Urusi na Ukraine: Wafahamu wanaume mabilionea wa Urusi wanaokabiliwa na vikwazo vya dunia kwa kuwa na ushirika na Putin

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali za Uingereza, Muungano wa Ulaya na Marekani zimejibu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kwa vikwazo vikali dhidi ya mabilionea wafanyabiashara wanaoaminiwa kuwa ndio wandani wa Rais Vladmir Putin.
Bw Putin amewatahadharisha washirika wake kwa miaka mingi kuwa wanapaswa kujilinda dhidi ya hatua za aina hiyo, hususan wakati ambapo mahusiano baina yake na Marekani na mataifa ya Muungano wa Ulaya yalipoharibika baada ya kuittwa Crimea.
Lakini huku baadhi ya wale walio karibu naye wakifuata ushauri wake na kuendelea kuwekeza nchini Urusi, wengine walitunza pesa zao katika biashara ya uwekezaji wa nyumba na wengine waliwekeza katika klabu za soka katika nchi za ng'ambo na kampuni zao zilibakia katika orodha ya hisa za kimataifa za ubadilishaji wa fedha za kigeni.
Sasa wamejipata wakihangaika kushikilia mali zao huku adhabu kali zaidi za kiuchumi kuwahi kushuhudia katika enzi hii zikiwekwa dhidi yao. Haya ndio tunayoyajua kuhusu baadhi ya mabilionea wa Urusi

AMEWEKEWA VIKWAZO NA : US, EU, UK
Akisemekana kuwa mmoja wa Mfanyabiashara tajiri mwenye ushawishi wa kisiasa anayependelewa zaidi na Rais Putin, Alisher Usmanov pia ni mmoja wa matajiri wa juu, akikadiriwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 17.6 , kulingana na jarida la Forbes. Zamani akiwa na taaluma ya kuweka uzio, Muungano wa EU unamuelezea kama " mfanyabiashara-rasmi" ambaye humsaidia rais kutatua matatizo yake ya kibiashara.
Akiwa mzaliwa wa Uzbekistan wakati ilikuwa bado ni sehemu ya Muungano wa Usovieti, anaendesha kampuni ya USM Holdings, inayohusika katika machimbo ya madini na mawasiliano, ikiwa ni pamoja na kampuni ya pili kwa ukubwa ya mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi - MegaFon.
Amevitaj vikwazo dhidi yake kutokuwa vya haki na akadai kuwa madai dhidi yake ni ya uongo.

Chanzo cha picha, Reuters
USM Holdings ilionekana kuwa na matumaini ya kuepuka vikwzo vya EU kwani anamiliki 50% ya hisa zake. Mashua yake kubwa iliyopewa jina la mama yake Dilbar, inakarabatiwa katika Hamburg na sasa inakabiliw ana hatari ya kushikiliwa.
Nchini Uingereza, malizake zinaoponekana ni majumba. Beechwood House, nyumba yenye thmanini ya pauni milioni 65, ikiwa katikati ya jiji, na pia nje kidogo ya London Eneo la Surrey,- anamiliki jumba la Tudor , kasri la Sutton .Majumba yite haya yamehodhiwa na mamlaka za Uingereza
Mshirika wake wa kibiashara Farhad Moshiri anamiliki klabu ya Everton, na makampuni ya Usmanov- USM, MegaFon na Yota yamekuwa wafadhili wakubwa wa klabu, huku kukiwa na madai kuwa uhusika wake ulikuwa hata ni wa karibu zaidi. Everton imesitisha mkataba wa ufadhili wake Jumatano, na Bw Moshiri aliacha kazi kama mjumbe wa bodi ya USM.

ALIYEMUWEKEA VIKWAZO: HAKUNA
Akiwa mmoja wa mabilionea wa hali ya juu wa Urusi kwasababu ya mafanikio makubwa ya klabu yake ya Chelsea FC, Roman Abramovichbado hajawekewa vikwazo, labda kwasababu ana ushawishi wa chini kuliko washirika wengine war ais Putin. Ni vipi ana ushawishi katika Kremlin ni jambo linalojadiliwa sana.
Baadhi wanasema huvumiliwa na rais Putin, wengine wanasema uhusiano wake ni zaidi ya huo.
Bw Abramovich anakanusha vikali kuwa na uhusiano wa karibu na Bw Putin au Kremlin, lakini anakadiriwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 12.4 . Jumatano alitangaza kuwa alikuwa anataka kalabu ya Chelsea kwa pauni bilioni 3 na nyumba yake kwa pauni milioni 150 iliyopo katika eneo la Kensington Palace Gardens mjini London inaripotiwa kuwekwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa.
Bw Abramovich alitengeneza fedha zake miaka ya 1990 na awali alikuwa mfanyabiashara mwenye ushawishi wa kisiasa (oligarchs ) wakati wa urais wa Bw Boris Yeltsin.

AMEWEKEWA VIKWAZO: NA MAREKANI
Wakati Rais Putin alipoingia madarakani , Oleg Deripaksa alikuwa Tajiri sana, utajiri wake ukipanda kwa takriban dola bilioni 28-lakini sasa anadhaniwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 3.

Chanzo cha picha, Kremlin/EPA
Alipigania utajiri wake kakati miaka ya 1990, na kufikia nafasi ya juu katika mapambano makali kwa ajili ya sekta ya mabati. Marekani inasema alihusika katika utakatishaji wa pesa, hongo, wizi na madai yaliyoripotiwa kwamba aliamuru ''mauaji ya mfanyabiashara, na kuhusika na kikundi cha uhalifu cha Warusi ". Anakanusha madai hayo.
Aliumia vibaya katika msukosuko wa kiuchumi wa mwaka 2008 na alimuhitaji Bw Putin amdhamini. Katika mwaka 2009, Rais Putin alimuaibisha kwa kusema wazi mbele ya umma kwamba alikuwa ameiba kalamu. Tangu wakati ule, alionekana alifanya juhudi na kurejesha upendelea kutoka kwa Putin na alielezewa katika ripoti ya Muller - uchunguzi wa Marekani kuhusu juhusi za urusi za kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016- kama mtu ambaye ni "mshirika wa karibu " wa rais
Ni muanzilishi wa kampuni ya nishati safi -green energy and metals, En+ Group, ambazo zimejisajili katika soko la hisa la London, lakini alipunguza hisa zake hadi chini ya 50% wakati aliwekewa vikwazo vya Marekani mwaka 2018.
Anamiliki sehemu kubwa biashara yake ya mapambo ya katika Hamstone House jingo lililopo Weybridge, Surrey, ambalo limekuwa likijaribu kuuzwa kwa pauni milioni 18 tangu uhusiano wa Ungereza na Urusi uingie. Pia anamiliki mashua ya kifahari , Clio, ambayo ilikuwa Maldives jumatano.

AMEWEKEWA VIKWAZO: NA MAREKANI NA MUUNGANO WA ULAYA(EU)
Uhusiano wa Igor Sechin na Vladimir Putin ni wa ndani na wa muda mrefu, kulingana na EU ambayo ilitangaza vikwazo dhidi yake tarehe 28 Februari. Anasemekana kuwa mmoja wa washauri wa karibu na wanaoaminiwa zaidi na Bw Putin, akiwa pia ni rafiki yake binafsi, na wawili hao wanadhaniwa kuwa huwasiliana kila siku.
Mafanikio yake yalipatikana kwa kuwasukuma kando wapinzani- jina lake la bandia anaitwa Darth Vader.
Bw Sechin alifanya kazi na Bw Putin katika ofisi ya meya katika St Petersburg katika miaka ya 1990, na anaaminiwa kuwa katika huduma za ujasusi zinazoogopwa zaidi - KGB, ingawa hawahi kukubali hilo wazi.
Akiwa na makao yake Urusi, hakuna anayejua ni pesa kiasi gani alizonazo.

AMEWEKEWA VIKWAZO: NA MAREKANI
Alexey Mille ni Rafiki mwingine wa zamani wa Vladimir Putin . Mwanaume huyu , pia alijenga kazi yake kwa kumuenzi Bw Putin, akianza wakati alipokuwa naibu wa Bw Putin katika kamamti ya masuala ya kigeni ya ofisi ya Meya wa St Petersburg katika miaka ya 1990.

Chanzo cha picha, Kremlin/EPA
Ameendesha mfulurizo kampuni ya taifa ya nishati ya gesi - Gazprom tangu mwaka 2001, lakini ulikuwa ni uteuzi wa kushitukiza na inaaminiwa kwa kiasi kikubwa kwamba anatekeleza tu amri za bosi wake wa zamani.
Bw Miller aliwekewa vikwazo baada ya Urusi kuitwaa Crimea katika mwaka 2014, lakini alipoongezwa kwenye orodha ya Marekani yam waka 2018 ya vikwazo alisema anajivunia . "Kwa kutojumuishwa katika orodha ya kwanza . Hata nilikuwa na shaka kiasi - labda kitu fulani hakikuwa sawa? Lakini hatimaye sasa nimejumuishwa. Hii inamaana kuwa tunafanya kila kitu sawa ," alisema.
Mali zake nje ya Urusi hazipatikani kwa urahisi na hakuna taarifa kuhusu utajiri wake kamili.

WAMEWEKEWA VIKWAZO: NA EU
Muungano wa Ulaya ulimuelezea Pyotr Aven (aliye pichani kushoto) kama mmoja wa wafanyabiashara wenye ushawishi wa kisiasa aliye karibu zaidi na Bw Putin , na MIkhail Fridman kama muwezeshaji wa wandani wa Putin. Kwa Pamoja wanaume hao wawili walibuni Alfa-Bank, ambayo ndio benki kubwa zaidi ya kibinafsi nchini Urusi.
Ripoti ya Muller ilisema kuwa Bw Aven hata alikutana na Putin katika Kremlin kama mara nne kwa mwaka , ikisema "alielewa maelezo au ukosoaji alioutoa Putin wakati wa mikutano ilikuwa ni maagizo, na yangekuwa na athari kwa Aven hata iwapo asingeyafuata ".
Walionywa na Putin mwaka 2016 kulinda maslahi yao dhidi ya vikwazo vijavyo. Wiki hii wawili hao walijiuzulu katika makao makuu ya uwekezaji wa ya London- LetterOne investment group ambayo waliukanzisha takriban miaka 10, kwasababu hisa zao zilifujwa na vikwazo vya EU tarehe 28 Februari. Bw Aven pia alijiuzulu kama mjumbe wa bodi ya taasisi ya Sanaa ya London- Royal Academy of Arts.
Wafanyabiashara hawa wawili walisema "watapinga vikali kuwekewa vikwazo hivi visivyo na msingi wowote-kwa njia zozote ziwezekanazo ".
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA: Urusi inapiga makombora katika miji iliyotangaza kusitisha mapigano Ukraine
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine












