Mzozo wa Ukraine: Ukweli kuhusu madai ya Urusi kwenye mauaji ya Bucha

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitisha uchunguzi unaojitegema dhidi ya picha za mauaji ya rais huko Bucha Ukraine.

Onyo: Habari hii ina picha zinaweza kuogofya.

Baada ya vikosi vya Urusi kuondoka nje ya mji wa Kyiv, picha za miili iliyotapakaa kwenye mitaa zilisambaa na baadhi ya waandishi wa habari waliona maiti.

Ukraine inashutumu Urusi kwa mauaji ya halaiki, lakini Urusi inasema ni mpango wa propaganda wa Kiev.'' iliendelea kutoa madai kuhusu picha za video kutoka Bucha.

Madai:'Miili feki ya watu waliokufa'

Baada ya Urusi kujiondoa, picha za video zilizorekodiwa kutoka kwenye gari zinaonesha miili ikiwa imetapakaa katika pande zote za mitaa.

Mitandao ya kijamii inayounga mkono urusi, wamesambaza video hiyo na kusema kuwa mkono wa mwili wa mtu mmoja ulikua ukisogea.

Ubalozi wa Urusi nchini Canada waliweka video, Ubalozi wa Urusi nchini Canada, ulituma video kwenye mtandao wake wa Twitter na kuandika kuwa''Video hii imetengenezwa ikionesha miili ya watu waliogiza wamekufa''

Video haionekani vizuri lakini yale madai ya kuwa mkono uliosogea, si sahihi bali ni alama iliyopo kwenye upande wa kulia wa kioo cha gari.

Madai mengine ya Urusi yanatikita kwenye eneo tofauti la video hiyo. Gari inapita na kuonesha mwili mwingine ambao umelazwa kwenye kibaraza chenye mawe ya njano na pembeni kuna uzio wa udhurungi.

Lakini video hiyo ikienda kwa taratibu Urusi inadai kuwa mwili wa mtu huyo unaonekana ukikaa. Lakini uhalisia wa video hauonekani kwasababu haionekani vizuri ikiwemo majengo katika eneo hilo.

BBC imelinganisha miili yote miwili kutoka kwenye video iliyosambazwa tarehe 2 Aprili, na picha yenye ubora iliyotolewa na Getty Images na AFP tarehe 3 April.

Katika Video mwili wa kwanza umelala kwenye pembe ya barabara na pembe ya kulia ina majani. Gari rangi ya Silver inaonekana kwenye kibaraza na mlango wa nyuma ukiwa wazi, na vitu vyote hivyo vinaonekana kwenye picha ya Getty na AFP.

Mwili wa pili una koti jeusi, na kuna bandeji yenye damu katika mkono wa kulia. zipo upande wa kibaraza chenye rangi nyekundu na njano, mbele ya jengo liloharibiwa, koti jeusi, bandeji na na uzio vyote vinafanana na picha ya mwili iliyotolewa na AFP/GETTY.

Madai: 'Miili haijakakamaa'

Wizara ya mambo ya nje ya urusi ilituma kwenye ukurasa wake wa twitter ''Inashangaza kuona kua picha zote zilizotumwa na Kiev, miili bado haijakauka mbali ya kuonekana siku nne zilizopita''

Kwa mujibu wa jeshi la Ukraine, Urusi iliondoa vikosi vyake mapema tarehe 31, na Urusi inasema iliondoka tarehe 30.

Masaa baada ya kifo mwili hupitia mabadiliko ikiwemo viongo kukamaa na kuwa vikavu.

Tulimuuliza mtaalamu kuwa je baada ya siku nne mwili unaweza kukauka ama kukamaa. Mtaalam mmoja ambaye amefanya kazi Cosovo na Rwanda kwenye uchunguzi wa uhalifu wa kivita amesema kuwa ndani ya siku nne mwili unaweza kupungua kukaamaa.

Urusi pia imedai pia kuwa miili haina ''alama zozote''.

Hakuna uhakika kuwa wana maana gani lakini wataalamu wanasema kuwa majeraha ya silaha hutofautina kutokana na aina mbalimbali za silaha zilizotumika, na umbali gani ulihusika wakati wa shambulizi.

Hakuna damu inayoonekana inaweza kuwa imefyozwa na nguo tena hususani mtu akiwa amevaa nguo nzito za kuzuia baridi.

Madai ya Urusi pia yanaweza kumaanisha kuwa mwili wa mtu unaweza kubadilika na kuwa na rangi ya zambarau kwasababu damu haitembei tena mwilini. Lakini kama mwili uko chini, rangi haiwezi kutambulika kutoka kwenye picha tu.

Madai: 'Hakuna mkazi yoyote ambae amekumbwa na mashambulizi'

Wizara ya ulinzi ua Urusi inadai kuwa wakati Bucha ikiwa chini ya uvamizi wa Urusi hakuna hata raia mmoja ambaye alishambuliwa.

Lakini hata hivyo madai hayo yanapingana na mashuhuda ambao ni wakazi na waliona mashambulizi kadhaa.

Mwalimu kutoka enelo hilo aliambia shirika la Human Right Watch siku ya tarehe 4 machi kuwa Urusi ilivamia watu wanne na kumuua mmoja wao.

Mkazi mwingine wa Bucha aliiambia tovuti ya uchunguzi ya Urusi kuwa ''zilikua siku ngumu sana, hakuna unachomiliki kuanzia uhai wako hadi nyumba yako, hakuna umeme, maji wala gesi na ukitoka nje unapigwa risasi''

Wizara ya ulinzi ya Urusi imedai kuwa vikosi vyake viliondoka bucha tarehe 30 machi na kuwa video zinazoonesha miili zilianza kusambazwa siku ya nne yake, pale ambapo vyombo vya habati vya urusi na vikosi vyake vilivyoingia Bucha.

Lakini mashirika ya habari kama AFP walituma picha za miili tarehe 2 Aprili na tulipata video zilizoambazwa kwenye mitandao ya kijamii mapema tarehe 1 Aprili.