Fahamu nchi mbili za kiislamu ambazo ni marufuku kuoa wake wengi

th

Chanzo cha picha, MANAN VATSYAYANA/AFP VIA GETTY IMAGES

Katika maeneo mbalimbali duniani hasa nchi ambazo si za kiislamu kuna sheria zinazokataza mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja.

Kwa upande wa nchi za kiislam, nyingi zinaruhusu ndoa za wake zaidi ya mmoja kutokana na maandiko katika dini ya kiislam.

Lakini kuna nchi mbili za kiislamu ambazo mbali na kuwa ni mataifa ya kiislam lakini ni marufuku kuoa mke zaidi ya mmoja.

Nchi hizi mbili ni Uturuki na Tunisia.

Uturuki imekuwa nchi ya kwanza ya kiislamu kupiga marufuku ndoa za wake wengi, huku Tunisia ikiwa ni nchi pekee ya kiarabu ambako sheria hiyo inatumika.

Mnamo 1926, ndoa ya wake wengi ilipigwa marufuku nchini Uturuki, na uamuzi huo haukuwa wa kidini bali wa mfumo wa kidunia.

Kwa upande wa Tunisia, ilipiga marufuku ya kwanza mnamo 1956 na kufanyiwa marekeisho upya mnamo 1964.

Kipindi cha televisheni cha Ramadhani kwenye televisheni ya Tunisia kimezua gumzo katika siku za hivi karibuni kuhusu kujumuishwa kwa ndoa za mitala.

Mmoja wa waigizaji wa vichekesho alimwambia mke wake na watoto kwamba ana haki ya kidini ya kuoa mke wa pili. Lakini Hata hivyo, sheria inatoa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa yoyote atakayekiuka sheria hiyo.

W
Maelezo ya picha, Ndoa za wake wengi ni kawaida katika mataifa mengi ya Kiislamu

Mashirika ya kutetea haki za wanawake ni miongoni mwa yale ambayo yamelaani suala hilo lenye utata.

Kipindi hicho cha televisheni kimekosolewa vikali kwenye mitandao ya kijamii.

"Inasikitisha kuona mada hii ikijadiliwa," alisema mwigizaji wa tunisia mariem ben hussein.

Habib Bourguiba, kiongozi wa nchi hiyo baada ya uhuru alipiga marufuku ndoa za mitala, na sheria hiyo ilitungwa miezi mitano tu baada ya Tunisia kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wa Ufaransa.

Kisha ikatambulishwa nchini humo kwamba talaka ilikuwa kesi ya mahakama iliyoamuliwa na majaji, ambayo ilimaanisha kwamba mume hawezi kumtaliki mke wake kwa urahisi, kwa maneno tu.

Katika nchi nyingine za kiislamu, ndoa za mitala ama wake wengi ni halali lakini imedhibitiwa.

Nchi hizi ni pamoja na Misri, Sudan, Algeria, Jordan, Syria, Morocco, Bangladesh, Iraq, Iran, Kuwait na Lebanon.

w
Maelezo ya picha, Shekhe akifungisha ndoa ya kiislamu

Indonesia, nchi yenye waislamu wengi zaidi duniani, haipigi marufuku mitala lakini baadhi ya majimbo yana sheria zao dhidi yake.

Mnamo mwaka wa 2008 kulikuwa na maandamano ya kupinga mitala nchini Indonesia lakini matokeo yake hayakubadilisha sheria za nchi.

Wanaume waislamu wanaruhusiwa kuoa hadi wake wanne, ingawa masharti makubwa.

Mnamo machi 2019, Mwanazuoni maarufu wa Misri, Al-azhar Imam Ahmed El-Tayeb alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu ndoa za mitala, alisema mara haikuwa sawa kwa mke wake na watoto.

Imam Ahmed wakati huo aliwataka wanaume kuzingatia masharti ya kuoa wako wengi.