Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je ni kwanini sehemu ya ndani ya dunia inapoa kwa kasi na yapi madhara yake?
Ikiwa umewahi kuambiwa "Ninahisi kama baridi inaendelea kuongezeka," unajua kuna kitu hakiko sawa.
Vivyo ndivyo ilivyo kwa sehemu ya ndani ya sayari ya Dunia, ambayo ina msingi ambao umekuwa moto sana kwa zaidi ya miaka bilioni 4.5, lakini inapoa polepole na hilo haliwezi kuepukika.
Sehemu ya ndani ya Dunia ndio msingi wa uhai, kwa hivyo ikiwa itakuwa giza, sayari yenyewe itageuka kuwa mwamba mkubwa, baridi sana.
Sasa, katika utafiti wa hivi majuzi, timu ya wanasayansi imekokotoa kuwa mchakato wa kupoa kwa dunia unafanyika haraka kuliko ilivyofikiriwa hapo awali.
Hali hii ya kupoa au kuwa baridi hutokea katika kipindi cha mabilioni ya miaka, kwa hivyo haijalishi kunatokea kwa haraka kiasi gani, hakuna hata mmoja wetu atakayekuwa hai kuona jinsi baridi mbaya zaidi ya sayari ingefanana.
Wataalamu, hata hivyo, wanakubali kwamba kuchunguza michakato hii ya asili ni muhimu kuelewa vyema mabadiliko ya Dunia na matukio yanayoathiri maisha kwenye sayari.
Kupoa huku ni nini na waligunduaje kuwa hali hiyo inatokea haraka kuliko ilivyofikiriwa hapo awali?
Sehemu ya ndani ya sayari ya Dunia
Sehemu ya ndani kabisa ya Dunia ni eneo ambalo liko karibu kilomita 3,000 ndani ya tabaka la juu la Dunia, na eneo la kilomita 3,500.
Halijoto kuu inaweza kubadilika kati ya 4,400°C na 6,000°C, halijoto inayofanana na ile ya Jua.
Eneo la ndani kabisa ni tufe thabiti, inayojumuisha zaidi chuma.
Sehemu ya nje imeundwa na kioevu inachojumuisha chuma na nikeli.
Sehemu ya nje ndio inayotengeneza ugasumaku, ambayo inalinda sayari kutokana na upepo hatari wa jua.
Kiasi kikubwa cha nishati ya joto inayotoka ndani ya sayari hutengeneza matukio kama vile miamba ya dunia na shughuli za volkeno.
Kwa kuongeza, mchakato hutokea kwenye mpaka wa sehemu ya ndani ambao ulikuwa muhimu katika utafiti mpya: ambao unahusu uhamisho wa joto kutoka sehemu ya ndani hadi nje.
Shinikizo na joto
Wanasayansi hawajui kwa hakika itachukua muda gani kwa Dunia kupoa hadi kiwango ambapo matukio asilia ambayo hutokea ndani kabisa yatakoma kutokea, au kwa uga wa sumaku kutoweka, kwa mfano.
Timu kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Shirikisho la Uswizi huko Zurich na Taasisi ya Sayansi ya Carnegie, nchini Marekani, zinaamini kwamba kufumbua fumbo hili kunategemea madini ambayo husafirisha joto kutoka sehemu ya chini hadi juu.
Eneo hili la mpaka linaundwa hasa na madini yanayoitwa 'bridgmanite', ambayo ina muundo imara na angavu na inaweza kuwepo tu chini ya shinikizo kubwa, kuanzia kwa kina cha kilomita 700.
Hakuna teknolojia iliyopo ya kuchimba na kuchunguza madini kwa kina hicho, kwa hivyo profesa wa Taasisi ya Teknolojia ya Shirikisho la Uswizi huko Zurich Motohiko Murakami alibuni jaribio la kuiga hali hizo katika maabara.
Shinikizo na joto
Murakami na wenzake walibuni mbinu ya kupima ni kiasi gani cha joto kinachoweza kutengeneza madini ya bridgmanite.
Walichofanya ni kutengeneza almasi ya bridgmanite kutokana na hiyo yenyewe.
Kisha waliingiza kipande kile angavu na imara kwenye kifaa ambacho huiga shinikizo na halijoto iliyo ndani ya Dunia.
Ndani ya kifaa hicho, walirusha mapigo ya miale ya leza ambayo ilitengeneza mnunurisho na kuchoma madini hayo.
Kwa njia hiyo, wangeweza kuona jinsi madini hayo yalivyobadilika kwa shinikizo na halijoto tofauti.
"Mfumo huu wa kipimo uliweza kuonyesha kuwa upitishaji wa joto wa madini ya bridgmanite ni karibu mara 1.5 kuliko ilivyodhaniwa hapo awali," Murakami anasema katika taarifa.
Kulingana na mtafiti, hii inaonyesha kuwa joto kutoka eneo la ndani hadi eneo la juu pia ni la juu zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo awali.
Matokeo ya jaribio yanaonyesha kuwa jinsi joto linavyohamishwa haraka kutoka eneo la ndani, ndivyo joto linavyopoa haraka sana kutoka eneo la chini, hatua ambayo ina harakisha kupoa kwa Dunia.
Zaidi ya hayo, waandishi wanaamini kuwa kupozwa huku kungebadili muundo kwenye tabaka la dunia.
Wakati madini ya bridgmanite yanapoa, yanageuka kuwa madini mengine inayoitwa 'post-perovskite'.
Post-perovskite hupata joto haraka zaidi kuliko bridgmanite, kwa hivyo kama bridgmanite kwenye mpaka wa eneo la tabaka la juu inabadilika na kuwa post-perovskite, Dunia ingepoa hata kwa haraka zaidi, watafiti wanasema.
Je imekusudiwa kufa?
Kupoa huku kwa haraka kunaweza kuwa na matokeo kadhaa, waandishi wa utafiti wanabainisha.
Kwa jambo moja, inaweza kusababisha miamba mikuu yaani (tectonic plates), ambayo huwekwa kwa mwenendo na mtiririko wa mnunurisho, na kupungua kwa kasi zaidi kuliko inavyotarajiwa.
"Matokeo yetu yanaweza kutupa mtazamo mpya juu ya mabadiliko ya mienendo ya Dunia," anaelezea Murakami.
Murakami, hata hivyo, anaonya kwamba kwa wakati huu hawawezi kukadiria itachukua muda gani kupoa huko kwa dunia ili kuzuia shughuli katika eneo la juu la dunia.
Kwa kufanya hivyo, wanahitaji kuelewa vyema mienendo ya eneo la juu la dun
"Utafiti huu unatoa mtazamo mpya wa mchakato mkuu wa kijiolojia unaoathiri sayari zenye miamba (kama Dunia): kasi ya kupoa," anasema Paul Byrne, profesa wa Sayansi ya Sayari na Dunia katika BBC Mundo.
"Mihiri, Zebaki na Mwezi zimepoa sana katika kipindi cha miaka bilioni 4.5 hivi kwamba, kwa kusema kijiolojia, kimsingi hazina tena nguvu.
Kwa hiyo, tofauti na Dunia, Mihiri, Zebaki na Mwezi hazina miamba ya dunia, anaelezea mtaalam.
"Je, hiyo ndiyo hatima inayongojea ulimwengu wetu? ", maajabu ya Byrne.