Ukraine na Urusi: Makabiliano ya NATO na Urusi yatasababisha vita vya tatu vya dunia-Biden

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Marekani, Joe Biden, alihakikisha kwamba makabiliano ya moja kwa moja kati ya NATO na Urusi yatasababisha Vita vya Tatu vya Dunia.
"Nataka kuwa wazi: Tutalinda kila nchi ya eneo la NATO kwa nguvu kamili ya NATO iliyoungana na iliyoboreshwa," Trump alitweet.
"Lakini hatutapigana vita dhidi ya Urusi nchini Ukraine. Makabiliano ya moja kwa moja kati ya NATO na Urusi ni Vita vya III vya Dunia."
Biden amekataa mara kwa mara kutuma wanajeshi wa Marekani kwa makabiliano ya moja kwa moja na Urusi.
Katika siku za hivi karibuni, utawala wake umeendesha kampeni ya vikwazo dhidi ya Vladimir Putin na nchi yake.
Mengi zaidi unayoweza kusoma
TANGAZAO LA KUIUZA CHELSEA:Chelsea: Roman Abramovich anasema ana mpango wa kuiuza klabu hiyo
MATAJIRI WENGINE URUSI:Urusi na Ukraine: Wafahamu wanaume mabilionea wa Urusi wanaokabiliwa na vikwazo vya dunia kwa kuwa na ushirika na Putin
Ijumaa hii Biden alitangaza kupiga marufuku uagizaji wa vodka ya Kirusi, almasi na dagaa.
Rais pia alidokeza kuwa atazuia mauzo ya nje ya bidhaa za anasa za Marekani, sekta ambayo inazalisha dola za Marekani milioni 550 kwa mwaka. Miongoni mwa bidhaa ambazo soko la Urusi halitaweza kupata ni saa, magari na vito vya mapambo.
Kwa njia hiyo hiyo, Marekani na washirika wake watatafuta kubatilisha hadhi ya Urusi kama mshirika wa kudumu wa kibiashara , mojawapo ya kanuni za kimsingi za biashara ya kimataifa ambazo Shirika la Biashara Ulimwenguni linaziangalia.
"Putin ni mchokozi. Ni mchokozi na lazima alipe gharama," rais Biden alisema.
"Tunaonesha nguvu zetu na hatutakata tamaa," aliongeza.

Chanzo cha picha, EPA
Inamaanisha nini kwamba Urusi sio mshirika wa biashara anayependekezwa?
Kulingana na Biden, mabadiliko haya yataruhusu nchi ya Amerika Kaskazini kuanzisha ushuru mpya kwa anuwai ya bidhaa za Urusi, ambayo itaathiri moja kwa moja uchumi wake, ambao tayari umeathiriwa na vikwazo vya Magharibi.
Marekani imefuta hadhi hii kutoka nchi nyingine mbili pekee: Korea Kaskazini na Cuba.
Wanauchumi wanasema vikwazo hivyo vitaisukuma Urusi katika mdororo mkubwa wa kiuchumi mwaka huu.
Ukraine na Canada tayari zimefanya maamuzi sawa dhidi ya Moscow. Umoja wa Ulaya, G7 na washirika wa Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) pia wanatarajiwa kujiunga.
Ingawa Biden anahitaji kuungwa mkono na Bunge la Marekani, haitarajiwi kwamba atakuwa na matatizo katika kutekeleza hatua hiyo, kwa vile anaungwa mkono na wajumbe wa chama cha Democratic na Republican katika masuala yanayohusiana na mzozo kati ya Ukraine na Urusi.
Kwa njia hiyo hiyo, rais alitangaza kwamba G7 itafanya kazi ili kufunga ufikiaji wa Kremlin kwa chanzo chochote cha ufadhili kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia.
Onyo kwa Putin

Chanzo cha picha, Getty Images
Biden pia alimuonya Rais wa Urusi Vladimir Putin kwamba atalipa "gharama kubwa" ikiwa atatumia silaha za kemikali au za kibaiolojia nchini Ukraine.
Matangazo ya Marekani yanatokea wakati Ijumaa hii iliporipotiwa kwamba jeshi linaloongozwa na Moscow lilizidisha mashambulizi yake kuelekea magharibi mwa ardhi ya Ukraine, kwa mashambulizi ya mabomu katika Lutsk na Ivano-Frankivsk, miji karibu na Poland na Moldova. Poland ni mwanachama wa NATO.
Mashambulizi pia yaliripotiwa huko Dnipro.
Kwa upande wake, Urusi ilitangaza Alhamisi kuwa itapiga marufuku usafirishaji wa bidhaa na malighafi mbalimbali kwa nchi ambazo zimeiwekea vikwazo.
Pia uwezekano wa kutaifisha mali za makampuni ya kigeni ambayo yapo katika himaya yake na ambayo yaliamua kuondoka nchini mara tu uhasama ulipoanza.














