Afrika Kusini: Nchi ambayo iliharibu silaha zake za nyuklia

Frederick William de Klerk, Rais wa Afrika Kusini, alimaliza mpango wa nyuklia wa nchi yake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Frederick William de Klerk, Rais wa Afrika Kusini, alimaliza mpango wa nyuklia wa nchi yake

Mnamo Machi 24, 1993, aliyekuwa rais wa Afrika Kusini wakati huo Frederick William de Klerk alithibitisha kile ambacho kilikuwa kilikuwa uvumi kwa miaka kadhaa.

Aliambia ulimwengu kwa nchi yake ilikuwa ikifanyia kazi mradi wa kisiri na ilikuwa inamiliki silaha za nyuklia.

Katika hotuba iliyotolewa Bungeni, Rais aliambia nchi na ulimwengu kuwa Afrika Kusini imeunda mabomu sita ya atomiki.

Pia alikariri kuwa mabomu hayo yameharibiwa na kwamba mpango wa nyuklia wa nchi hiyo umesimamishwa kabisa kwa mahitaji ya kijeshi.

Afrika Kusini ikawa sehemu ya NPT (Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Nyuklia) wa Umoja wa Mataifa mnamo Julai 1991.

De Klerk pia alipatia shirika la nyuklia la Umoja wa Mataifa (IAEA) kibali cha kufika eneo la nyuklia ili kuchunguza madai yake.

Alisema shirika hilo linaweza kutembelea maeneo yote ya nyuklia nchini Afrika Kusini ili kuthibitisha madai yao.

Pia unaweza kusoma:-

Kutokana na tangazo hilo, de Klerk aliijumuisha Afrika Kusini katika makundi machache ya nchi ambazo ziliunda silaha za nyuklia. Pia, Afrika Kusini ikawa nchi pekee iliyoacha kabisa silaha za nyuklia kabla ya kuwa sehemu ya mkataba wa NPT.

Katika miaka ya 1990, Ukraine pia ilikubali kuharibu silaha zake za nyuklia. Lakini silaha hizo zilirithiwa na Muungano wa zamani wa Kisovieti.

Lakini swali ni je, Afrika Kusini ilitengeneza vipi mabomu ya atomiki na kwa nini iliamua kuyaangamiza?

Mpango wa nyuklia kwa madhumuni ya amani

Afrika Kusini ilikuwa ikitengeneza mpango wa nyuklia kwa kutumia teknolojia yake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Afrika Kusini ilikuwa ikitengeneza mpango wa nyuklia kwa kutumia teknolojia yake

Afrika Kusini ilianzisha Bodi ya Nishati ya Atomiki kwa kutunga sheria mwaka wa 1948. Madhumuni yake yalikuwa kuchunguza uwezekano wa nishati ya nyuklia.

Mapema miaka ya 1960, Afrika Kusini ilianza shughuli za utafiti na maendeleo, na kiwanda cha nyuklia cha Pelindaba kilianzishwa takriban kilomita 40 kutoka mji mkuu, Pretoria.

Katika awamu hiyo ya kwanza ya mpango wa nyuklia lengo lilikuwa la amani. Afrika Kusini pia ina akiba ya madini ya uranium. Kazi pia ilianzishwa kutafuta njia za kurutubisha madini hiyo muhimu.

Teknolojia ya urutubishaji wa Uranium ni muhimu katika uundaji wa silaha za nyuklia.

Pia unaweza kusoma:-

Baada ya kutiwa moyo na mafanikio ya awali katika miaka ya 1960, serikali ilianzisha mtambo wa majaribio kufanya kazi kwa kiwango cha viwanda.

Mnamo 1970, Waziri Mkuu wa wakati huo BJ Vorster aliarifu Bunge kuhusu mipango hiyo na kusema kwamba mpango wa nyuklia wa nchi hiyo ulikuwa kwa madhumuni ya amani.

Afrika Kusini ilikuwa na akiba kubwa ya uranium na ilikuwa ikielewa kuwa faida za kiuchumi zingeweza kufikiwa kutokana na urani iliyorutubishwa katika siku zijazo.

Kutokana na hilo, nchi pia ilianza kuchunguza uwezekano wa kutengeneza vilipuzi vya nyuklia kwa madhumuni ya kiraia.

Mwaka 1974, baada ya kugundua kwamba mafanikio yanaweza kupatikana katika kutengeneza silaha, serikali iliidhinisha mradi huo wa siri.

Hata hivyo, mipango huo uligeuka kuwa utengenezaji wa silaha za nyuklia kwa madhumuni ya kijeshi. Nini kilitokea?

Ulinzi wa silaha

Cuba ilituma wanajeshi kuunga mkono utawala wa Kimaksi nchini Angola katika miaka ya 1970-80

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cuba ilituma wanajeshi kuunga mkono utawala wa Kimaksi nchini Angola katika miaka ya 1970-80

Kama alivyosema de Klerk katika hotuba yake ya 1993, uamuzi wa Afrika Kusini wa kutengeneza silaha za nyuklia ulianza mnamo 1974. Hii ilitokana na tishio lililoletwa na upanuzi wa vikosi vya Soviet huko Afrika Kusini.

Hali ya wasiwasi ililiyotokana na mkataba wa Warsa, shirika la nchi zenye mtazamo wa kikomunisti, pia ilikuwa chanzo cha Afrika Kusini kuunda silaha za nyuklia.

Kubadilika kwa hali ya usalama barani Afrika pia kuliathiri uamuzi wa Afrika Kusini.

Idadi ya vikosi vya Cuba nchini Angola ilikuwa ikiongezeka. Afrika Kusini ilihisi kuwa inahitaji silaha ya kinga. Nchi ilitengwa katika ngazi ya kimataifa pia.

Rais aliliambia bunge kuwa nchi yake haiwezi kutegemea misaada kutoka nje iwapo kutatokea shambulio.

Afrika Kusini pia ilitengwa kimataifa kwa sababu ya sera yake ya ubaguzi wa rangi na ilikuwa ikipigwa marufuku kununua silaha.

Marekani ilizuia ubadilishanaji wa taarifa za silaha za nyuklia na Afrika Kusini. Mnamo 1978, Marekani ilipitisha sheria ambayo teknolojia ya nyuklia haiwezi kutolewa kwa nchi ambazo hazikuwa sehemu ya NPT (Mkataba wa Kuzuia Uenezaji).

Hatari iliyofichwa

Afrika Kusini ilihofia kuwa huenda ikashambuliwa na vikosi vya mrengo wa kushoto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Afrika Kusini ilihofia kuwa huenda ikashambuliwa na vikosi vya mrengo wa kushoto

Wakati wa Vita Baridi , ulimwengu uligawanyika mara mbili na Afrika Kusini haikuungwa mkono na Afrika Kusini haikuungwa mkono na mojawapo ya mataifa makubwa mawili ya zama hizo, Marekani na Urusi.

Mwaka 1977, wakati Afrika Kusini ilipojiandaa kwa majaribio ya kisiri ya silaha zake za nyuklia, Marekani na Muungano wa Kisovieti uliikomesha.

Katika mazingira haya, serikali ya Afrika Kusini ilifikia uamuzi kwamba inapaswa kutengeneza bomu la atomiki kwa usalama wake, na Aprili 1978, serikali ya Afrika Kusini ilipitisha mkakati wa hatua tatu wa kuzuia nyuklia.

Cha kwanza kati ya haya ilikuwa ni kuweka mashaka juu ya uwezo wa nyuklia wa nchi, yaani, haipaswi kukubaliwa au kukataliwa.

Awamu ya pili ilikuwa itekelezwe wakati kulikuwa na tishio dhidi ya Afrika Kusini.

Katika mazingira hayo, iliamuliwa kuwa nchi yenye nguvu kama Marekani ingeambiwa faraghani kwamba Afrika Kusini ina silaha za nyuklia. Hii ingesaidia kimataifa kumaliza tishio hilo.

Ikiwa tishio hili halitaisha, iliamuliwa kuwa Afrika Kusini ingekubali hadharani kuwa ina silaha za nyuklia. Wakati huo huo, iliamuliwa pia kwamba bomu hilo lingejaribiwa kisiri.

Hata hivyo, iliamuliwa kuwa Afrika Kusini haitatumia bomu kwa fujo kwani inaweza kusababisha athari kubwa ya kimataifa.

Nelson Mandela aliyeachiliwa huru na F.W. de Klerk baadaye alikuwa rais

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nelson Mandela aliyeachiliwa huru na F.W. de Klerk baadaye alikuwa rais

Ili kutekeleza mkakati huu, Afrika Kusini ililazimika kutengeneza angalau mabomu saba ya atomiki.

La kwanza liliundwa mwaka 1982. Lakini la saba halikuwahi kutengenezwa.

Kiuhalisia, mkakati huo wa Afrika kusini haukuendelea zaidi ya awamu ya kwanza.

Inakadiriwa kuwa mabomu haya yalikuwa na uwezo sawa na mabomu yaliyorushwa na Marekani huko Hiroshima na Nagasaki nchini Japan na yalipaswa kurushwa kutoka kwa ndege.

Silaha za kujiangamiza

Lakini kwa nini Afrika Kusini iliamua kuharibu mabomu yake ya atomiki?

Kulingana na Rais de Klerk, sababu zilifichwa kutokana na hali ya kisiasa za kimataifa ya miaka ya 1980.

Katika hotuba yake bungeni, alitaja usitishaji vita nchini Angola, kuondolewa kwa wanajeshi 50,000 wa Cuba kutoka Angola na makubaliano ya pande tatu za uhuru wa Namibia. Kando na hayo, pia alitaja kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, kumalizika kwa Vita Baridi na kuvunjika kwa Muungano wa Kisovieti.