Urusi na Ukraine: Ifahamu kambi ya kijeshi ya Urusi yenye uwezo mkubwa wa kijeshi iliyoijenga juu ya dunia

Soldado ruso
Muda wa kusoma: Dakika 5

Urusi imekuwa ikishutumiwa kwa kupanga kutumia silaha kali aina ya thermobaric - zinazofahamika pia kama mabomu ya vacuum, mabomu ya cluster na kwamba huenda ikawa inajiandaa kwa mashambulio ya nyuklia -katika vita vyake dhidi ya Ukraine, licha ya kwamba wataamu na wachambuzi wanapinga uwezekano wa mashambulio ya nyuklia.

Hatahivyo, tisho la uwezo wa kijeshi wa Urusi limekuwepo, kabla ya mashambulio ya uvamizi wa utawala wa Rais Putin dhidi ya Ukraine. Tangu awali Putin ameonekana kuwa amekuwa akijiandaa kwa vita vikubwa hususan kwa kuyajengea uwezo majeshi yake ya anga, majini na nchi kavu.

Inaaminiwa kuwa Urusi imejenga kambi kubwa ya kijeshi katika eneo la juu kabisa la dunia- kwenye katika Arctic iliyoyatia kiwewe mataifa ya magharibi.

Ardhi ya Franz Josef ni makao ya ngome ya jeshi la Urusi na chanzo cha kuwepo kwa mahusiano ya wasiwasi zaidi na nchi za magharibi.

Marekani imekuwa ikiishutumu mara kwa mara serikali ya Urusi kwa kuilifanya eneo la juu ya dunia yaani mzingo wa Arctic kuwa la ''kijeshi''.

Kujibu hayo, Mkuu wa kikosi cha Urusi cha manowari za kaskazini aliiambia BBC kwamba shughuli za Umoja wa Kujihami wa nchi za Magharibi (NATO) na jeshi la Marekani katika eneo hilo "bila shaka " ni za uchokozi na zimefikia kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu Vita vya Pili ya Dunia.

Arctic, kipaumbele cha Urusi

Waandishi wa BBC walikuwa miongoni mwa waandishi wa habari wa kwanza wa kigeni kukaribishwa kutembelea kisiwa cha Alexandra, uliopo mwendo wa saa mbili kwa safari ya ndege kutoka mji wa Murmansk juu ya Arctic.

Arctic, ambayo ni bahari ndogo zaidi ya bahari tano za dunia, ni mahali penye hali ya hewa isiyo na huruma katika sayari ya dunia, kuna baridi kali linalolindwa na barafu mwaka mzima.

Alambre de púas en la base rusa

Kiwanja kidogo cha ndege kimeboreshwa ili kuruhusu aina azote za ndege kutua katika kipindi chochote cha majira ya mwaka.

Na kwenda nje ya barabara ilikuwa ni kama kuteleza kwenye barafu.

Chini ya kilomita 960 chini ya ncha ya Kaskazini zaidi ya dunia hali ya hewa ni baridi kupita kiasi.

Mvua ya barafu hunyesha hata saa sita mchana.

Katika baridi kali, viwango vya joto hushuka hadi chini ya nyuzi joto hasi 50 na wanajeshi wanalazimika kuondosha kwa muda magari yao kwenye eneo hili ili kuwatawanya dubu ambao ni maarufu wanaozurura karibu na ngome ya jeshi.

Militares rusos en Franz Josef Land

Hata hivyo, licha ya hali ya hewa mbaya juhudi za kuongeza uwepo wake katika eneo hilo limekuwa ni jambo la kipaumbele kwa Urusi.

"Kama kituo cha anga za mbali "

Hata muundo wa ngome unataka kuweka wazi masuala machache: imepakwa rangi za bendera ya Urusi na inaonekana kwa rangi zake dhidi ya turubai jeusi linaloizingira.

Umbo lake lina sura tatu, ngome hii ni ya pili ya aina yake katika eneo la Arctic na inaweza kuwapokea hadi askari 150

Base ártica de Rusia

Kabla ya kuwaonesha wanahabari kila kitu, kamanda mkuu alisema kambi hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu na ina ufanisi wa kutosha wa kiikolojia na kwamba ni "kama kituo cha anga za mbali, katika eneo tu la Arctic badala ya obiti."

Lakini onyesho lenyewe liko nje, ambako mitambo ya kurusha makombora ya Bastion inapanda na kushusha mashine zake za kufyatua huku mwanajeshi aliyevalia magwanda meupe ya kujificha akiwa amesimama kwenye eneo la ulinzi mkali akiwa na bunduki mkononi na pisto kwenye kifua chake.

Makombora ya Bastion

Mifumo ya makombora ni ya "kuharibu meli za adui," alisema mwanajeshi mwingine.

Ina "ufanisi mkubwa" alisema.

Avión ruso después de aterrizar en el Ártico

Kikosi cha kaskazini kilionesha uwezo wake wa kijeshi mapema mwaka huu wakati mauari tatu za nyuklia zilipovunja barafu kwa wakati mmoja, ujanja ambao haukuwahi kushuhudiwa kabla.

Katika mazoezi hayo hayo ya Arctic, ndege mbili za mapigano aina ya jet zilipaa juu ya Ncha ya Kaskazini, na kuongezewa mafuta angani.

Ujanja huu wa kijeshi unaifanya Marekani na NATO kuwa makini na uwepo wa wanajeshi wa Urusi katika kanda iliyopanuka kwa kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu wakati wa Vita Baridi.

Msemaji wa NATO alithibitisha kwamba muungano huo umeanza doria na mazoezi, kujibu alichosema "mazingira yenye changamoto zaidi kiusalama."

Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi

Ilaumu NATO

Lakini Urusi haitazami jambo hilo kama waonavyo Nato.

Kabla kutembelea kambi hiyo, waandishi hao walitembelea manowari kubwa yeye urefu wa mita 252. Meli hiyo inayoendeshwa kwa nguvu za nyuklia inaitwa Pedro, the Great ni meli kuu na muhimu ya jeshi la Kaskazini la Urusi.

Akiwa ndani ya meli hiyo, kamanda wa vikosi vya kaskazini, Admiral Alexander Moiseyev, alizungumza na waandishi mbele ya picha ya mchoro wa Peter I, muasisi wa jeshi la Urusi la wanamaji na aliielekeza nchi hiyo katika mifumo ya kimagharibi.

Pedro, el Grande

Kamanda huyo alivishutumu vikosi vya NATO na Marekani kwa vitendo vyao katika eneo la Arctic na kudai vinaongeza hatari ya mzozo.

"Hapajawahi kuwa na uwepo mkubwa sana hapa wa vikosi vyao kwa miongo sasa. Ninaweza kusema tangu Vita kuu ya pili ya dunia," alijibu Mkuu wa kikosi Admiral Moiseyev, alipoulizwa na BBC kuhusu NATO kuilaumu Urusi kwa kuongeza hali ya wasi wasi.

"Tunaona shughuli hizi zikiwa karibu sana na mpaka wa Urusi, ambako tuna mali muhimu sana kama uchokozi. Kwa hili, ninamaanisha silaha za nyuklia."

Mwaka jana Urusi iliwarejesha wanajeshi wake katika eneo hilo ambalo ililiacha katika miaka ya 1990 wakati Muungano wa Usovieti ulipovunjika.

Map of Arctic
1px transparent line

"Tunaongeza tu uwezo wa kulinda mipaka yetu, sio kumtishia yeyote," anadai Lev Voronkov, mtaalamu wa eneo la Arctic katika Chuo Kikuu cha MGIMO.

"Baada ya kuvunjika kwa USSR, hata vituo vya mpaka katika kanda ile viliachwa bila wahudumu ."

Hilo halitafanyika kwa muda mrefu zaidi.

Ardhi yenye fursa

Huku barafu ikiyeyuka kuondoa pazia ya kinga asilia katika eneo hilo la ncha ya dunia, mpaka mrefu wa kaskazini wa Urusi utakuwa katika hatari zaidi.

Wakati makombora ya Bastion yakifyatuliwa na kucheza mbele ya kamera katika kisiwa cha Alexandria, mpasuaji wa barafu wa Urusi alikuwa akipita katikati ya barafu iliyoganda kwa umbali. Ndege ndogo ya mizigo ikafuata na mlima wa barafu ukajitokeza nyuma yao.

Rompehielos en el Ártico

Meli zilikuwa zinapita kwenye eneo la bahari ya kaskazini linalozingira visiwa vidogo na ambavyo Urusi inatumaini kulijenga na kulidhibiti kama ongezeko la joto duniani litawezesha shughuli hizo.

Biashara zitajumuisha mauzo ya nje kutoka hifadhi kubwa ya mafuta na gesi iliyopo hapa chini ya bahari.

Admiral Moiseyev anasema kwamba , zaidi ya mipaka ya Urusi , vikosi vyake "ni muhimu" katika kulinda maslahi hayo ya kiuchumi.

Huku mashindano yakianza kuongezeka, ziara yetu katika ardhi ya Franz Josef ilikuwa ni fursa ya Urusi ya kuonesha nguvu zake na kutuma ujumbe: Kwamba tamaa yake kwa Arctic ni kubwa na inaongezeka na kwamba wana maslahi ambayo wamejiandaa kuyalinda.

Raya