Vipandikizi vya chipu ndogo ambavyo vitakuwezesha kufanya malipo kwa mkono wako

A woman using a contactless payment microchip implant

Chanzo cha picha, Piotr Dejneka

Maelezo ya picha, Mwanamke akilipia mlo wake katika mkahawa kwa kutumia chipu ya malipo iliyopandikizwa mkononi mwake

Patrick Paumen husababisha mshangao kila anapolipia kitu dukani au kwenye mgahawa.

Hii ni kwa sababu kijana huyo mwenye umri wa miaka 37 hahitaji kutumia kadi ya benki au simu yake ya mkononi kulipa.

Badala yake, anaweka tu mkono wake wa kushoto karibu na kisoma kadi.

Nuru ndogo ya mwanga ya LED chini ya ngozi yake kisha huangaza mara moja, na malipo kufanyika."Mwitikio ninaoupata kutoka kwa washika fedha hauelezeki."

Anasema Bw Paumen, mlinzi kutoka Uholanzi.

Anaweza kulipa kwa kutumia mkono wake kwa sababu mwaka wa 2019 alikuwa na kifaa kidogo cha malipo yaani chipu, kikubwa kidogo kuliko punje ya mchele, kilichoingizwa chini ya ngozi yake.

"Utaratibu huo unauma kama vile mtu anapoifinya ngozi," asema Bw Paumen.

Patrick Paumen's payment chip implant lights up

Chanzo cha picha, Patrick Paumen

Maelezo ya picha, Bwana Paumen ana chipu iliyoingizwa chini ya ngozi ya mkono wake wa kushoto, na hutoa mwanga wakati malipo yanafanywa.

Chipu ilipandikizwa kwa binadamu kwa mara ya kwanza mwaka wa 1998, lakini ni katika muongo mmoja uliopita ambapo teknolojia hiyo imekuwa ikipatikana kibiashara.

Na linapokuja suala la malipo kupitia chipu zinazoweza kupandikizwa, kampuni ya Uingereza-yenye makao yake huko Poland, Walletmor, inasema kwamba mwaka jana ilikuwa kampuni ya kwanza kuziuza.

Kipandikizi hicho kinaweza kutumika kulipia kinywaji katika ufuo wa Rio, kahawa huko New York, kunyolewa nywele huko Paris - au kwenye duka lako la mboga," anasema mwanzilishi na mtendaji mkuu Wojtek Paprota.

"Inaweza kutumika popote ambapo malipo ya kielektroniki yanakubaliwa."

Chipu ya Walletmor, ambayo uzito wake ni chini ya gramu, inajumuisha chipu ndogo kabisa na antena iliyowekwa kwenye biopolymer - nyenzo asili, sawa na plastiki.

Bw.Paprota anaongeza kuwa ni salama kabisa, ina kibali cha udhibiti, inafanya kazi mara tu baada ya kupandikizwa, na itakaa imara mahali pake.

Pia hudumu kwa muda usiojulikana, na hauhitaji betri, au chanzo kingine cha nguvu ya nishati.

Kampuni hiyo inasema kwa sasa imeuza zaidi ya chipu 500.

Teknolojia ambayo Walletmor hutumia ni mawasiliano ya karibu-uga yaani near-field communication (NFC), mfumo wa malipo wa kielektroniki katika simu ya mkononi.

Vipandikizi vingine vya malipo vinatokana na utambulisho wa mitabendi za redio yaani radio-frequency identification (RFID), teknolojia ambayo kwa kawaida hupatikana katika kadi za malipo za mkopo za kielektroniki.

An x-ray showing a Walletmor implant

Chanzo cha picha, Walletmor

Maelezo ya picha, Picha ya x-ray inayoonyesha kipandikizi cha Walletmor, ambacho huingizwa kwenye mkono wa mtu baada ya kumfanya awe katika hali ya kupotewa na fahamu.

Kwa wengi wetu, wazo la kupandikizwa kwa chipu kama hiyo katika miili yetu ni la kutisha, lakini uchunguzi wa mwaka 2021 wa zaidi ya watu 4,000 kote Uingereza na Umoja wa Ulaya uligundua kuwa 51% wangeweza kufanyiwa.

Hata hivyo, bila kutoa idadi ya asilimia, ripoti hiyo iliongeza kuwa "uvamizi na masuala ya usalama kumesalia kuwa kero kubwa" kwa waliohojiwa.

Bw Pauman anasema hana wasiwasi wowote kati ya haya.

"Vipandikizi vya chipu vina aina ile ile ya teknolojia ambayo watu hutumia kila siku," anasema.

"Umbali wa kusoma hupunguzwa na koili ndogo ya antena ndani ya kipandikizi.

Kipandikizi kinahitaji kuwa ndani ya sehemu ya sumakuumeme ya kisomaji kinachooana cha RFID [au NFC].

Ni wakati tu ambapo kuna muunganisho wa sumaku kati ya msomaji na kifaa ndipo kipandikizi kinaweza kusomwa.

"Anaongeza kuwa hana wasiwasi kwamba aliko kunaweza kufuatiliwa. "Chipu za RFID hutumiwa kwa wanyama wa nyumbani kuwatambua wanapopotea," asema.

" Lakini haiwezekani kuwapata kwa kutumia kipandikizi cha chip cha RFID - mnyama anayepotea anahitaji kupatikana kimwili.

Kisha mwili wote huchanganuliwa hadi kipandikizo cha RFID kipatikane na kusomwa.

"Lakini bado suala la chipu kama hizo, (kinachosababisha wasiwasi), ni kama katika siku zijazo zitakuwa za hali ya juu zaidi, na kujazwa data binafsi ya mtu.

Na, kwa upande wake, kama habari hii ni salama, na ikiwa mtu angeweza kufuatiliwa kweli.

Teknolojia ya fedha au fintech, mtaalamu Theodora Lau, ni mwandishi mwenza wa kitabu cha 'Beyond Good: How Technology Is Leading A Business Driven Revolution'. anasema kwamba chipu za malipo zilizopandikizwa ni "kiendelezo tu cha mtandao wa mambo.

"Kwa kusema hivyo anamaanisha njia nyingine mpya ya kuunganisha na kubadilishana data.

Theodora Lau

Chanzo cha picha, Theodora Lau

Maelezo ya picha, Theodora Lau anasema kwamba katika siku zijazo tutahitaji kujua mpaka wetu linapokuja suala la vipandikizi kama hivyo.

Hata hivyo, anasema kwamba watu wengi wako tayari kwa wazo hilo - kwani litafanya malipo kufanyika kwa haraka na rahisi - faida lazima ziwe za juu kuliko hatari.

Hasa wakati chipu zilizopachikwa hubeba habari zetu za kibinafsi zaidi.

"Tuko tayari kulipa kiasi gani, kwa ajili ya malipo kufanyika kwa urahisi?", anasema.

"Tunahitajika kuweka wapi mpaka linapokuja suala la faragha na usalama? Nani atakuwa akilinda miundombinu muhimu, na wanadamu ambao ni sehemu yake?

Patrick Paumen

Chanzo cha picha, Patrick Paumen

Maelezo ya picha, Bw Paumen pia ana sumaku zilizopandikizwa kwenye vidole vyake

Huko Uholanzi, chipu ya malipo ya Bw Pauman ina taa ya LED iliyojengewa ndani ambayo inaendeshwa na nguvu ya kwenye kitu fulani kwenye mwili wake.

Akijielezea kama - mtu ambaye huweka vipande vya teknolojia katika mwili wake ili kujaribu kuboresha utendaji wake - ana vipandikizi 32 kwa jumla, ikiwa ni pamoja na chipu kufungua milango na sumaku zilizopachikwa.

"Teknolojia inaendelea kubadilika, kwa hivyo ninaendelea kukusanya zaidi," anasema.

"Vipandikizi vyangu huongeza mwili wangu. Nisingependa kuishi bila hivyo," anasema.

"Siku zote kutakuwa na watu ambao hawataki kurekebisha miili yao. Tunapaswa kuheshimu hilo - na wanapaswa kutuheshimu kama wadukuzi wa viumbe."