Kenya kupokea mamilioni ya kupambana na Covid ilionaswa huko Jersey

Mamilioni ya pesa za umma zinazodaiwa kuibwa na matajiri wawili wa Kenya zinatarajiwa kurejeshwa nchini humo kununua vifaa vya kjupambana na Covid-19 kufuatia kesi ya kihistoria.

Makubaliano hayo yaliyofanyika Jersey, kisiwa kinacho jitawala Uingereza, yametajwa kuwa ni "ushindi kwa watu wa Kenya" na balozi wao wa Kenya nchini Uingereza, Manoah Esipisu.

Mtandao huu wa utapeli uliibuka mara kwanza katika kesi ya talaka ya mwaka 2006, baada ya Samuel Gichuru, bosi tajiri wa kampuni ya umeme ya Kenya, na mkewe Salome Njeri walipo talikiana.

Ilipofikia wakati wa kugawanya mali zao, Bi Njeri alihisi kuwa hapati mgawo wake sawa.

Alidai baadhi ya mali za mumewe zilikuwa zimefichwa ili zisisikilizwe na, kortini, aliorodhesha maelezo ya akaunti alizodai kuwa ni za Bw Gichuru huko Jersey, ambayo mara nyingi huhusishwa na akaunti za siri za nje ya nchi na mazingira ya ushuru mdogo.

Hilo lilizua uchunguzi wa miaka tisa na mamlaka ya Jersey katika maeneo 12 ya mamlaka.

Kama sehemu ya uchunguzi huo, mwaka wa 2011, walimshutumu Bw Gichuru na aliyekuwa Waziri wa Fedha Chris Okemo kwa kuchukua pesa kutoka kwa mashirika ya kimataifa ambayo yalitumwa kwa kampuni iliyosajiliwa Jersey.

Mamlaka ya Jersey ilitoa vibali vya kukamatwa kwa wanaume wote wawili na wamekuwa wakisubiri kurejeshwa Kenya tangu wakati huo.

Uhalifu wa kiuchumi waliotuhumiwa nao ni pamoja na makubaliano na kampuni ya Kifini ya kujenga kituo cha umeme karibu na Mombasa, jiji la pili kwa ukubwa nchini Kenya, na kuchukua mamilioni ya pauni kama rushwa kutoka kwa makampuni ya uhandisi ya Uingereza, Norway na Ujerumani, pamoja na kampuni kubwa ya mawasiliano ya Marekani. .

Licha ya BBC kujaribu mara kwa marakuwasiliana nao, matajiri hao na mawakili wao hawakutoa maoni yoyote kuhusu tuhuma zinazotolewa dhidi yao.

Hata hivyo mwaka 2016, kampuni iliyosajiliwa huko Jersey ya Windward Trading Limited ilikubali mashtaka manne ya utakatishaji fedha haramu katika mahakama ya Jersey.

Mahakama iliamua kwamba kampuni hiyo, ambayo mmiliki wake mkuu alikuwa Bw Gichuru, inapaswa kunyang'anywa zaidi ya dola milioni 4.9m (£3.6m) za mali kwa utakatishaji wa pesa.

Pesa hizo nyingi ndizo zinazodaiwa kutokana na ufisadi nchini Kenya kati ya mwaka 1999 na 2002 ambazo sasa zinarejeshwa nchini.

Hilo liliwezeshwa katika makubaliano ya 2018 yaliyotiwa saini nchini Kenya na Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Theresa May, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na serikali za Uswizi na Jersey.

Katika mpango huo, ilibainika kuwa mali zinazodaiwa kuibiwa zinaweza kurejeshwa nchini Kenya, mradi tu zitumike kwa miradi ya maendeleo pekee.

Mpango huu, unaojulikana kama Mfumo wa Kurudisha Mali zilizotokana na Ufisadi na Uhalifu hadi Kenya (Fracck), ulisifiwa na Umoja wa Mataifa kwa"ubunifu"

Inaipa Jersey mamlaka ya kutoa leseni ya kufungia pesa ambazo wanaamini ziliibwa na kuzirudisha kabla ya wale wanaoshutumiwa kuziiba kusomewa mashtaka.

"Swali kwetu [kwaJersey] lilikuwa: je, tungojee mchakato wa kimahakama uliovurugika kulingana na vitendo vya watu wawili, ambao... wameonekana kuwa kinyume cha sheria katika mahakama ya Jersey? Au turuhusu pesa zirudishwe kwa ajili ya manufaa ya raia wa Kenya?" Seneta Ian Gorst, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jersey, alieleza.

Kukabidhiwa kwa mamilioni ya pesa za Bw Gichuru zinazodaiwa kuibwa na kuwarudishia Wakenya wa kawaida ni mtihani wa kwanza wa Fracck.

Kuitumia kwa uwazi na uwajibikaji ni kazi kampuni ya Crown Agents, Kampuni ya isiyo ya kibiashara ya maendeleo ya kimataifa

Bosi wake Fergus Drake aliambia BBC kwamba alikuwa akiwasiliana na wizara ya afya ya Kenya ili kutathmini kile kinachohitajika katika vita dhidi ya Covid-19.

Alisema ilitaka "vifaa maalum vya maabara kupima Covid-19" na vifaa vya ziada "kama mirija ndogo, vipimo vya PCR, na vifaa vingine".

Bw Drake anatarajia kupeleka vifaa hivyo muhimu kwa nusu dazeni ya hospitali katika muda wa miezi miwili.

Alisema kuongeza upimaji kutaruhusu Wakenya kudhibiti vyema janga hili na kujua ni maeneo gani yanahitaji chanjo ya haraka.

Kwa sasa, chini ya asilimia 20 ya Wakenya wamechanjwa kikamilifu.

Bw Drake alikiri kwamba jumla ya pesa anazotoa - $3.5m - hazitafika mbali katika suala la mwitikio wa nchi kupambana na Covid-19, lakini anatumai aina hii ya msaada uliolengwa utakuwa na "athari kubwa." dhidi ya virusi.

Wanaharakati wanaamini kuwa Fracck ni kielelezo cha njia mpya ambayo faida zilizopatikana kwa njia isiyohalali zinaweza kurejeshwa.

Uingereza pia imetia saini makubaliano mengine - Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Ufisadi - hivyo inalazimika kurejesha fedha za uhalifu pale ambapo masharti ya kufanya hivyo yanatimizwa.

Lakini kulingana na mkuu wa utafiti na uchunguzi wa Transparency International (TI) Uingereza,Steve Goodrich, mapato kutoka Uingereza mara nyingi hayaendi moja kwa moja kwenye miradi ya maendeleo.

Alitaja kurejeshwa kwa pesa zilizoibiwa na Gavana wa zamani wa jimbo la Delta la Nigeria James Ibori mwaka wa 2012 ambazo zilitolewa kwa serikali ya shirikisho wa nchi hiyo ambapo kulikuwa na wasiwasi kwamba fedha zilizorudishwa zinaweza kupotea kwa rushwa.

Kwa hivyo Bw Goodrich alisema kesi hii ilikuwa "ilikuwa katika mwelekeo sahihi".

Lakini, aliongeza, kuwa na "kizuizi cha kuaminika" dhidi ya wale wanaotaka kuficha pesa zao zilizoibiwa nchini Uingereza, alisema serikali "inahitaji sana kuongeza nguvu" juu ya kurejesha mali.

Kwa mfano, alisema Uingereza inapaswa kuanza kwa kuangalia kile alichoamini ni "zaidi ya Pauni Bilioni 5-thamani ya mali ya Uingereza iliyonunuliwa kwa fedha zinazoshukiwa".

Kipindi hiki pia kinaangazia vita vya Kenya dhidi ya ufisadi nyumbani.

Nchi hiyo imeorodheshwa ya 128 duniani katika mitazamo ya TI ya ripoti ya ufisadi, huku maafisa wa umma na wafanyabiashara wakidawa kuwa tayari kwa kupokea hongo.

Imesalia miezi michache kabla ya Rais Kenyatta kumaliza muda wake madarakani, baada ya kuahidi vita dhidi ya ufisadi kuwa sehemu ya urithi wake atakaoacha.

Kama sehemu ya hayo, wanasiasa na viongozi wa umma kwa sasa wanaombwa kutangaza utajiri wao, huku kukiwa na ukaguzi wa kupambana na ufisadi.

Balozi wa Kenya Kenya nchini Uingereza, Bw Esipisu, ambaye wakati mmoja alikuwa msemaji wa rais, aliambia BBC kwamba makubaliano ya Fracck yalikuwa na "mchango mkubwa" katika ajenda ya rais kwani yalitoa ishara kwamba " wanaofamya Ufisadi hawatakuwa salama kisa wanaficha pesa zao nje ya nchi. ".

Aliongeza kwa kwamba "hizi ni fedha zilizoibiwa kutoka kwa Wakenya, zilizoporwa kutoka kwa Wakenya, na kwa makubaliano haya, fedha hizi zinarudishwa kusaidia watu wa Kenya ambao walikusudiwa mara ya kwanza. Kwa hiyo huu ni ushindi kwa watu wa Kenya."

Huku fedha hizo zikiwa njiani kutoka Jersey hadi Kenya, mtazamo pia unageukia kama kuna uwezekano wa kuwarejesha kutoka Kenya hadi Jersey washukiwa hao wawili.

Mwanzoni mwa Februari, kesi ya kuwarejesha nyumbani hatimaye ilianza katika Mahakama ya Jiji la Nairobi, baada ya mzozo wa miaka 10 kuhusu iwapo afisa mkuu wa sheria wa serikali au mwendesha mashtaka wa umma anafaa kuongoza kesi hiyo.

Idara ya mashtaka ya umma nchini Kenya sasa ndiyo inasimamia mchakato huo na Naibu Mkurugenzi wake Victor Mule alisema kusikilizwa tena kunatarajiwa kufanyika mwezi Mei.

Aliamini kuwa haitachukua miaka 10 zaidi kutatua.

Wakili wa Bw Gichuru alichagua kutozungumza lolote kuhusu mchakato wa kisheria unaoendelea alipotafutwa na BBC.

Seneta wa Jersey Bw Gorst anakubali kulikuwa na mapungufu ambayo yaliruhusu pesa hizi zinazodaiwa kuibiwa kuingia kisiwani hapo kwanza.

Aliwaonya wahusika wa siku za mbele kwamba kanuni zake zimeimarishwa lakini fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali zitapatikana na "tutazirudisha kwa raia ambao ni mali yao".