James Franco akiri kulala na wanafunzi wake wa chuo cha uigizaji

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mwigizaji James Franco amekiri kufanya mapenzi na wanafunzi wa shule yake ya uigizaji, takriban miaka minne baada ya madai ya utovu wa kingono kutolewa.

Alikubali kulipa $2.2m (£1.6m) mwezi Julai baada ya kushtakiwa kwa kujihusisha na "tabia ya kuwahusisha na ngono wanafunzi wa kike".

Akiongea kwenye The Jess Cagle Podcast, alisema kuwa alipokuwa akifundisha, "alilala na wanafunzi, na hiyo haikuwa sawa".

Alisema hajaanzisha shule hiyo ili kuwarubuni wanawake kwa ajili ya ngono.

Muigizaji huyo alisema alikaa kimya kwa muda mrefu kwa sababu "kuna watu walinikasirisha na nilihitaji kusikiliza".

Sarah Tither-Kaplan na Toni Gaal, ambao walisoma shule ya uigizaji ya Franco ya Studio 4 ambayo sasa imefungwa , walidai Franco alijaribu "kuunda bomba la wanawake vijana ambao walifanyiwa unyanyasaji kibinafsi na kitaaluma kijinsia kwa jina la elimu".

Kesi ya pamoja - iliyowasilishwa Los Angeles mnamo 2019 - inadaiwa alitumia vibaya nafasi yake na kuzitumia fursa za majukumu katika filamu zake kama chambo cha kuwanasa wasichana hao.

Katika kesi hiyo, wanafunzi walidai kuwa ni waathiriwa wa udanganyifu wa kulipia shule ya uigizaji huku wakidhulumiwa kingono na kutishwa.

Madai hayo yalipoibuka mara ya kwanza, Franco alisema "sio sahihi".

Lakini hatimaye malipo yalifanywa kwa Bi Tither-Kaplan na Bi Gaal, pamoja na wanafunzi wengine ambao waliwasilisha malalamiko.

Katika nukuu za podikasti hiyo zilizowekwa hadharani Jumatano, Franco, 43, alisema amekuwa akipata nafuu kutoka kwa uraibu wa ngono tangu 2016 na "amekuwa akifanya kazi nyingi" baada ya tuhuma dhidi yake "na kubadilisha nilivyokuwa".

"Nadhani wakati huo, mawazo yangu yalikuwa kama yanakubalika, sawa," aliiambia podcast kwenye SiriusXM.

Maoni hayo ni jaribio la kwanza la mwigizaji huyo kuzungumzia madai hayo kwa kire

Alipoulizwa ni jinsi gani hangeweza kufahamu athari ya mienendo yake kati ya mwalimu na mwanafunzi kupotosha dhana ya ridhaa, Franco alijibu: "Wakati huo, sikuwa na ufahamu wa wazi."

Franco aliteuliwa kuwa muigizaji bora katika tuzo za Oscars mnamo 2011, kwa jukumu lake la kuigiza katika 127 Hours, ambayo ilielekezwa na Danny Boyle.fu.