusi ndani ya Ukraine kama uchokozi na uchochezi wa hisia : "Tunawakumbusha kwamba Urusi haijawahi kumshambulia yeyote katika historia yake. Na Urusi, ambayo imenusurika na vita vingi sana- hii ni nchi ya mwisho ya Ulaya ambayo haitaki kuzungumzia kabisa, hata kutamka neno ''vita'' ,alisema Msemaji wa Rais

Maelezo kwamba tarehe 9 Mei Putin anaweza kutangaza uhamasishaji , pamoja na kutangaza vita kamili ''dhidi ya ulimwengu wa Wanazi ", ilitolewa awali na Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace.

Wakati huo huo kulingana na Papa Francis, Waziri wa Hungary Viktor Orban alimwambia yeye wakati wa mkutano tarehe 21 Aprili kuwa maafisa wa Urusi wanapanga kumaliza uhasama wa kivita tarehe 9 Mei.

Москва

Chanzo cha picha, Sergei Bobylev/TASS

Kulingana na katiba ya Shirikisho ya Urusi "kuhusu sheria ya jeshi ",orodha yifuatayo inaonyesha hatua inayoweza kutambuliwa kama uchokozi wa kigeni. (maelezo ya kina zaidi yanaweza kupatikana katika katiba ya Urusi).

  • Shambulio la jeshi la kigeni katika eneo lla Shirikisho la Urusi, uvamizi wa jeshi, kuchukuliwa kokote kwa eneo au sehemu yake na hivyo,
  • Matumizi ya silaha dhidi ya Urusi. Kwa mfano, kupiga makombora au kupiga mabomu kwenye eneo
  • Kufungwa kwa bandari au maeneo ya mwambao ;
  • Shambulio la jeshi la kigeni dhidi ya vikosi vya Urusi, bila kujali viko sehemu gani,
  • Kutolewa kwa eneo kwa taifa la eneo lake kwa ajili ya mashambulio ddhidi ya Urusi'
  • Kutumwa kwa makundi ya taifa la kigenu, vikosi vya kawaida au mamluki au ambao watatumia kikosi chenye silaha dhidi ya Urusi

Hali ya vita na utawala wa kijeshi

Utawala wa jeshi pia unaweza kuanzishwa baada ya Urusi kutangazwa rasmi vita. Utaratibu wenyewe wa tangazo hili hauelezewi kwa kina katika sheria za Urusi. Iaonyesha tu hali zinazoweza kupelekea kutangazwa kwa hali ya vita katika nchi.

Hali ya vita hupelekea kuanzishwa uawala wa jeshi, ingawa haya ni tofauti na mtizamo wa kisheria-neno "hali ya vita "inahusiana na mahusiano ya mataifa, "utawala wa kijeshi" ni utawala maalumu ndani ya taifa.

Utawala wa kijeshi katika urusi unadhibitiwa na sheria kadhaa - "sheria kuhusu utawala wa kijeshi", " Kuhusu Ulinzi ", "Kuhusu uhamasishaji", "Kuhusu mawasiliano", "Kuhusu jukumu la jeshi na sheria kuhusu Huduma ya jeshi ".

Inahusika karibu katika maeneo yote ya taifa-maisha ya umma, mamlaka, uchumi, biashara, vyombo vya habari, udhibiti wa siasa na maeneo mengine.

Rais na tawi la utendaji watapokea mamlaka ya kipekee katika hali kama hiyo.

Uhamasishaji

Chini ya Utawala wajeshi, uhamasishaji unaweza kutangazwa. Unanaweza kuwa kamili au wa kiwango kidogo, hii ikimaanisha kuwa unaweza kuanzishwa kote nchii au katika maeneo fulani . Uhamasishaji hauhusiani na kuanzishwa kwa utawala wa jeshi-unaweza kutangazwa bila utawala wa jeshi.

Dhana hii, haiwahusu tu wale waliosajiriwa katika jeshi. Uhamasishaji unahusu mamlaka, viwanda, na uchumi wote kwa ujumla.

Lakini zaidi ya yote, inavihusu vikosi vya kijeshi, ambavyo vitahitaji kuongeza wanajeshi kutoka kwenye vikosi vya akiba ambavyo vinajumuisha wanajeshi maalumu wa uhamasishaji wa raslimali zinazohitajika.

Российский солдат в Донецке

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utawala wa jeshi, kulingana na wanaouunga mkono, ni muhimu, kwanza kabisa, kuhakikisha uhamasishaji

Kikundi cha kwanza- cha wanajeshi wa akiba ambacho kiko tayari zaidi kwa uhamasishaji, ambao wamekamilisha mkataba maalumu na taifa, cha pili - ni cha wanajeshi wa akiba wote waliohudumu katika jeshi na wameajiriwa kama wanajeshi wa akiba watahusishwa.

Baadhi ya wale ambao wanaweza kuajiliwa katika jeshi kama chini ya sheria ya uhamasishaji wanaweza kupewa kazi- hakikisho kwamba wataendelea kubakia kazini . Hii ni muhimu ili kuhakikisha kazi za mamlaka na viwandani zinafanyika.

Azimio la vita na uhamasishaji linaweza kutatua walau matatizo mawili ambayo wataalmau wengi wanasema jeshi la Urusi linakabiliana nayo-upungufu wa wanajeshi na kukataliwa kuingia katika maeneo ya vita ndani ya Ukraine.

Marekani inasemaje kwa sasa?

Kwa sasa, mashambulio ya jeshi la Urusi katika Ukraine yanafanyika kwa kasi ya chini. Vikosi vya Urusi vina ukomo wa maeneo vinavyoyadhibiti katika miji wa mashariki wa Izyum na Popasnaya lakini mafanikio yamekuwa ni ya "kujivuta na sya kutofautiana," alisema afisa wa Pentagon.

Zaidi ya hayo pentagon ilisema kuwa vikosi vya Urusi vinaonekana kuwa vinakwepa hatri na kujaribu kuepuka kupata majeruhi miongoni mwa wanajeshi wake, wa anga na wa ardhini.

Ukweli ni kwamba jeshi la Urusi hali watu wa kutosha na pia ni hilo linaonekana wazi kwa ukweli kwamba Wizara ya ulinzi ya Urusi imekuwa ikijaribu kuwaajiri wanajeshi kwa mkataba tangu mwanzoni mwa mwezi Machi kwa kutuma matangazo kupitia wavuti wa kazi wa kiraia unaofahamika kama HeadHunter na ule wa SuperJob.

Uchumi

Utawala wa kijeshi pia unaweza kuwa na athari mbaya kwa uchumi wa Urusi.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Utawala wa kijeshi pia unaweza kuwa na athari mbaya kwa uchumi wa Urusi.

Utawala wa kijeshi pia unaweza kuwa na athari mbaya kwa uchumi wa Urusi.

Aya tofauti ya cha sheria kuhusu utawala wa jeshi kinaelezea kuhusu mashirika. Kwa mfano, makampuni yanapaswa kutoa mali zao zote kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya ulinzi wa nchi . wakati huo huo, nchi inachukua jukumu la kulipa garama ya mali hizi.

Ukweli, kulingana na kanuni hiyo, taifa litaweza kunyakua mali kutoka kwa raia katika eneo ambako utawala wa kijeshi umeanzishwa. Mashirika pia yatakuwa na jukumu la kutekeleza maagizo na majukumu kwa ajili ya malengo ya ulinzi- kulingana na makubaliano yaliyofikiwa.

Katika hali hii pia, kulingana na sheria, raia wanaweza kuhusika katika kuondoa athari za matumizi ya silaha, kurejesha vifaa vya kiuchumi, mifumo ya kunusuru maisha na vifaa vya kijeshi, na pia kusaidia kwa mfano kukabiliana na mioto.