Mwalimu wa Finland aliyewafunza kisiri watoto wa IS nchini Syria

Ilona Taimela sitting at her laptop at home

Chanzo cha picha, Elisabeth Tikka

Maelezo ya picha, Ilona Taimela alibuni programu ya kipekee ya kufundisha kwa watoto wa Finland wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Syria

Kila siku ifikapo saa 09:00, Ilona Taimela aliwasalimia wanafunzi wake na kuwaeleza kazi zao.

Utaratibu wake wa kila siku ulidumu takriban mwaka mmoja kutoka Mei 2020 na sawa na walimu wengine wengi alikuwa akifanya kazi kwa mbali.

Tofauti ni kwamba wanafunzi wa Bi Taimela walikuwa wakifundishwa katika kambi ya kuwazuilia IS kaskazini-mashariki mwa Syria - ulimwengu ulio mbali na dawati lake nchini Finland.

Katika jumbe zilizotumwa kupitia WhatsApp, alifundisha masomo kuanzia hisabati hadi jiografia kwa lugha ya Kifini na Kiingereza.

Wanafunzi wake walikuwa watoto 23 wa Kifini wanaoishi katika kambi ya al-Hol, jiji kubwa la mahema kwa watu wanaohusishwa na kundi la Islamic State (IS).

Takriban watu 60,000 wanaishi huko, wengi wao wakiwa wanawake na watoto kutoka mataifa kadhaa, ikiwemo Ulaya.

Baadhi ya watoto hao walikuwa wanafunzi wa Bi Taimela.

"Haijalishi mahali popote walipo, watoto wana haki ya kupata elimu," aliambia BBC.

Short presentational grey line

Kabla ya masomo ya Bi Taimela, wangeweza tu kupata elimu isiyo rasmi katika shule za muda zinazoendeshwa na mashirika ya misaada.

Kufuatia kushindwa kwa IS nchini Syria mwanzoni mwa 2019, kambi hiyo ikawa gereza lao na vikosi vinavyoongozwa na Wakurdi vinavyoungwa mkono na Marekani kuwa wasimamizi wao wa gereza.

Kwa miaka mingi watoto wa mataifa yote wamekuwa wakizuiliwa huko nchi zao zikitathmini hatari za usalama za kuwarejesha nyumbani, kwa kuhofia kuwa huenda bado wako katika msukumo wa itikadi kali.

Hata hivyo, watoto hao wamekuwa wakikulia katika hali mbaya, inayolaaniwa kuwa ni ukatili na makundi ya kutetea haki za binadamu.

Mwishoni mwa mwaka wa 2019, serikali ya mseto ya mrengo wa kushoto ya Finland ilisisitiza wazo la kuwarudisha nyumbani watoto 30 wa nchi hiyo kwenye kambi hiyo.

Hatua hiyo yenye utata iligusa mshipa wa kisiasa na kufichua utata wa kisheria wa kuwatenganisha watoto na mama zao. Ili kutatua tatizo hili, serikali ilimteua mjumbe maalum, Jussi Tanner, ambaye aliongoza mazungumzo na mamlaka zinazoongozwa na Wakurdi zinazosimamia kambi hiyo.

Mchakato huo ulikuwa mgumu. Kadiri wiki zilivyogeuka kuwa miezi, Bw Tanner alianza kuzingatia hatua za muda za kulinda haki za watoto hawa chini ya sheria za Finland.

Wakati janga la Covid-19 lilipolazimisha shule kufungwa mnamo Machi 2020, Bw Tanner alipata wazo. Ikiwa wanafunzi wangeweza kufundishwa kwa mbali nchini Finland, je, mbinu hiyo inaweza kutumiwa kuwafundisha watoto wa Kifini wanaozuiliwaa al-Hol?

Kambi ya al-Hol camp nchini Syria

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Takriban watu 60,000 wanazuiliwa na vikosi vinavyoongozwa na Wakurdi katika kambi ya al-Hol kaskazini mwa Syria.

Serikali ya Finland iliunga mkono wazo hilo na kuagiza Wakfu wa elimu wa Lifelong Learning kuunda programu ya kufundisha wanafunzi walio mbali.

Wakfu huo ulikuwa na na mtu mahsusi wa kutekeleza programu hiyo kupitia Bi Taimela, ambaye ana uzoefu katika ufundishaji wa tamaduni nyingi.

Aliwasiliana na Tuija Tammelander, mkuu wa shule ya masafa ya wakfu huo.

Ndani ya wiki chache, Bi Taimela na mwalimu mwingine walikuwa wamebuni mtaala wa kitaalam. Kwa kuwapatia watoto mafunzo ya kila siku, alilenga kuboresha ujuzi wao katika masomo ya msingi na kuwatayarisha kwa maisha nchini Finland.

Cha kushangaza, mtandao wa kijamii wa WhatsApp ndio ulikuwa njia pekee ya mawasiliano kati yake na wanafunzi wake.

"Hatukuwa tumewahi kufanya kiti kama hiki tena," asema Bi Tammelander, ambaye aliashiria mpango huo unaweza kuwa wa kwanza wa aina yake.

Wanafunzi waliweza tu kushiriki kwa idhini ya mama zao, ambao waliwasiliana na Bi Bw. Tanner.

Baada ya kupata idhini ya wazazi wa watoto 23, ujumbe wa kwanza ulitumwa Mei mwaka jana.

Short presentational grey line

"Habari za asubuhi! Leo ni Alhamisi tarehe 7 (tarehe saba) Mei 2020. Siku ya kwanza ya shule ya masafa!," ujumbe wa kwanza ulisema.

Aliumia picha akiwa amevalia miwani ya jua na kufunga kitambaa kichwani na kuonekana mwenye kubwa. Alijitambulisha kama Saara, jina la kisiri ili kulinda utambulisho wake.

Ilona Taimela

Chanzo cha picha, Ilona Taimela

Ilona Taimela's message

Chanzo cha picha, Ilona Taimela

Baadhi ya jumbe zake ziliandikwa kwa Kifini na kwa baadhi ya kazi, emoji zilitumiwa badala ya picha zinazotumia data nyingi.

Lugha ya Kifini na hisabati iliunda msingi wa mtaala wake, ambao ulirekebisha mgawo kulingana na umri na uwezo wa kila mtoto.

Bi Taimela alisema alishuhudia uelewa wa watoto ukiimarika kadri muda ulivyosonga. Hatimaye, mtoto mmoja mwenye umri wa miaka sita angeweza kusoma hadithi kwa Kifini, huku wanafunzi wakubwa wakiweza kufahamu vipengele tata zaidi vya lugha.

Screen shots of lessons taught on WhatsApp
1px transparent line
Screen shots of lessons taught on WhatsApp
1px transparent line
Screen shots of lessons taught on WhatsApp
1px transparent line

Uelewa wa watoto ulitokana na ushirikiano na mamia ya ujumbe wa maandishi na sauti. Kwa sababu akina mama hao walipigwa marufuku kumiliki simu za rununu, jumbe hizi zilibidi zifichwe ili zisipatikane na mamlaka ya Wakurdi na umma wa Finland.

Bado, Bi Taimela alishuku walinzi walizipata. Wakati mwingine, akina mama hawakujibu kwa wiki, na kuongeza wasiwasi juu ya usalama wao.