Ufugaji wa pweza duniani waingia utata, Je unapaswa kuendelea?

Chanzo cha picha, Getty Images
Taarifa za kuwa ufugaji wa kwanza wa Pweza kwa ajili ya biashara duniani kuwa unakaribia kuanza zimepokelewa kwa masikitiko na wanasayansi na wanaharakati wa mazingira na maliasili.
Wanasema kuwa viumbe wenye akili "wenye hisia" ambao wanaweza kuhisi maumivu na kuwa na hisia hawapaswi kamwe kukuzwa kwa ajili ya biashara ya chakula.
Stacy Tonkin ni miongoni mwa timu ya watu watano wanaosimamia mantanki maalumu ya kutunzia samaki -Aquarium katika mji wa Bristol nchini Uingereza, amekuwa akicheza na Pweza mkubwa wa Pasifiki anayejulikana kama DJ ikiwa ni kifupi cha Davy Jones kama sehemu ya kazi yake.
Stacey Tonkin amekuwa akimshushudia Pweza DJ akionesha hisia tofauti tofauti kwa kila mtu kama vile kukaa kimya na kumshika mkono kwa kutumia mikono yake (tentacles)

Chanzo cha picha, BRISTOL AQUARIUM
Pweza wanaishi hadi miaka minne kwa hivyo, akiwa na mwaka mmoja ni sawa na kusema ni kijana.
"Hakika anaonyesha jinsi unavyotarajia kijana awe, siku zingine ana huzuni na analala siku nzima, siku zingine ni hufurahi sana na anakuwa na shughuli nyingi"
Wafugaji huwalisha pweza Kome na kamba na vipande vya samaki na kaa. Muda mwingine huweka chakula katika vyombo vya mbwa ili acheze na zile mbawa zake (tentacles)kuonesha ujuzi wake wa kuwinda
Anasema rangi yake hubadilika kutoka na hali aliyokuwa nayo na hisia zake. anapokuwa na rangi ya chungwa na kahawia anakuwa na shuhuli na michezo mingi lakini anapokuwa na madoa madogo na mabaka yenye rangi anakuwa na hamu ya kutaka kujua zaidi
"Hivyo ataogelea akiwa kama ana rangi ya chungwa na kahawia kisha atakuja kukaa kando yako huku akikuangalia tu na kubadilika kuwa na madoa madogo madogo kitu ambacho ni cha kushangaza"

Chanzo cha picha, STACEY TONKIN
Stacy anasema Pweza anaonesha uwezo wa akili kupitia macho yake "pale unapomuangalia na anapokuangalia, unaweza kuhisi kuna kitu hapo" aliongeza Stacy
Kiwango cha ufahamu ambacho Stacey anashuhudia moja kwa moja kitatambuliwa katika sheria za Uingereza kupitia marekebisho ya Mswada wa Ustawi wa Wanyama (Sentience).
Mabadiliko yanakuja baada ya timu ya wataalamu kuchunguza tafiti zaidi ya 300 za kisayansi na kuhitimisha kuwa pweza walikuwa "viumbe wenye hisia" na kulikuwa na "ushahidi mkubwa wa kisayansi" kuwa wanaweza kupata raha, msisimko na furaha lakini pia wanapata maumivu, mawazo na madhara.
Waandishi wa tafiti walisema kuwa wana uhakika kwamba ufugaji wa pweza wa ustawi wa juu hauwezekani na serikali inatakiwa kufikiria kupiga marufuku kuagiza kutoka nje ya nchi pweza wanaofugwa katika siku zijazo.
Mikono (tentacles) ya pweza hutengwa kwenye sufuria, hupakuliwa kwenye sahani na kuelea kwenye supu ulimwenguni kote kutoka bara Asia hadi Mediterania, na zaidi hasa nchini Marekani na wakati mwingine katika nchi ya Korea Kusini, viumbe hawa huliwa wakiwa hai.
Idadi ya Pweza wasiofugwa inapungua na bei inapanda. Inakadiriwa tani 350,000 hukamatwa kila mwaka ikiwa ni zaidi ya mara 10 ya idadi iliyopatikana mnamo 1950.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutokana na hali hiyo, ugunduzi wa siri ya ufugaji wa Pweza wakiwa kifungoni zimekuwa zikiendelea kwa miongo kadhaa. Ni vigumu kwani hula mabuu na wanahitaji mazingira yaliyodhibitiwa kwa uangalifu.
Kampuni ya Uhispania, Nueva Pescanova (NP) imezishinda kampuni za Mexico, Japan na Australia, katika kinyang'anyiro cha ufugaji wa pweza hao na imetangaza kwamba itaanza kuuza pweza wanaofugwa msimu ujao wa joto ili kuwauza mnamo mwaka 2023.
Kampuni hiyo ilitumia utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kihispania ya Oceanographic (Institute Espagnol de Oceanografia), ikiangalia tabia za kuzaliana kwa Pweza aina ya vulgaris.

Chanzo cha picha, Getty Images
Eneo la ufugaji wa Pweza hao wa kibiashara la Nueva Pescanova NP litakuwa ndani ya nchi karibu na bandari ya Las Palmas katika Visiwa vya Canary hii ni kulingana na jarida la PortSEurope.
Inaripotiwa kuwa shamba hilo litazalisha tani 3,000 za Pweza kwa mwaka. Kampuni hiyo imenukuliwa ikisema itasaidia kukomesha pweza wengi wasiofugwa kuchukuliwa.
Kampuni ya Nueva Pescanova imekataa kuiambia BBC maelezo yote juu ya mazingira na hali gani ambayo Pweza hao watahifadhiwa ikiwemo ukubwa wa mizingira, chakula watakachokula na jinsi watakavyouawa vyote vimekuwa ni siri.
Mipango hiyo imeshutumiwa na kundi la kimataifa la watafiti kuwa haifai kimaadili na kiikolojia. Kundi la Compassion in World Farming (CIWF) limeziandikia serikali za nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Uhispania likizitaka kupiga marufuku mpango huo
"Mtu yeyote ambaye ametazama makala ya filamu ya mwaka 2021 iliyoshinda tuzo ya Oscar My Octopus Teacher atakubaliana na hilo" alisema Dr Elena Lara wa CIWF
Pweza wana akili kubwa, ufahamu wao umethibitishwa katika majaribio mengi ya kisayansi. Wameonekana wakitumia magamba ya bahari na nazi kujificha na kujilinda na wameonyesha kuwa wanaweza kujifunza kazi zilizowekwa haraka, wameweza pia kutoroka kutoka kwenye maji na kuepuka mitego iliyowekwa na watu wanaovua.
Binadamu na pweza wametoka katika kizazi kimoja ambapo miaka milioni 560 iliyopita walikuwa na uhusiano na babu mmoja na mwanabiolojia Dk Jakob Vinther kutoka Chuo Kikuu cha Bristol pia ana wasiwasi.
"Tuna mfano wa kiumbe ambacho kimebadilika na kuwa na akili ambayo inalinganishwa sana na yetu uwezo wao wa kutatua matatizo, uchezaji na udadisi ni sawa na ule wa wanadamu" asema Dk Vinther
Kampuni ya Nueva Pescanova inasema kwenye tovuti yake kwamba imejitolea kikamilifu katika ufugaji wa samaki kama njia ya kupunguza shinikizo kwenye maeneo ya uvuvi na kuhakikisha rasilimali endelevu, salama, zenye afya na kudhibitiwa, inayosaidia uvuvi.
Lakini Dk Lara wa CIWF anahoji kuwa hatua za kampuni ya NP ni za kibiashara tu na hoja ya kampuni kuhusu mazingira haina mantiki.
Pweza ni wanahitaji kula mara mbili hadi tatu ya uzito wao wenyewe katika chakula ili kuishi. Hivi sasa karibu theluthi moja ya samaki wanaovuliwa kuzunguka sayari wanageuzwa kuwa chakula cha wanyama wengine na takriban nusu ya kiasi hicho huenda kwenye ufugaji wa samaki. Kwa hivyo pweza anayefugwa angeweza kulishwa kwa bidhaa za samaki kutoka kwenye hifadhi ambazo tayari zimevuliwa kupita kiasi.
Mjadala mzima umejaa utata wa kitamaduni.
Sekta ya ufugaji ardhini imebadilika kote ulimwenguni kwa mfano Nguruwe, ameonesha kuwa na akili kwa hivyo kuna tofauti gani kati ya kiwanda cha nguruwe kinachozalisha sandwich na pweza wa kiwandani kuwekwa kwenye sahani ya kawaida ya Kihispania?
Wahifadhi wanasema hisia za wanyama wengi wanaofugwa hazikujulikana wakati mifumo yenye nguvu ilipowekwa na makosa ya zamani hayapaswi kurudiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kwa sababu nguruwe wamefugwa kwa miaka mingi, tuna ujuzi wa kutosha kuhusu mahitaji yao na tunajua jinsi ya kuboresha maisha yao, tatizo la pweza ni kwamba hatujui ni nini hasa wanachohitaji au jinsi gani tunaweza kuwapa maisha bora."" anasema Dk Lara.
Anamalizia kwa kusema kuwa Pweza ni viumbe tata sana na kama wanadamu tunapaswa kuheshimu ikiwa tunataka kuwafuga au kula."















